CCM, Serikali Mbili Zilizoboreshwa, na Hatima Ya Muungano

Hotuba nzima ya kikwete ili-base kwenye tafsiri ya takwimu na siyo kwenye takwimu yenyewe. Mbona unashindwa kuelewa hili?


Takwimu hazisemi kuwa asilimia kubwa ya watanzania wanataka serikali tatu, hili ni pendekezo la tume kutokana na walivyotafsiri takwimu walizopata. Kwa mfano tu, wanaotaka serikali ya mkataba na wanaotaka serikali tatu asilimia zao zinafanana, sasa utasemaje wanaotaka serikali tatu ni wengi?

Hii ndiyo hoja. Ongelea takwimu, nielezee kivipi umekuja na conclussio kuwa watu wengi wanataka serikali tatu ... concisely plz.
 
Mkuu Mchambuzi yaani natamani nikulipie deni lako la Mkopo wa Elimu ya Juu. Natamani Loan Board wakufutie deni.
 


Umekosa majibu kwa swali langu la msingi kabisa juu ya framework unayotumia ku analyse and arrive kwenye hitimisho kwamba serikali moja ni gharama nafuu kuliko tatu. Nimekuelimisha how and what you need to do before arriving to any conclusion, unaita haya ni political antics.
Maana ya antics ni "foolish or outrageous". Inawezekana ukawa sahihi lakini najua wapo wanaoelewa naeleza nini, na wanaona jinsi gani unakimbia hoja ya msingi.

Kukimbilia wizara zipo ngani, zitakuwa ngapi, ni low thinking kwani kabla ya kujadili wizara, lazima ujue unataka ku achieve nini, na pia central gvnt itakuwa efficient katika mambo yepi na the two constituent parts zitakuwa efficient na sehemu zipi na kukusanya na kutumia kwa faida ya wananchi. Nimeelezea haya huko juu, masuala ambayo yakipatiwa majibu ndio suala la wizara, idara, yanakuja, unaita hizi ni foolish political arguments.

Mfumo wetu unahitaji a major ovehaul - mfumo wa public finance. Na hili linajadiliwa hata kwenye academic and donor cycles. Mfumo wetu wa bajeti ni mbovu, upo structured kuhudumia siasa kuliko uchumi na jamii. Huko juu nimegusia kidogo what can be done kusogeza serikali kwa wananchi, kwa kuwa na constituent political units with fiscal autonomy, huku central government ikikabiliana na maeneo machache ambayo ipo more competent. Unaita haya ni "foolishness".

Hauwezi jenga hoja kwamba serikali moja, mbili au tatu ni nafuu kwa kwenda kuchimba content ya bajeti kama unavyofanya. Inatakiwa uangalie mfumo mzima wa public finance, and intergovernmental fiscal relationships. Nimekueleza kwamba haya yanahitaji kuwekwa in an analytical framework ambayo itasaidia kufikia conclusion mfumo upi ni nafuu. Nikakueleza kwamba naandaa uzi maalum, kwa sasa ntakupa tu highlights. You describe it as politically outrageous.

Let me tell you something - hauna uelewa na masuala ya uchumi, wala public finance. Mbaya zaidi, hauna interest ya kujifunza. Kama una uelewa basi ni wa kukaririshwa. Mjadala wa kuangalia bajeti ya sasa kama kigezo cha kujenga hoja kwamba hakuna pesa, hiyo mijadala ni yenu wachumi uchwara pamoja na kina mwigulu. Matatizo mliyoyajenga kimfumo mnayalazimisha yawe kikwazo kwetu sote.

Nikimaliza uzi wangu juu ya kwanini serikali tatu ni nafuu, ntakualika uje. Na kama utakavyoona, suala la bajeti litakuwa ni suala very marginal. At the centre nitajadili serikali ipi katika ya ile kuu na shiriki zipo more competent in allocation, distribution and macro economic stability. Haya ndio yana determine muundo wa public finance, gharama kwa mwananchi, na hatimaye bajeti.

Until then, let me remain foolish.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 

Kwani ccm munapong'ang'ania serikali 2 mumutumia takwimu zipi? Kwa mtu yoyote anaejua asili ya serikali mbili tunafahamu ni maoni ya watu wawili Nyerere na Karume na hakuna historia inaonesha kwamba kuna mtu zaidi ya Karume na Nyerere walitoa maoni juu serikali mbili. Sasa kama Tume ya Warioba imekuja na idadi ya watu elfu 17 wanaotaka serikali tatu, inakuaje watu wawili Karume na Nyerere wawe wengi kuliko watu elfu 17?.
Warioba kaja na maoni ya wananchi wanaotaka serikali 3, sasa CCM maoni ya Serikali 2 wamekusanya wapi au tume ipi?
 
