CCM, tafuteni namna ya kumshauri Rais Magufuli maana muda mwingine anaumiza sana

CCM, tafuteni namna ya kumshauri Rais Magufuli maana muda mwingine anaumiza sana

Watu walipwe kulingana na uzalishaji wao, kwa vile waliboronga kazi basi ni busara wapunguziwe mshahara kufidia hasara waliolisababishia taifa na tena walipaswa kustaafishwa kabisa, rais ana huruma.
Tuna Rais mwendawazimu asiyeshaurika.
Alishawahi kutamka hadharani kuwa wale alowakuta wakipata mishahara minono wakiishi kama Malaika atawashusha waishi kama Mashetani!!!
 
Kiwango chao cha kuboronga wakijua au?
Waliboronga vipi na kwa nini?
Mambo mengine utakuta yalikuwa nje ya uwezo wao.
Watanzania tumegeuka kuwa viumbe wa ajabu sana na tusio na shukrani, kipindi cha awamu ya 4 kulikuwa na utaratibu wa kuwahamishia maeneo tofauti watendaji walioboronga kazi ama kufanya ubadhirifu, na hii ilikuwa kero kubwa kwa wananchi! awamu hii imeamua kupambana na kero hiyo, sisi hawahawa Watanzania tena tumegeuka kuwa watetezi wa wazembe na kuwalaumu wanaoshughulika na wazembe! Hiiiiiiii....!
 
Tumbo kwanza utaifa baadae
 

Attachments

  • Screenshot_20201214_174029.jpg
    Screenshot_20201214_174029.jpg
    68.9 KB · Views: 1
Huenda Raisi ameona wafanyakazi wanatolewa kwenye hizo nafasi za uongozi halafu mishahara haiguswi inakuwa kama wamepongezwa. Na wengine hawaogopi kutumbuliwa. Ni lazima aendelee kukaza bolti zikamate vyuma sawasawa. Nchi ilishafikia pabaya kabisa! Alipoanza sikuamini niliposikia eti tulikuwa na wafanyakazi hewa elfu kumi. Halafu akachaguliwa Mkuu wa Mkoa akambishia kuwa mkoa wake hauna wafanyakazi hewa? Aliposafisha hiyo siuliona hesabu zilikaa sawa mara moja? Kama angemsikiliza asingeweza kumaliza ile kazi. usemi wa "hapa kazi tu" sasa ndiyo umeanza kueleweka vizuri. Mwacheni Raisi afanye kazi yake, anaiweza na anamoyo nayo.
 
Rais wetu anauwezo mkubwa wa kusema ukweli, ni Rais wa kipekee barani Afrika na hata duniani. Muacheni afanye kazi yake aliyojitolea kwa ajili ya manufaa ya taifa letu !
Mtoto asiye tembea hujua kuwa mama yake pekee ndiye mtaalam wa mapishi hivyo si kosa kufananisha mtu aliyekosa sifa za kuwa rais wa kuigwa bali yeye anawaiga akina mseveni,kagame na marais kutoka burundi na kongo hebu nikuulize ni nchi gani katika Afrika iliyoiga utawala wa huyu bwana mkubwa.
 
Kwanini waliwapeleka huko ambako mishahara ni midogo? Siwangewapeleka huko alikokutaja TRA? Kwahiyo wabadili kanuni ili kushusha mshahara wa mtu?? Nahizo kanuni zitakuwa za mwaka gani? Yaani GN no ngapi ya mwaka gani?
Labda niuoga wa maisha tu.
Au khari ngumu ya maisha
Km vp mnasongeshana CMA
Iliaminika kuwalipa vizuri tea kutapunguza ushawishi wa kuomba rushwa, kinyume chake wafanya biashara wanaibiwa. Kodi ya serikali haiguswi. Mlipa kodi stahili ya sh 500000, anaambiwa kodi yako ni sh 1500000. Akilalamika anambiwa kama una sh 500000 let tukusaidie ili ulipe sh 500000, anawapa na kweli anakadiriwa sh 500000. Kifuatacho mtaji unakatika, bank marejesho yanagoma. Akikosa ya kuwapa anambiwa akafunge biashara. Hiyo ndio TRA.
 
Mtoto asiye tembea hujua kuwa mama yake pekee ndiye mtaalam wa mapishi hivyo si kosa kufananisha mtu aliyekosa sifa za kuwa rais wa kuigwa bali yeye anawaiga akina mseveni,kagame na marais kutoka burundi na kongo hebu nikuulize ni nchi gani katika Afrika iliyoiga utawala wa huyu bwana mkubwa.
Hawawezi kuiga kwa sababu hawana uwezo, nabii hakubaliki kwao. Iko siku mtamkumbuka Rais Magufuli na kuelewa kile anachokipigania sasa !
 
Watu walipwe kulingana na uzalishaji wao, kwa vile waliboronga kazi basi ni busara wapunguziwe mshahara kufidia hasara waliolisababishia taifa na tena walipaswa kustaafishwa kabisa, rais ana huruma.
Wakishapunguziwa hiyo mishahara na watachapa kuongeza uzalishaji ili waongezwe tena au ndo utendaji utadorola kabisa?
 
