CCM ni Lazima Tuwe Accomodative Kwenye Katiba Mpya

CCM ni Lazima Tuwe Accomodative Kwenye Katiba Mpya

Joined
Apr 27, 2006
Posts
26,584
Reaction score
10,400
- Sio siri kwamba CCM tuna nafasi kubwa sana ya Kuandika Katiba mpya kwa sababu ndicho Chama kinachokubalika sana na Wananchi wengi na ndio chama tawala chenye nafasi kubwa na Mabaraza ya katiba. Lakini kama tusipokuwa makini tunaweza kujikuta tukipigana na kivuli chetu wenyewe, kwenye Siasa za kisasa ni muhimu sana kuwa Accomodative, kwa maana ya kwamba na sisi CCM tunahitaji kukubali kuchukua some bullets katika Katiba mpya hasa kwenye areas za Mgombea binafsi na Mawaziri kutokuwa Wabunge. CCM hatuwezi kuathirika na hizi hoja mbili infact zitatusaidia sana kujiimarisha na kuondokana na wasaliti wengi ndani ya chama chetu ambao ndio chanzo cha CCM kupoteza nafasi nyingi za ubunge uchaguzi uliopita.

1. MGOMBEA BINAFSI:- Pamoja na kwamba ni hoja inayoonekana kutisha sana, lakini ukweli ni kwamba ni hoja ambayo itawaumiza sana Wapinzani kuliko CCM, itatusaidia sana kuwapunguza waroho wa madaraka ndani ya Chama chetu, na ni guarantee kwamba wakisha jitosa huko hawatakuwa na future ya kisiasa zaidi tu ya kukwama hapo hapo watakapokuwa na mwisho sana wa safari yao itakuwa ni ubunge tu!!

- The Fear kwamba mgombea binafsi anaweza kushika urais ni ndoto ya mwendawazimu, hakuna kiongozi mwenye akili timamu anayeweza hata kuthubutu hilo na ndio maana wale wanaodaiwa kuwa miamba wa kugombea urais 2015 ndani ya CCM hakuna hata mmoja wao anayeweza kuthubutu kutoka CCM, maana wanajua nje ya CCM hawana ubavu. Tanzania ni kubwa sana kwa mgombea binafsi kuifikia kila kona ya Tanzania ili aweze kuchaguliwa kuwa Rais, ni CCM pekee yake kama chama ndio kina hiyo luxury ya kuwepo kila kona ya Taifa hili, hata Wapinzani hawajalifikia hilo kuna Wilaya nyingi sana za hili Taifa Wapinzani hawapo kabisa. Kwa hiyo kwa kuikubali hoja ya Mgombea binafsi CCM tutajipa nafasi kubwa sana ya kuondokana na mamluki ndani ya chama chetu!

2. MAWAZIRI KUTOKUWA WABUNGE:- Itatusaidia sana CCM kupunguza mifarakano yetu ya wakati wa kura za maoni na rushwa wakati wa uchaguzi. Waziri asiye Mbunge bado anawajibika kusimamia ilani ya chama kinachotawala kwa hiyo hana uhuru mkubwa sana kwa sababu bado ataitwa kwenye Vikao vya CCM kujibu maswali ya kwanini hatekelezi ilani ya Serikali ya CCM iliyomuajiri. Itaondoa kabisa magomvi makubwa sana ndani ya CCM sasa hivi ambayo yamesababisha Wapinzani kushika nafasi nyingi za ubunge nchini.

- Pamoja na kwamba CCM tuna nafasi kubwa sana ya kuiandika katiba mpya ni muhimu sana tukawafikiria na wasiokuwa na huo uwezo na pia kujiwekea nafasi nzuri ya kutawala taifa hili kwa miaka mingi sana ijayo ni muhimu sana tukachukua risk ya hizo hoja mbili, CCM tuna Katiba mpya mbele yetu, ndio the only tool we have katika kujipanga kujiweka sawa na kutawala kwa miaka mingi sana hili taifa!

KIDUMU CHAMA TAWALA! KIDUMU CCM!

Le Mutuz
 
le mutuz siasa za msimu uchaguzi ukipita na wewe unapotea nchini na mitandaoni:kev:
 
Utumbo!!!!!! By the way suala la katiba mpya lilikuwa katika ilani ya uchaguzi ya CHADEMA!!! Ninyi magamba mmeparamia tu ilani ya chadema!!
 