Huwezi kujenga hoja based on hearsay au political probability katika mazingira halisia.

Unachokifanya ni sawa na kudanganya wanaJF kuwa haya ni mapendekezo ya CCM kama vile CCM haina official channels katika mawasiliano na wanachama wake au wananchi.

Jenga hoja based on what is on political table na siyo hisia kwa misingi ya kufurahisha nafsi. Hakuna mbunge wa Bunge Maalum aliyetoa bungeni mapendekezo ya CCM kuhusu kile unachokiita "Serikali mbili zilizoboreshwa".

CCM haijatoa mapendekezo zaidi ya mapendekezo iliyotoa kwenye Tume ya Katiba kama taasisi.

Mnatumia muda mwingi kuainisha mapungufu ya serikali mbili wakati wananchi wanayafahamu kwa kuyaishi kwenye mfumo huo, lakini mnashindwa kutetea hoja za serikali tatu kama zinaweza kusimama na kuufanya Muungano uimarike zaidi katika mazingira ya extreme unbalanced economically, politically and socially.

Waelezeni wananchi jinsi mgawanyo wa uchangiaji wa Muungano katika serikali tatu utakuwaje. Ratio gani itatumika katika kuchangia.

Waambieni wananchi, gharama za muungano wa serikali tatu ni zipi na zitalipwa vipi katika mfumo wa serikli tatu kwa maana kuwa, serikali ya Tanganyika italipa % ngapi na serikali ya Zanzibar italipa % ngapi.

Waambieni wananchi kama gharama za Muungano zitapungua au kuongezeka.

Kuna contingency plan gani katika kukabiliana na athari za serikali moja kushindwa kuchangia kutokana na hali ya kisiasa ilivyo katika Taifa hususani Zanzibar.

Mgawanyo wa madeni ya nje katika serikali tatu utakuwa katika ratio zipi?.

Mkiambiwa kuanisha hoja za serikali tatu katika uhalisia mnaanza kuuliza tena maswali ya namna utendaji wa serikali mbili unavyofanyika wakati tayari mmeshasema muundo wa serikali mbili haufai, kwa maana kuwa mnaufahamu vizuri.

Kama muundo wa serikali mbili mnaufahamu, kwa nini tena mnaanza kuuliza maswali kuhusu Muundo na gharama zake. Au ndiyo yale yale ya kusema unafahamu wakati hata hufahamu!.

Ninyi mmesema Muundo wa serikali tatu utakuwa wa wazi na kila kitu kitafahamika, tuambieni basi hizo ratio kabla hatujafanya maamuzi ya kuachana na Muundo wa Serikali mbili.

Guys, You are so desperate to outperform two tier government in a dobious distinction.

Nimalizie kwa kuweka andiko la Judge Warioba kama unaamini alichokisema kwenye hotuba katika bunge la Katiba on 18th March 2014 aliposema, Hapa hatujafahamu hata gharama za serikli ya Tanganyika ambapo kuna uwezekano wa kuwa na Wabunge wawili wawili tena kutoka kwenye kila jimbo la uchaguzi katika bunge la Tanganyika,avhilia mbali wabunge wawili wawili wa bunge la Muungano kwa maana nyingine, kila jimbo la Uchaguzi litakuwa na wastani wa wabunge wanne wanne.
 
Tume hiyohiyo ya Warioba.
Usipende kufuata upepo, angalia halafu utoe maamuzi au maoni.
Yaani wewe kichwani mwako umejazwa maoni kuwa kila mtu asiyetaka serikali tatu, basi anataka serikali mbili. Brazil ina serikali 1100 na zina nguvu.
 
Utaziboresha vipi?
Jee wabunge wa znz watoke zikijadiliwa mfano budget za kilimo
Maji
Miundo mbinu
Elimu
Ufugaji nk ambazo hazina uhusiano na kwao?
Jee wao kushiriki kujadili bill zinazohusu tanganyika jee watoke?
Jee wanavo pendekeza rais wa znz awe makamo ikitokea marais hao wametoka vyama tofauti tunajua madhara yake? Ni rais atarithi wa chama kingine
Ili kuleta usawa katika mambo ya uchumi lazima sera ya fedha ibadilike..aidha znz wawe na currency yao
au shilingi iendelee lakini znz wawe na bank kuu yao na wawe na ruhsa ya kuprint note zao ikibidi kufanya hivo(scortland wanafanya hivyo)
Au njia nyengine ni kuifix fedha yetu na currency kubwa kama dolla au euro yaani iwe pegged hivyo kusiwe na devaluation ambayo inadhiofisha uchumi wa znz kila mwaka.
Kuna mengi ya kufanya ambayo ccm hawatokubali kwani hawana nia nzuri na znz na pia vibaraka wao ccm unguja wapo wapo tu kama mazumbukuku
 
Tume hiyohiyo ya Warioba.
Usipende kufuata upepo, angalia halafu utoe maamuzi au maoni.
Yaani wewe kichwani mwako umejazwa maoni kuwa kila mtu asiyetaka serikali tatu, basi anataka serikali mbili. Brazil ina serikali 1100 na zina nguvu.

