Huwezi kujenga hoja based on hearsay au political probability katika mazingira halisia.
Unachokifanya ni sawa na kudanganya wanaJF kuwa haya ni mapendekezo ya CCM kama vile CCM haina official channels katika mawasiliano na wanachama wake au wananchi.
Jenga hoja based on what is on political table na siyo hisia kwa misingi ya kufurahisha nafsi. Hakuna mbunge wa Bunge Maalum aliyetoa bungeni mapendekezo ya CCM kuhusu kile unachokiita "Serikali mbili zilizoboreshwa".
CCM haijatoa mapendekezo zaidi ya mapendekezo iliyotoa kwenye Tume ya Katiba kama taasisi.
Mnatumia muda mwingi kuainisha mapungufu ya serikali mbili wakati wananchi wanayafahamu kwa kuyaishi kwenye mfumo huo, lakini mnashindwa kutetea hoja za serikali tatu kama zinaweza kusimama na kuufanya Muungano uimarike zaidi katika mazingira ya extreme unbalanced economically, politically and socially.
Waelezeni wananchi jinsi mgawanyo wa uchangiaji wa Muungano katika serikali tatu utakuwaje. Ratio gani itatumika katika kuchangia.
Waambieni wananchi, gharama za muungano wa serikali tatu ni zipi na zitalipwa vipi katika mfumo wa serikli tatu kwa maana kuwa, serikali ya Tanganyika italipa % ngapi na serikali ya Zanzibar italipa % ngapi.
Waambieni wananchi kama gharama za Muungano zitapungua au kuongezeka.
Kuna contingency plan gani katika kukabiliana na athari za serikali moja kushindwa kuchangia kutokana na hali ya kisiasa ilivyo katika Taifa hususani Zanzibar.
Mgawanyo wa madeni ya nje katika serikali tatu utakuwa katika ratio zipi?.
Mkiambiwa kuanisha hoja za serikali tatu katika uhalisia mnaanza kuuliza tena maswali ya namna utendaji wa serikali mbili unavyofanyika wakati tayari mmeshasema muundo wa serikali mbili haufai, kwa maana kuwa mnaufahamu vizuri.
Kama muundo wa serikali mbili mnaufahamu, kwa nini tena mnaanza kuuliza maswali kuhusu Muundo na gharama zake. Au ndiyo yale yale ya kusema unafahamu wakati hata hufahamu!.
Ninyi mmesema Muundo wa serikali tatu utakuwa wa wazi na kila kitu kitafahamika, tuambieni basi hizo ratio kabla hatujafanya maamuzi ya kuachana na Muundo wa Serikali mbili.
Guys, You are so desperate to outperform two tier government in a dobious distinction.
Nimalizie kwa kuweka andiko la Judge Warioba kama unaamini alichokisema kwenye hotuba katika bunge la Katiba on 18th March 2014 aliposema,
167. Kwa maana hiyo, Muundo wa Serikali tatu utakuwa na changamoto zake. Moja ni gharama kuongezeka. Ongezeko hilo halitakuwa kubwa sana kama inavyofikiriwa. Gharama kubwa kwa shughuli za Muungano ni katika eneo la ulinzi na usalama, yaani jeshi la wananchi, polisi, usalama wa taifa na mambo ya nje. Gharama hizo hazibadiliki, zinabaki zile zile bila kujali kama ni Muundo wa Serikali Mbili au Serikali Tatu. Gharama zitaongezeka kwenye utawala. Tume ililiona hilo na ndiyo maana imependekeza Serikali ndogo.
Hapa hatujafahamu hata gharama za serikli ya Tanganyika ambapo kuna uwezekano wa kuwa na Wabunge wawili wawili tena kutoka kwenye kila jimbo la uchaguzi katika bunge la Tanganyika,avhilia mbali wabunge wawili wawili wa bunge la Muungano kwa maana nyingine, kila jimbo la Uchaguzi litakuwa na wastani wa wabunge wanne wanne.