Wakuu
Katibu wa CCM Wilaya ya Rufiji Prudence Sempa amesema atalifanyia kazi Ombi la Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rufiji la kuwataka kumpitisha Mbunge Mohamed Mchengerwa kuwa Mgombea pekee wa Ubunge kupitia CCM.
View attachment 3223700
Bw. Sempa alitoa kauli hiyo baada ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rufiji Abdul Chobo kukitaka Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya kuitisha Mkutano Mkuu wa wanachama na kuangalia vifungu vya katiba vinasemaje ili waweze kumpitisha Mbunge wa sasa wa Rufiji Mohamed Mchengerwa kuwa Mgombea pekee na Rasmi kupitia CCM kwa Jimbo la Rufiji.
View attachment 3223702
Kombo ambaye pia ni moja wa Madiwani aliibuahoja hiyo leo katika Maadhimisho miaka 48 ya CCM yaliyoadhimishwa katika viwanja vya Tanki mbili katika Wilaya ya Rufiji.
==
Maoni ya mdau