CCM pawaka moto Dodoma

CCM pawaka moto Dodoma

Duh! Watu kama Mafisi vile tunangoje Mkono uanguke tusherehekeee, Hauanguki huo washapatana tangu last week Mjengoni, baadaye watakutana Ukumbi wa Pius Msekwa wakitumbuizwa na Hadija Kopa, huku blues kubwa ikitumbuiza, Mzee JSCM akishikilia kiuno cha Mama Sophia Lion, huku RA akiwa na Mama yetu wa Same, Sekurakamba aking'ang'ania kiuno cha Manyanya aah Blues tamu hilo huku wakingongeana Shampeni na kutakiana maandalizi mema ya Uchaguzi ujao
 
Hivi ndugu yangu kilewo... ndio taratibu za chama chenu kutoa kila siri za kikao? au ni vipi?
DE N, unaweza usiwe utaratibu, ila minyukano inayoendelea inawakela, namtakia kila la heri katika harakati zake za kutujuza.......leta nyeti Kilewo.
CCM ifie mbele
 
Hivi ndugu yangu kilewo... ndio taratibu za chama chenu kutoa kila siri za kikao? au ni vipi?

Naona huyu ni member mpya! (Join Date: Tue Feb 2010, Posts: 12, Thanks: 0, Thanked 3 Times in 2 Posts) Labda ana nia kubwa ya kutujulisha, au anapima upepo itakuwaje ikitokea!! Ni mawazo tu, tusubiri na kutafakari!!!
 
kuna hatari, huku ndan hakutamaniki kabisa.
mkulu yupo kimya anawaangalia waheshimiwa wanavyotupiana maneno.

naona makundi mawili huku ndani ila kusema kweli kundi la lowasa lina nguvu sana.

muheshimiwa mmoja amesema ili aman ya yerusalem(nadhan anamaanisha Tz) ipatikane inabidi lowasa awajibishwe. la sivyo hata akifa na akamkuta lowasa mbinguni kwa Mungu baba basi atamuomba Mungu ampeleke jehanam kuliko kukaa pepon na lowasa''.

Naomba udahaifu wa mwenyekiti kushindwa kuchukua maamuzi sahihi uendelee kudumu katika huo mkutano.Udhaifu wa rais wetu unaweza kuwa ndiyo ukombozi wa mtanzania...hapo nitaridhia Jk ni chaguo la Mungu!
 
kuna hatari, huku ndan hakutamaniki kabisa.
mkulu yupo kimya anawaangalia waheshimiwa wanavyotupiana maneno.

naona makundi mawili huku ndani ila kusema kweli kundi la lowasa lina nguvu sana.

muheshimiwa mmoja amesema ili aman ya yerusalem(nadhan anamaanisha Tz) ipatikane inabidi lowasa awajibishwe. la sivyo hata akifa na akamkuta lowasa mbinguni kwa Mungu baba basi atamuomba Mungu ampeleke jehanam kuliko kukaa pepon na lowasa''.

Ama kweli. Basi kuna watu wamechoka sana huko Dodoma. Sijui kama aliyesema hivyo anaelewa uzito wa kauli hiyo. Si kila kitu kinafanyiwa mzaha. Basi ni bora tu kuachia ngazi CCM.
 
Mchanga wa macho huo
trick ya jakaya kikwete kuwafanya ccm wendawazimu
subiri hitimisho
 
Hivi ndugu yangu kilewo... ndio taratibu za chama chenu kutoa kila siri za kikao? au ni vipi? naona kila wakibana nyeti zinatoka nje

next time ntawashauri wakafanyie kikao mikese huko

Popote watakapofanyia vikao vyao 'wazalendo' watakuwepo tuu, ... lazima watakuwepo ambao hawatakuwa tayari 'kumpigia magoti bahari' hata kama wanaishi 'ndani' ya kambi ya waabudu sanamu na bahari.

Kilewo, ninyi mnaotuhabarisha ni masikio ya wengi ... wengi tuu, ambao wanapigiwa sauti kubwa ya shangwe wakiwa msibani.
 
Hivi ndugu yangu kilewo... ndio taratibu za chama chenu kutoa kila siri za kikao? au ni vipi? naona kila wakibana nyeti zinatoka nje

next time ntawashauri wakafanyie kikao mikese huko

Mkuu De Novo
TANU hoyeeeeeeeeeeeeee!!!
 
dah! kuna wengine walisha tishiana maisha!!

kusema kweli lowasa ana wakati mgumu sana ila kitakachomsaidia ni kundi lake. wana nguvu sana na pia wanaongea kweli kuliko hawa wengine naona hapa huyu jamaa atasave.

inaonekana mkulu hajui mambo mengi sana maana kuna mazito yanatolewa humu anashangaa tu na kwa hali ya kawaida alipaswa ajue.
 
