William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,400
- Sio siri kwamba CCM tuna nafasi kubwa sana ya Kuandika Katiba mpya kwa sababu ndicho Chama kinachokubalika sana na Wananchi wengi na ndio chama tawala chenye nafasi kubwa na Mabaraza ya katiba. Lakini kama tusipokuwa makini tunaweza kujikuta tukipigana na kivuli chetu wenyewe, kwenye Siasa za kisasa ni muhimu sana kuwa Accomodative, kwa maana ya kwamba na sisi CCM tunahitaji kukubali kuchukua some bullets katika Katiba mpya hasa kwenye areas za Mgombea binafsi na Mawaziri kutokuwa Wabunge. CCM hatuwezi kuathirika na hizi hoja mbili infact zitatusaidia sana kujiimarisha na kuondokana na wasaliti wengi ndani ya chama chetu ambao ndio chanzo cha CCM kupoteza nafasi nyingi za ubunge uchaguzi uliopita.
1. MGOMBEA BINAFSI:- Pamoja na kwamba ni hoja inayoonekana kutisha sana, lakini ukweli ni kwamba ni hoja ambayo itawaumiza sana Wapinzani kuliko CCM, itatusaidia sana kuwapunguza waroho wa madaraka ndani ya Chama chetu, na ni guarantee kwamba wakisha jitosa huko hawatakuwa na future ya kisiasa zaidi tu ya kukwama hapo hapo watakapokuwa na mwisho sana wa safari yao itakuwa ni ubunge tu!!
- The Fear kwamba mgombea binafsi anaweza kushika urais ni ndoto ya mwendawazimu, hakuna kiongozi mwenye akili timamu anayeweza hata kuthubutu hilo na ndio maana wale wanaodaiwa kuwa miamba wa kugombea urais 2015 ndani ya CCM hakuna hata mmoja wao anayeweza kuthubutu kutoka CCM, maana wanajua nje ya CCM hawana ubavu. Tanzania ni kubwa sana kwa mgombea binafsi kuifikia kila kona ya Tanzania ili aweze kuchaguliwa kuwa Rais, ni CCM pekee yake kama chama ndio kina hiyo luxury ya kuwepo kila kona ya Taifa hili, hata Wapinzani hawajalifikia hilo kuna Wilaya nyingi sana za hili Taifa Wapinzani hawapo kabisa. Kwa hiyo kwa kuikubali hoja ya Mgombea binafsi CCM tutajipa nafasi kubwa sana ya kuondokana na mamluki ndani ya chama chetu!
2. MAWAZIRI KUTOKUWA WABUNGE:- Itatusaidia sana CCM kupunguza mifarakano yetu ya wakati wa kura za maoni na rushwa wakati wa uchaguzi. Waziri asiye Mbunge bado anawajibika kusimamia ilani ya chama kinachotawala kwa hiyo hana uhuru mkubwa sana kwa sababu bado ataitwa kwenye Vikao vya CCM kujibu maswali ya kwanini hatekelezi ilani ya Serikali ya CCM iliyomuajiri. Itaondoa kabisa magomvi makubwa sana ndani ya CCM sasa hivi ambayo yamesababisha Wapinzani kushika nafasi nyingi za ubunge nchini.
- Pamoja na kwamba CCM tuna nafasi kubwa sana ya kuiandika katiba mpya ni muhimu sana tukawafikiria na wasiokuwa na huo uwezo na pia kujiwekea nafasi nzuri ya kutawala taifa hili kwa miaka mingi sana ijayo ni muhimu sana tukachukua risk ya hizo hoja mbili, CCM tuna Katiba mpya mbele yetu, ndio the only tool we have katika kujipanga kujiweka sawa na kutawala kwa miaka mingi sana hili taifa!
KIDUMU CHAMA TAWALA! KIDUMU CCM!
Le Mutuz