Heee, Le Mutuz hivi kumbe we ni mtu hatari kiasi hicho. We intend to have KATIBA YA WANANCHI wewe unaongelea kuwa na Katiba ya CCM,,,nimegundua kwa nini umekuwa ukimwagwa katika Chaguzi nyingi. Please badilika angalau katika hili tu. TUNATAKA KATIBA YA TANZANIA NA WATANZANIA na si KATIBA YA CCM na watawala...He umenishangaza
 
Mkuu Le Mutus,
Kwanza nakupongeza kwa kuwa very frank kwenye issue za maslahi ya taifa!.
Nakuunga mkono kwa 100% kuwa the wind of change is sweeping across Tanzania, kama CCM isipochange to the direction of that wind, itazolewa na kupotezwa na hizo changes!. The only way for CCM to survive, is to change before changes changes it!.

Japo na mimi ni CCM ila mimi ni CCM con temporary, tunaotaka CCM ya mabadiliko. Nakiri CCM kuendelea kutawala nchi hii kwa miaka mingi ijayo japo sio kutawala milele kama unavyoamini wewe, bali CCM itaanzwa kutikiswa ni kipindi kifupi kichacho kwa sababu mpaka uchaguzi wa 2015, CCM bado itakuwa inatambia ule mtaji wake mkubwa wa ignorance ya Watanzania na umasikini uliotopea, kiasi kwamba ukigawa tuu T-shirt na kofia na ile shibe ya siku moja, kura unazilamba!.

Kadri miaka inavyokwenda wale ma ignorants wanaichagua CCM kwa ignorance yao, watapungua na kuanza kuerevuka, huku umasikini ukipungua, kufikia bei ya kura sio tena t-shirt, kofia na shibe ya siku moja!. Hapa sijawahesabu wale wanaochagua CCM kwa informed decisions ambao ni wachache, wengi wanaichagua kwa mazoea tuu, na wanazidi kupungua huki kikiibuka kizazi kipya ambacho hakina mazoea na CCM!.

Tukifika stage hizo, CCM nayo ili iendelee kutawala, lazima ibadilike kwa kufanya siasa za ukweli badala ya hizi za hadaa kama ahadi za maisha bora kwa kila Mtanzania, kumbe ni maisha bora kwa baadhi tuu ya walala hai na walala heri na sio walalala hoi, kwa wenye nacho au walionacho wakizidi kuongezewa na huku wale akina sisi, tusianacho na wasio nacho wakinyang'anywa hata kidogo walichonacho kama ilivyo kwa wana Mtwara, baada ya kukopwa korosho zao, gesi yao pia tunawanyang'anya!.

Tena CCM tushukuru sana, tutaendela kutawala kutoka na kukosekana kwa mbadala makini. Japo Chadema imeonyesha njia, ila bado haijafikia kiwango cha kuwathibitishia Watanzania kuwa wameiva na kukomaa kufikia kiwango cha kuwakabidhi nchi come 2015!, ila kwenye baadhi ya maeneo mengi tuu, CCM tukubali, tukatae, tutake tusitake, hata tufanye nini, tutapigwa chini!.

Nakufuatilia you doing a good job huko Wazazi, na nimesikia fununu kuwa unatarajia kukiondoa kile kibajaji chenye mdomo mchafu pale Mtera. Naomba nikitakie mafanikio mema kwa sababu kwa low literacy level ya Dodoma na level ya umasikini uliotopea, Dodoma itaendelea kuwa a strong hold ya CCM kwa miaka mingi ijayo, hivyo ukiweza tuu kufanikiwa kumuweka kando kibaji kwenye vikao vya ndani vya uteuzi, then for sure, 2015, wewe ndie mbunge wa Mtera, na kama ungejiunga na "ile kambi!", hata unaibu waziri wa diasphora unaweza kuukwaa kama mawaziri wataendelea kuwa wabunge.

All the best.

Pasco.
 
Katiba sio ya CCM ,CMD WALA CUF ni ya wananchi kama ccm mpo 6m je watanzania tupo wangapi?? Acha kufikiria kwa kutumia tumbo .umepewa kichwa na mwenyezi mungu ili ukitumie vizuri ............
 
Mkuu Le Mutus,......
.........,
....then for sure, 2015, wewe ndie mbunge wa Mtera, na kama ungejiunga na "ile kambi!", hata unaibu waziri wa diasphora unaweza kuukwaa kama mawaziri wataendelea kuwa wabunge.