Serikali 3 ndo mpango mzima hata musipotaka tutawalazimisha tu na mutanyooka tu. Kwanza tunataka Tanganyika yetu kwa lazima. Kama ccm hamtaki Tanganyika hamieni Rwanda.
 
Nikaambiwa mbona zake zinafanana na Afrobarometer? ... nikaleta link ya Afrobarometer inayoonyesha 14% ndiyo wanaotaka serikali 3 according to the same Afrobarometer.

Mbona unaleta takwimu nusu nusu. Vipi kuhusu utafiti wao mwaka 2013 ambapo wananchi waliulizwa kuhusu serikali tatu POINT BLANK - na majibu yakawa hivi (tembelea tovuti husika):

*Strongly agree 26pct
*Agree 25pct
*Disagree 22pct
*Strongly Disagree 26pct

Tunachoona hapa bado takwimu hizi zipo consistent na za tume, hence za tume kuwa more valid, reliable, replicable kuliko zako na za Kikwete kwani:

Wanaounga mkono serikali tatu hapo juu ni: 26 + 25 = 51%

Wanaopinga ni 22 + 26 = % 48%

Sasa kwa vile unapenda sana kujadili kundi la wasiopenda serikali tatu, na ni mzuri sana wa kucheza na numbers, ebu tusaidie au Kikwete atueleze katika hiyo 48% ni wangapi wanataka serikali mbili, wangapi serikali moja?




Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Utaziboresha vipi?
Jee wabunge wa znz watoke zikijadiliwa mfano budget za kilimo
Maji
Miundo mbinu
Elimu
Ufugaji nk ambazo hazina uhusiano na kwao?
Jee wao kushiriki kujadili bill zinazohusu tanganyika jee watoke?
Jee wanavo pendekeza rais wa znz awe makamo ikitokea marais hao wametoka vyama tofauti tunajua madhara yake? Ni rais atarithi wa chama kingine
Ili kuleta usawa katika mambo ya uchumi lazima sera ya fedha ibadilike..aidha znz wawe na currency yao
au shilingi iendelee lakini znz wawe na bank kuu yao na wawe na ruhsa ya kuprint note zao ikibidi kufanya hivo(scortland wanafanya hivyo)
Au njia nyengine ni kuifix fedha yetu na currency kubwa kama dolla au euro yaani iwe pegged hivyo kusiwe na devaluation ambayo inadhiofisha uchumi wa znz kila mwaka.
Kuna mengi ya kufanya ambayo ccm hawatokubali kwani hawana nia nzuri na znz na pia vibaraka wao ccm unguja wapo wapo tu kama mazumbukuku
 
Nipe link chapchap, mimi nilikupa link ukurasa wa 21.
http://www.repoa.or.tz/images/uploads/Afrobarometer_Round_5_Survey.pdf
 

Karibu katika mjadala. Nianze na hili la Rasimu Mbadala. Nikikuambia ninayo Nakala utasema nimeitengeneza mwenyewe?

Nikikupa audio clips za mkutano wa NEC mwishoni mwa february ambapo asha migiro anasikika anawasilisha hoja, huku wajumbe wakihaha kujadili jinsi gani hayo hayatekelezeki utasema nimechakachua?

Nikukupa audio clips jinsi gani chama kiligawanyika juu ya mapendekez hayo, huku nape baadae akienda danganya umma kwenye press kwamba chama kimetoa msimamo mmoja na ni maboresho ya serikali mbili, utasema nimechakachua?

Na mwisho, kati ya suala na gharama, na lile la zanzibar kuvunja katiba ya muungano, kitendo ambacho kama ingekuwa ccm haipo dominant bungeni, rais wa jamhuri ilitakiwa awe impeached - kipi kina umuhimu zaidi katika justification ya serikali mbili vs tatu? Kwa maana nyingine, iwapo tuna amua to hold gharama factor constant for a second, je how do you solve ukiukwaji wa znz kikatiba, suala ambalo sio ccm, sio serikali ya muungano, na sio jeshi mnalotishia wananchi, wataweza badilisha wazanzibari katika hili?

Tuanze na haya kwanza.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nipe link chapchap, mimi nilikupa link

Natumia simu; just google twaweza, afrobarometer, survey, three governments. Ninazo details book marked kwenye PC, nikirudi mjini na kama hautakuwa nazo bado, I will share.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kwa kutumia takwimu zako, thats a statistical tie.
And since yeye ana bunge ambalo limepewa mamlaka kikatiba na hata kidemokrasia kusimamia mchakato huu, he will be dumb not to gamble with a two-tier.

