Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 790
- 1,316
Kama kunaeneo methali ya "samaki mkunje angali mbichi" inaishi, basi eneo hilo ni eneo la siasa.
Juzi tumemsikia Alli Happy, katibu wa jumuia ya wazazi CCM, kufuatia kurudi kwa Msigwa CHADEMA, akisema kwa jinsi alivyomfahamu Msigwa alijua hawezi kukaa CCM.
Jambo hili ni dhahiri sio kwa Msigwa tu, ila hata kwa matangazo mawili ya hivi karibuni kuwa Selasini aliyekuwa mbunge wa Rombo na Halima Mdee aliyekuwa mbunge wa Kawe wote kurudi CHADEMA.
Kwakifupi tu hawa watu ukiwatazama kwa hulka zao, ni jambo lisilowezekana hata kidogo kuuishi utamaduni wa CCM.
Tafakari; siasa za CCM msingi wake mkubwa ni 'uenzetu' kwamaana ya kuheshimiana, kustahiiana na kukubaliana. Ukigombea CCM, wajumbe hawakupigii kura kwasababu ya hotuba zako bali mahusiano yako nao uliyoyajenga kwa muda mrefu.
Kwamnaofuatili, mtakubaliana na mimi hakuna muhamiaji aliwahi shinda kura za maoni CCM! Wote waliowahi kuteuliwa kugombea hawakupata nafasi hizo kwa kura za wajumbe bali waliteuliwa na kamati kuu.
Sasa unapomchukua mtu kama Msigwa au Mdee, watu waliozoea siasa za harakati za kukosoa na kukashfu, waje waishi huku CCM, mahali ambapo tunafanya siasa za uenzetu, unategemea watatoboa kweli?
Siasa za CCM, zinataka heshma, nidhamu, uenzetu, mtandao na mahusiano ya muda mrefu baina yako na wenzako. Huu ni utamaduni ambao kama hujauzoea basi maisha yako ndani ya CCM yatakuwa magumu sana.