All the best.

Pasco.

Duh!
Yani LE MUTUZ Waziri?
Kweli MACCM Kwishney!
 
Walau umetumia akili hapa. Wenzako wamelewa kabisa madaraka na wanaamini kelele za chura hazitawazuia kulala. Kwa sababu mabadiliko yanakuja kwa nguvu sana. Japo matamko hayatawasaidia sana kwa sababu kinachofanya msikubalike sio katiba mpya. Itakapofika point watanzania wakijiona hawana kilichobakia kupotea na ndipo umilele wenu utakapokoma.
 
- Sio siri kwamba CCM tuna nafasi kubwa sana ya Kuandika Katiba mpya kwa sababu ndicho Chama kinachokubalika sana na Wananchi wengi na ndio chama tawala chenye nafasi kubwa na Mabaraza ya katiba. Lakini kama tusipokuwa makini tunaweza kujikuta tukipigana na kivuli chetu wenyewe, kwenye Siasa za kisasa ni muhimu sana kuwa Accomodative, kwa maana ya kwamba na sisi CCM tunahitaji kukubali kuchukua some bullets katika Katiba mpya hasa kwenye areas za Mgombea binafsi na Mawaziri kutokuwa Wabunge. CCM hatuwezi kuathirika na hizi hoja mbili infact zitatusaidia sana kujiimarisha na kuondokana na wasaliti wengi ndani ya chama chetu ambao ndio chanzo cha CCM kupoteza nafasi nyingi za ubunge uchaguzi uliopita.

1. MGOMBEA BINAFSI:- Pamoja na kwamba ni hoja inayoonekana kutisha sana, lakini ukweli ni kwamba ni hoja ambayo itawaumiza sana Wapinzani kuliko CCM, itatusaidia sana kuwapunguza waroho wa madaraka ndani ya Chama chetu, na ni guarantee kwamba wakisha jitosa huko hawatakuwa na future ya kisiasa zaidi tu ya kukwama hapo hapo watakapokuwa na mwisho sana wa safari yao itakuwa ni ubunge tu!!

- The Fear kwamba mgombea binafsi anaweza kushika urais ni ndoto ya mwendawazimu, hakuna kiongozi mwenye akili timamu anayeweza hata kuthubutu hilo na ndio maana wale wanaodaiwa kuwa miamba wa kugombea urais 2015 ndani ya CCM hakuna hata mmoja wao anayeweza kuthubutu kutoka CCM, maana wanajua nje ya CCM hawana ubavu. Tanzania ni kubwa sana kwa mgombea binafsi kuifikia kila kona ya Tanzania ili aweze kuchaguliwa kuwa Rais, ni CCM pekee yake kama chama ndio kina hiyo luxury ya kuwepo kila kona ya Taifa hili, hata Wapinzani hawajalifikia hilo kuna Wilaya nyingi sana za hili Taifa Wapinzani hawapo kabisa. Kwa hiyo kwa kuikubali hoja ya Mgombea binafsi CCM tutajipa nafasi kubwa sana ya kuondokana na mamluki ndani ya chama chetu!

2. MAWAZIRI KUTOKUWA WABUNGE:- Itatusaidia sana CCM kupunguza mifarakano yetu ya wakati wa kura za maoni na rushwa wakati wa uchaguzi. Waziri asiye Mbunge bado anawajibika kusimamia ilani ya chama kinachotawala kwa hiyo hana uhuru mkubwa sana kwa sababu bado ataitwa kwenye Vikao vya CCM kujibu maswali ya kwanini hatekelezi ilani ya Serikali ya CCM iliyomuajiri. Itaondoa kabisa magomvi makubwa sana ndani ya CCM sasa hivi ambayo yamesababisha Wapinzani kushika nafasi nyingi za ubunge nchini.

- Pamoja na kwamba CCM tuna nafasi kubwa sana ya kuiandika katiba mpya ni muhimu sana tukawafikiria na wasiokuwa na huo uwezo na pia kujiwekea nafasi nzuri ya kutawala taifa hili kwa miaka mingi sana ijayo ni muhimu sana tukachukua risk ya hizo hoja mbili, CCM tuna Katiba mpya mbele yetu, ndio the only tool we have katika kujipanga kujiweka sawa na kutawala kwa miaka mingi sana hili taifa!

KIDUMU CHAMA TAWALA! KIDUMU CCM!