Atachogombea yeye ni wale 30% wa mkataba kwa kuwapa more autonomy na bara anajua ataikwaa two thirds. Sioni kwanini asi-gamble on that. He will probably get it, ndiyo maana inabidi UKAWA wajitoe kwa sababu they can see that.

La sivyo, mjaribuni kwenye refferrendum, mbona aliwatoa nishai serikali ya shirikisho Zanzibar? Rudini bungeni, cast your vote, tally them and see wus up.
 
Serikali 3 ndo mpango mzima hata musipotaka tutawalazimisha tu na mutanyooka tu. Kwanza tunataka Tanganyika yetu kwa lazima. Kama ccm hamtaki Tanganyika hamieni Rwanda.
Itabidi usubiri.
 
Kwa kutumia takwimu zako, thats a statistical tie.
A statistical tie? Kwanini kwenye takwimu nyingine mnaingiza hoja za 80pct?


Is this still in line na kukubali kwako earlier kwamba trend ya umma inaelekea kutaka serikali tatu?


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Tume imeeleza kuwa hoja ya mkataba haikuweza kutetewa na wahusika. Kama ujuavyo mwasisi wa hoja Maalim na mwenzake Ahmed Rajab hawajaweza kutetea suese mvuvi wa samaki.

Hotuba ya kikwete haikuwa katika kutafsiri takwimu. Ilikuwa kutafuta vifungu vya takwimu vinavyoweza kumtia hatiani Warioba ili atukanwe vilivyo. Hilo amefanikiwa. Kinachosikitisha ni kuwa kilichopo midomoni na akilini mwa wananchi ni hotuba ya Warioba kwasababu ina 'subsatnce' ile ya mwenyekiti ni hocus pocus Kobello.

Warioba hana conclusion, Mchambuzi amekueleza ni indicator za kufanyia kazi. Wenye conclusion ni wananchi.
Hilo lingewezekana kwa wananchi kupewa fursa ya kuangalia rasimu na ku prove kuwa ni wrong au right.
CCM wameogopa wanataka kutengeneza rasimu yao ikiwa na sample ya watu 400, tena wakiwa wamefungwa midkono na midomo kwa pamba.
 
Kwanza nianze kwa kusema, huwa ninasikitika sana kuona mwanaJF anapata hukumu kwa kukiuka taratibu na sheria za JF. Nani amekuambia kama mimi ni Mwigulu. Mimi ni MwanaDiwani. Naomba uondoe hilo jina kwenye mwanzo wa post yako. Kukimbilia kutafuta real ID's za wanaJF ni dalili mojawapo ya kukosa hoja na kutafuta personal attack.

Pili, Mbona unaanza kunitafutia majibu?. Mbona unaanza Pre-emptive strike and defence?.

Jamiiforums is Where we Dare to Talk Openly! Weka hapa hizo audio au documents kwanza kabla hatujaingia kifikra pevu kwenye hoja zako ili uisaidie hoja yako kusimama na pia uwasaidie wanaJF wengine. Achana na hoja za kusema nitasema hiki au kile kabla hata ya kile unadai kipo hujakiweka juu ya meza.

Rasimu mbadala haiwezi kuwa ni kipande cha karatasi kimoja bali lazima iwe na kurasa za karatasi ya A4 zaidi ya makumi kama siyo mamia.
 
Labda utufahamishe, kama Rais ana mandate kwa kupitia bunge kwanini asipeleke mswada wa marekebisho ya katiba ya 1977 ambayo ana mamlaka nayo. Kwanini kuunda tume.

Pili, kama bunge linaweza kuandika rasimu mbadala na kuwapa wananchi, maoni ya wananchi yalikuwa ya nini.

Tatu, lazima uelewe the whole process is flawed. Endapo JK ana mandate ya bunge na majority ya bunge anachoogopa rasimu kwenda kwa wananchi ni kitu gani?

Nne, Rais kama alijua kuna uwezekano wa lolote kutokea ambalo halikubaliani na matakwa yake ni kwanini aliunda tume na ili tume ifanye kitu gani cha kumsaidia katika adhama yake.

Tano, katiba haiandikwi kwa uchama. Huo ni umasikini wa akili ambao ni mkubwa kuliko wa fedha.
KANU haipo tena Kenya, wala UNIP haipo Zambia. Kenya ipo na Zambia ipo. Kufikiria majority ya chama na siasa za uchama ndicho chanzo cha umasikini wa nchi. Kama hatutabadilika tutaendelea kuwa masikini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…