Hata akiwafanya watanzania karibu wote kuwa adui zake watamfanya nn? Watanzania hawana la kumfanya huyu jiwe.

Anajiamini, ana dola, yuko juu ya sheria na anaweza hata kuwaua hao watumishi wa TMAA na hakuna wa kumgusa. Rais wa Tanzania ni Mungu wa watanzania.
Ona aibu basi eeeeh!!
 
Nimesikiliza hotuba ya mh. JPM baada ya kumuapisha Naibu Waziri wa madini Prof. S. E.Manya.
Moja ya sababu zilizosababisha kuleta huu uzi ili wana CCM wenzangu ambao wanaweza kutafakari uzi huu na ikibidi kumshauri mh. Rais.

KIMEJIRI KITU GANI KWA MAONO YANGU?
Mh. Rais alizungumzia mambo ya msingi kuhusu hii wizara kuendelea kuwa wabunifu wa kuibua vyanzo vingine kama cool, coper, gas nk. Badara ya kukomalia dhahabu peke yake. Alikuwa sahihi kabisa.

Shida ilikuja alipoanza kuwazungumzia waliokuwa watumishi wa TMAA, ni kweli kulikuwa na mapungufu katika tume ile, na aliivunja, na matokeo kweli tumeyaona na tunayaona. Ila sidhani kama lugha na maagizo aliyotoa yamepitia kwa washauri wake.

KWANINI?
Sidhani kama ni vizuri kuwasema watumishi wale ambao wengine bado wapo ndani ya Wizara na tume kuwa walifanya kazi za hovyo. Katika hili ajue tume hiyo ilianzishwa na Serikali iliyokuwepo chini ya Rais kama yeye, hivyo kabla ya kuwatukana wale amtukane kwanza Rais aliyekuwepo.

Lakini ajue kuwa mishahara waliyopewa watumishi wale hawakujipangia bali walipewa kwa mujibu wa taratibu walizozikuta waajiriwa wale. Hivyo hawakuwa na kosa.

Ok, kama aliona kuna utofauti mkubwa wa mishahara basi angeshauliwa eidha kuwapeleka kufanya kazi maeneo ambayo inalingana na mishahara yao kama vile TRA aliyoitaja kuwa hata yeye inamzidi mshahara maana hata TMAA kazi yao ilikuwa kukusanya kodi zitokanazo na madini kama ilivyo TRA.

Au angewaongeza wafanyakazi wte waliokuwa chini ya hawa watumishi wa TMAA ili kubalance. Mimi binafsi Enzi na Enzi sioni afya ya maagizo aliyoyatoa ya kutaka hata kanuni zibadilishwe kwa lengo la kushusha mshahara wa mtu au kikundi cha watu.

Mh Rais na washauri wake wakae wakijua kuwa hawa kumshusha mtu mshahara ambao amezoea kuuishi na familia yake ni kumpa magonjwa ya moyo au presha kwa aliyekuwa hana.

Lakini pia watumishi hawa najua hawataacha kazi maana maisha ni magumu lkn watakaa wakimlilia yeye muda wote. Ni bora kama alikuwa hawataki angewafanyia hiyo Retrinchment maana nalo lina taratibu zake.

ANGALIZO KWA MH SPIKA JOB NDUGAI
Ifike sehemu Bunge nalo lijisimamie na litetee wananchi na wafanyakazi badala ya kuunga mkono kila hisia za kiongozi.

Wana ccm mshaurini Rais ajifunze kupunguza maadui badala ya kuongeza maadui kila uchwao ikibidi kumkatalia kabisa, ipo siku atakuja na jingine tena.

Huko nje kuna watu walitumikia nchi hii ktk mfumo uliokuwepo walikuja kuachwa bila malipo yeyote hilo nalo lilikuwa ni uonevu, ni bora angewalipa kama alivyofanya Mkapa mwaka 1997 baada yakuwaondoa darasa la7 ktk Wizara ya Afya.

Rais awe anatumia lugha mwanana kushairi, kuonya, au kukemea maana yeye ni kiongozi mkuu hata akiongea anacheka litafanyiwa kazi tu.

Asijitambulishe kuwa nikatiri mno hana huruma nk. Kumbe ni namna ya anavyotatua matatizo hata kaam yana tija lakini nguvu inakuwa kubwa mno, eti kubadili kanuni !! Loh! Kwasababu ya mshahara wa mtu tu. Akumbuke hawa ni waajiriwa. Mh. Asipoangalia atakuja akiponze chama pendwa cha CCM, sijui nao wanamuogopa?

Nawasilisha tafadhali.
Enzi na enzi.

Mkuu ungetulia kwanza. Watu hulipwa kwa masaa na utendaji wao. Siku nyingine sifia tu sio dhambi
 
Taarifa za Ben wanasubiri wananchi, lkn taarifa za wanaomkosoa jiwe na zile za chadema wanaotaka kuandamana huwa wanazipata.
Tatizo la Chadema wanapenda kusalitiana sana,hasa wakioneshwa mpunga kidogo ndiyo maana unaona information zao police wanazipata mapema sana!!
 
Back
Top Bottom