Le Mutuz

Haya Ndio Mawazo Huru Ya Will Malecela ...aka ...mzee wa sauti ya umeme nanayemjuwa Mimi.....ukipeleka Mawazo Kama haya ndani ya Chama tunaendelea kujivunia kuwa na mkongwe wa JF kwenye safu za Chama akiwakilisha...

PIA ONGEZENI TUTUNGE KATIBA ISIYOKANDAMIZA WAPINZANIA ...KATIBA RAFIKI...AMBAYO ITATOA FURSA KWA CHAMA CHOCHOTE KUPATA MADARAKA ...NA SMOOTH TRANSITION IELEZEWE KIKATIBA...IE KATIBA IMPE KINGA GAVANA WA BENKI NA VYIMBO VYAKE NA TASISISI KULAZIMISHWA KUIDHINISHA MALIPO YEYOTE KWENYE MWAKA WA MWISHO WA UCHAGUZI...KWA AMRI YA RAIS.....NCHI ZA AFRIKA IMEDHIBITIKA KUWA VYAMA VINGI VIKIONA VINAENDA KUSHINDWA UCHAGUZI ....HUFANYA MASS FRAUD...KWENYE BENKI NA TAASISIS.

TUTUNGE KATIBA AMBAYO INAO UWEZO PIA WA KUKIRUDISHA CCM AU CHAMA CHOCHOTE MADARAKANI PALE KINAPOSHINDWA KAMA US AU UK....TUONDOKANE NA MAWAZO YA KUTUNGA KATIBA YA KUFANYA TUTAWALE MILELE ...HILO SASA HALIWEZEKANI............
ANGALIENI .....MFANO WA UNIP ,KANU ,UPC ...etc...tungependa kwetu tuwe na vyama vyenye nguvu viwili au viatu ambayo CHOCHOTE kinaweza kushindwa ...hapo tutakuwa na demokrasia ya kweli. Na ndoto ya Mwalimu ya kuwa Siku moja tutakuwa na vyama vichache vyenye nguvu itatimia
 
Mtu yeyote anaefikiria CCM itawale tena juu ya miaka 50 iliyokwisha tumia, na faida zake ni viwanda kufa, epa, Richmond, mikataba ya siri utazani viungo vya binadamu, elimu duni, umaskini, afya feki yaani bado viongozi wetu wanakimbilia ulaya kwenda kutibiwa, nashukuru Nyerere alifia huko ili aibu ikae vema, utamaduni umeporomoka, nani hajui kuwa wamama au dada zetu sasa wanaenda uchi? skin jeans etc, MTU HUYO AMEKWISHA KUFA ANATAKA AFE NA TANZANIA, kama niko hai sitakubali.
 
Sikujua Kama Wiliam ni mbinafsi kiwango hiki, kweli huwezi hata ona kuwa CCM is a disaster kwa mstakabali wa nchi, au vile mzee anavuta mafao ya kufa mtu unaponea hapo ndo lazima uwe mjinga, ETI watumie fursa hii ya kuandika katiba kuweka mazingira ya CCM kutawala miaka mingi, not when WATANZANIA wameamuka, uhuru wa mawazo sio uhuru wa kusema ujinga mbele za watu, kama unasema kuna rushwa kwenye uchaguzi na eti mtumie fursa ya katiba kuweka hali hiyo vizuri basi wewe ni zuzu, rushwa ambayo ni motto wa CCM utamwondoa kirahisi hivyo CCM ikiwa hai??? kauli ya Hoseah kwetu sisi ni ujumbe mzito kwa CCM, rushwa haiwezi isha au pungua CCM ikiwa Ikulu.
 
Haya umeandika mwenyewe au kuna mtu ameiba password yako?
- sio siri kwamba ccm tuna nafasi kubwa sana ya kuandika katiba mpya kwa sababu ndicho chama kinachokubalika sana na wananchi wengi na ndio chama tawala chenye nafasi kubwa na mabaraza ya katiba. Lakini kama tusipokuwa makini tunaweza kujikuta tukipigana na kivuli chetu wenyewe, kwenye siasa za kisasa ni muhimu sana kuwa accomodative, kwa maana ya kwamba na sisi ccm tunahitaji kukubali kuchukua some bullets katika katiba mpya hasa kwenye areas za mgombea binafsi na mawaziri kutokuwa wabunge. Ccm hatuwezi kuathirika na hizi hoja mbili infact zitatusaidia sana kujiimarisha na kuondokana na wasaliti wengi ndani ya chama chetu ambao ndio chanzo cha ccm kupoteza nafasi nyingi za ubunge uchaguzi uliopita.

