Manufaa ya uchaguzi ukiwa wa uwazi, huru na wa haki ukijumuisha wote kuanzia mwanzo wa mchakato mzima ni haya katika mfano wake hapa chini:
23 September 2024
New York City
Mahojiano na rais Cyril Ramaphosa kuhusu jinsi 4R zilivyoiinua imani ya wananchi na wafanyabishara ndani ya nchi na wale wawekezaji kutoka nje
JINSI CYRIL RAMAPHOSA ANAVYOTUMIA 4R ZA UKWELI, KAMA ZANA YA KUVUTIA MAENDELEO
View: https://m.youtube.com/watch?v=4gF-YkcFMFQ
Kwa kujivunia kutoka moyoni bila kuwa na ulaghai wa kutumia 4R kuwezesha chama chake pekee kuwa na wabunge 100% bunge la taifa na bunge la majimbo, Mheshimiwa Cyril Ramaphosa wa South Africa anajivunia jinsi ANC ilivyovuna 40 % ya kura huku chama kinachofuatia DA 21 % huku asilimia zilizobaki 39% zimegawana vyama vingine vidogo.
Kupitia 4R za ukweli nchi inaendelea kuwa na mihimili huru ya Bunge, Mahakama na vyombo vya habari.
Hali hiyo imewapa imani wawekezaji wa ndani wana imani kuwekeza zaidi ndani na pia hali hiyo inavutia wawekezaji zaidi kutoka nje.
Kutokana na kuwa na kuaminiana ndani, South Africa imekuwa mfano kwa mataifa dada jirani zilizo nchi za SADC na mbali zaidi.
4R za ukweli zisizo na hila ovu zimemuondolea rais wa South Africa kutokukosa usingizi na kuwaza kutumia majeshi ya usalama kama polisi na usalama wa taifa kuwatishia raia.
kutokana na mazingira mazuri yaliyoletwa na 4R kupitia serikali ya Umoja wa Kitaifa GNU, sana nchi ina nafasi ya kutumia viongozi wa vyama vingine vya kisiasa katika kulitumikia taifa ktk nafasi za kiuongozi na hivyo nchi kufaidika na kila raia aliye na upana wa maono bila kujali wametoka vyama vingine.
Tofauti na kama ingekuwa utawala wa kimabavu, kuzuia raia kufikia nafasi za kiuamuzi kupitia kura walizopata baada ya kuaminiwa na wapiga kura waliowacgagua katika uchaguzi ulio wazi, huru na wa haki kuanzia ngazi ya mchakato wa mikutano ya vyama vyao, kampeni hadi kutangazwa wameshinda.
Source: SABC News
CCM watambue kuwa uchaguzi ulio huru na haki una manufaa makubwa mtambuka, badala ya wao chama dola kongwe kufikiria jambo kubwa ni kuingia ofisini kwa uchaguzi usio wa haki, ulioporwa kwa hila kama ule wa 2019, 2020 kurudiwa tena 2024 na 2025 serikali itakayoingia madarakani kupitia uchaguzi fiche wa hila itapata tabu siyo tu kutoka kwa raia tu bali nchi kukosa maendeleo.