Mkuu Pasco,
Sio kweli kuwa UWT wameweka jicho JF 24/7 nakupa habari yenye uhakika 99% Kuna haja ya kutafuta mbinu nyingine ya kuwafanya washughulike. Hizi tunazopiga hapa ni kelele za Mlango................!
Watanzania tuna tatizo .
japo wengi wanajaribu kurusha mpira kwa watu wa kijijini ,eti waelimishwe kweli mie mtoto wa kijijini nafadhaishwa sana na kauli za namna hii.
Nakubali ,kweli na hakika ni tabia ya binadamu asiye mwelevu(yani mpumbafu) akifikiri yeye ni mwelevu. Binadmu huyu ana tabia ya kuhamisha tatizo ya kwamba lazima tatizo hili nililonalo limesababishwa na fulani na wala si yeye.
fuatilia tu, binadamu mpumbafu hata kama akiwa amebeba bilauli yake ya maji na bahati mbaya akaidondosha na kupasuka ,binadamu mpumbafu lazima atatafuta wa kumtushwa tatizo hilo.mfano mbona umeweka kiti hapa, ama kitambaa hiki ndo kimesababisha .
binadamu mpumafu siko zote hatafuti chanzo cha tatizo, na mara zote atatafuta jibu jepesi kabisa nalo ni kumtwika hilo zigo mtu fulani.
Jamani nawaombeni kwa niaba ya wanakijiji wenzagu ,mtupe kalikizoeti ya kwamba mnataka kutuelimisha,eti ya kwamba sisi ndo chanzo cha matatizo,eti ya kwamba sisi ndo tunaiweka ccm madarakani.
One moment
Lakini nikijaribu kufunua na kuperuzi kumbukukumbu na wanakijiji wenzagu naona kumbukukumbu zinaleta takwimu ya kwamba sisi wavijijini, tusio na elimu tuna historia nzuri ya kupeleka wabunge wa upinzani bungeni ,tofauti na wasomi na watu wa mjini .
Ehe
Sisi wanakijiji tunachojiuliza je tatizo la tanzania ni sisi wanakijiji,tusio na elimu? ama tatizo ni wamjini na wasomi ?
kwanini sisi wa vijijini tunabebeshwa mizigo? je ni kwa sababu hatuna media kama jamiiforums.com ama ITV?
Je tatizo lina mizizi yake i mingine tofauti ila kwa sababu ya upumbafu wa watanzania wote hasa wasomi na wamjini wanajaribu kutafuta jawabu rahisi kuhalalisha upumbafu wao.?