Duh! Watu kama Mafisi vile tunangoje Mkono uanguke tusherehekeee, Hauanguki huo washapatana tangu last week Mjengoni, baadaye watakutana Ukumbi wa Pius Msekwa wakitumbuizwa na Hadija Kopa, huku blues kubwa ikitumbuiza, Mzee JSCM akishikilia kiuno cha Mama Sophia Lion, huku RA akiwa na Mama yetu wa Same, Sekurakamba aking'ang'ania kiuno cha Manyanya aah Blues tamu hilo huku wakingongeana Shampeni na kutakiana maandalizi mema ya Uchaguzi ujao

Umeitoa kama ngonjera vile lakini ndio ukweli hakuna chochote kitakachobadilika situmeona sakata la Richard Monduli watu walikuwa wanaongea hadi mapovu yanatoka lakini siku ya siku wakanywea kama kuku kanyeshewa mvua
 
imekaa vema, tuombe Mungu awatie nguvu wamaanishe wanachokisema.
ccm ndiyo mwisho wake ddoma hawatoke na chama kipindi hiki dodoma lazima wakivunje chama ila nafuu yao ni lowassa awajibishwe ipasavyo na ripoti ya richmondi ni batili
 
Yaani kwenye hicho kikao hoja ya msingi ni kuhusu Lowassa? mnataka tuaamini kuwa CCM imechafuliwa na Lowassa? Before Richmond CCM ilikuwa safi? I dont think Lowassa ni hoja itakuwa hamtendei haki....the whole system is broken, inatakiwa kusukwa upya....Kuna kashifa za Rada, IPTL, ndege ya Rais, TRC/TRL, ATCL, Kiwira, SUKITA, Buhemba, Williamson, Songo songo, .name it...hizi hazichafui ila Lowassa...
 
Wana JF mbona mnadanganyika kirahisi hivyo? Huyo mtu kama yuko kwenye kikao hawezi kuwa na uwezo wa kutuma ujumbe JF mpaka watoke. Hawaruhusiwi kuwa na simu humo.

Pia suala la tume ya Mwinyi inasemekana lilijadiliwa jana.

Kuna watu wako hapa kudanganya JF.
 
Kwa hiyo matatizo ya nchi nzima kuanzia rushwa mpaka umaskini,foleni,hakuna umeme wala maji,elimu duni etc ni Lowassa,yaani huyu jamaa kishaachia ngazi na hakuna chochote kilichofanyika maana hakuna umeme wala hakuna aliyefikishwa mahakamani,leo still wanaongelea huu utumbo awajibishwe...hawa ni wendawazimu,JUST VOTE THEM OUT lakini seems kwa bongo hilo haliwezekani,tatizo ni wananchi wanaoiweka CCM sio Lowassa kwa hiyo they deserve kila kitu chini ya CCM mpaka watakapo pata akili
 
kwahiyo RA ndio CCM, na CCM ndio RA ?
MIMI naamini LOWASSA ANANGUVU KUBWA KULIKO RA.

Mkuu nguvu hiyo inatoka wapi?, Ana veto power yaani bila kura yake maamuzi hayapiti au vipi?. CCM walikuwepo akina J.K Nyerere, R.M Kawawa jiulize leo wapo wapi? na Chama kipo wapi?. Hakuna mwenye nguvu CCM ziadi ya mwenyekiti wake amabaye ni rais wa jamhuri mwenye mamlaka ya kuamrisha nguvu za dola zitumike. Wengine wote wana nguvu za majungu na kupitisha fitina ambayo wapambe wakiamua kuzikataa hazipiti na wao wanaenda na maji.

JK akiamua CCM itameguka lakini si RA wa EL hawa nguvu zao ni kupitia mwavuli wa mtu wao JK
 
- Briefly, ni kwamba hakuna lolote la maana, hawa kabla ya kwenda huko walikuwa tayari wamekaa kikao cha siri wakakubaliana kwamba wayazime yote ya kero za wananchi mpaka uchaguzi utakapoisha kwa makubaliano kwamba mafisadi hawatagusa majimbo ya wabunge wasio kwenye kundi lao,

- Pia ndani yao kulikuwa na kikundi kimoja kilichokuwa kinataka kuisukuma ishu ya Richimond kupelekea kwenye vote of no confidence kwa Waziri Mkuu na Rais, ambapo wangemlazimisha Rais kuvunja bunge sasa na kuamuru uchaguzi mpya, kunusuru hilo ndio hasa sababu ya makubaliano ya amani kati ya mafisadi na wabunge wengine, kwa kifupi maamuzi ya kueplekea hiki kikao yalikuwa yameshaamuliwa kwenye vikao vya siri kabla ya hiki kikao.

- Kwa kifupi ni kwamba kikao hiki hakikuwa na lolote la maana kwa masilahi ya taifa letu, kilikuwa ni kikao cha kulindana ili kushinda uchaguzi, was the number one priority.

Respect.

FMEs!
 
DE N, unaweza usiwe utaratibu, ila minyukano inayoendelea inawakela, namtakia kila la heri katika harakati zake za kutujuza.......leta nyeti Kilewo.
CCM ifie mbele

sawa, niliuliza tu maana mambo mazito haya
 
Duh,mkuu Field Marshall Es uko wapi? maanake unamwaga dataz mkuu wangu.Hebu rekebisha comrade!
 
Wana JF mbona mnadanganyika kirahisi hivyo? Huyo mtu kama yuko kwenye kikao hawezi kuwa na uwezo wa kutuma ujumbe JF mpaka watoke. Hawaruhusiwi kuwa na simu humo.

Pia suala la tume ya Mwinyi inasemekana lilijadiliwa jana.

Kuna watu wako hapa kudanganya JF.

shauri yako amini hivyo, umechunguza sole za viatu vyao walioko ndani?!

kwa taarifa yako mawimbi ya sauti yanaruka hadi amerika.

NOT EVERY THING YOU SEE IS AS IT IS!!
 
Back
Top Bottom