1. Mgombea binafsi:- pamoja na kwamba ni hoja inayoonekana kutisha sana, lakini ukweli ni kwamba ni hoja ambayo itawaumiza sana wapinzani kuliko ccm, itatusaidia sana kuwapunguza waroho wa madaraka ndani ya chama chetu, na ni guarantee kwamba wakisha jitosa huko hawatakuwa na future ya kisiasa zaidi tu ya kukwama hapo hapo watakapokuwa na mwisho sana wa safari yao itakuwa ni ubunge tu!!

- the fear kwamba mgombea binafsi anaweza kushika urais ni ndoto ya mwendawazimu, hakuna kiongozi mwenye akili timamu anayeweza hata kuthubutu hilo na ndio maana wale wanaodaiwa kuwa miamba wa kugombea urais 2015 ndani ya ccm hakuna hata mmoja wao anayeweza kuthubutu kutoka ccm, maana wanajua nje ya ccm hawana ubavu. Tanzania ni kubwa sana kwa mgombea binafsi kuifikia kila kona ya tanzania ili aweze kuchaguliwa kuwa rais, ni ccm pekee yake kama chama ndio kina hiyo luxury ya kuwepo kila kona ya taifa hili, hata wapinzani hawajalifikia hilo kuna wilaya nyingi sana za hili taifa wapinzani hawapo kabisa. Kwa hiyo kwa kuikubali hoja ya mgombea binafsi ccm tutajipa nafasi kubwa sana ya kuondokana na mamluki ndani ya chama chetu!

2. Mawaziri kutokuwa wabunge:- itatusaidia sana ccm kupunguza mifarakano yetu ya wakati wa kura za maoni na rushwa wakati wa uchaguzi. Waziri asiye mbunge bado anawajibika kusimamia ilani ya chama kinachotawala kwa hiyo hana uhuru mkubwa sana kwa sababu bado ataitwa kwenye vikao vya ccm kujibu maswali ya kwanini hatekelezi ilani ya serikali ya ccm iliyomuajiri. Itaondoa kabisa magomvi makubwa sana ndani ya ccm sasa hivi ambayo yamesababisha wapinzani kushika nafasi nyingi za ubunge nchini.

- pamoja na kwamba ccm tuna nafasi kubwa sana ya kuiandika katiba mpya ni muhimu sana tukawafikiria na wasiokuwa na huo uwezo na pia kujiwekea nafasi nzuri ya kutawala taifa hili kwa miaka mingi sana ijayo ni muhimu sana tukachukua risk ya hizo hoja mbili, ccm tuna katiba mpya mbele yetu, ndio the only tool we have katika kujipanga kujiweka sawa na kutawala kwa miaka mingi sana hili taifa!

Kidumu chama tawala! Kidumu ccm!

Le mutuz
 
Nimependa ulivyomalizia kwa kusema kuwa katiba mpya IS THE ONLY TOOL CCM HAVE to survive... Unfortunately that tool also is already out of your control...
 
Sipendi siasa za kibinafsi na kimasimango...unang'ata kidogo na kupuliiiza saaaana wakati si ya moto na wala haiumi.

1.Tambua katiba inaandikwa na wananchi na si mafisadi waliotafuna nchi yetu na kujipa matumaini ya kuendelea kutafuna kwa uhakika zaidi.

2.Kumbuka CCM sera zenu na utekelezaji upo kwaajili ya kuwanufaisha wenyewe na si watanzania kwa ujumla-tunalijua hilo.

3.Mtoto wa pimbi ni pimbi tu,hawezi kuwa kuku siku moja akaliwa nyama na watu wakashiba...sisi si vilaza kama walivyo wengi wenu.

Mnatia hasira sana CCM, i wish niwatafune nyama zenu hadi muishe!
 
Nakubaliana na William. Kwa hili la Katiba CCM tusiendelee na kung'ang'ania Ya mwaka 47 na kukataa mabadiliko katika KATIBA AMA sivyo CCM itazikwa na SERIKALI zake Mbili. Hii 21st century ni ya majadilano na makubalano. Wana CCM wasidanganywe na waraka. Watumie bongo ZAO. Hongera kijana wa mwanasiasa shupavu mzee aw WAGOGO Mzee MALECELA. Bravo William and keep it up.
 
Back
Top Bottom