CCM, tafuteni namna ya kumshauri Rais Magufuli maana muda mwingine anaumiza sana

CCM, tafuteni namna ya kumshauri Rais Magufuli maana muda mwingine anaumiza sana

Sijaona hoja hapo. Umeisoma mada vizuuri lakini Pascal? Hii imefanana na kijana aliyejaribu kumchumbia binti, alipomkosa akaanza kuona makovu aliyo nayo usoni na kuanza kutangazia watu kuwa ana sura mbaya .

Utakuwa unadhani mtoa mada ni mtumishi , au muathirika wa hiyo habari!! La hasha!
Nakama huwa unafatilia mada za mleta uzi huu, ni team jpm leo jana nahata siku zijazo.

Nampenda sana jpm, na jpm siyo maraika, lkn pia tunayohaki ya kumshauri kwa njia hizi au kuonyesha kuwa sisi wapambe wake, kuna mambo hatukubaliani nae. Siyo kila kitu ndio. Au kushangilia, tutakuwa tunampoteza, ni kheri tuseme kuliko kukaa kimya.

Mwisho, hata kama jamaa baada ya kukataliwa na binti then akaanza kutangaza sura ya binti kuwa ni mbaya, bado wewe unayetangaziwa usipuuze mwangalie binti sura yake km kweli inamakovu??? Ukibaini haina basi sema kuwa jamaa anamtangaza binti kwakuwa katoswa.

Nenda ukasome habari ya kuzama kwa meli kubwa ya titanic hata ktk mtandao!. Uone namna ilivyozama na namna watu walivyoangamia.

Kifupi nikwamba wengi wao nahata nahodha wao, walizarau maonyo.
 
Labda kama hujui kwanini hili tunalisemea, nikwamba, linaweza kuathiri watu wengi sana nahata sisi wananchi wanyonge.

Usizani wafanyakazi wte watalipokea sawa sawa! Ndio maana kukawa na utaratibu wa kumshughulikia mkosaji kisheria, tena ndani ya mahakama. Ili kulinda utu wake.
Kunawatu wamepoteza maisha kaka kwa hii stail.
Utu wa mtu ndilo jambo muhimu ktk maisha ya binadam.
Utu wa mtu hauthaminishwi kwa cheo, pesa, au madaraka.

Km wewe ni mkristo, nijibu hili swali dogo, kwamba kwanini yule mwanamke aliyekamatwa amezini ,nakisha kupelekwa kwa yesu ili yesu atoe hukumu, unadhani kwa nini yesu aliwaambia wale washtaki wake kuwa ambaye hana dhambi aanze kumponda huyu mwanamke jiwe? Je! Kwa nini hakutokea hata mmoja?
KWANINI YESU
ALIFANYA HIVYO?... Alijua hakuna ambae hana makovu ya makosa , na alitaka tuonyane kwa staha na kuheshimiana siyo kama mafarisayo yalivyomburuta mama wa watu.

NIJIBU SWALI HILI.
............................................
Kicheree alivyotolewa TRA kwenda kuwa RAS nae alitangazwa kupunguziwa mshahara? Nae sialiharibu TRA?
Diwani alipopelekwa kuwa RAS nae alipunguziwa mshahara?
Aijipi aliyepewa ubarozi, nae alitangazwa kupunguziwa mshahara?
Andegenyee wa fire nae alipunguziwa mshahara???
Nawengine wengi.

Tuweni wakweli , maana msema kweli ni mpenzi wa mungu.
Enzi na Enzi
 
Wewe nawe usilete ushabiki wa vyama hapa.
1.tundu lissu alistahili kilichompata, huyo niadui wetu sote watanzaia.
2.seth na lugemalila nikweli wameliibia hili taifa na hawataki kurudisha wangerudisha wangekuwa uraiani.
3. Ben sa8 no comment, maana cjui chochote kuhusu yeye zaidi yakusikia tu, inaweza kuwa kweli katekwa au kajiteka pia, maana wa tz nao kwakutengeneza story za kuchafuana tumo.
Kwa majibu haya, tunakuomba mheshimiwa endelea kupunguza mshahara wa hawa watu ikibidi walipwe mia tano, hadi siku akili ziwakae sawa!

Kwamba Lissu ni adui yako???? Alikufanya nini? Hebu eleza huku ukiambatanisha ithibati thabiti hapa.
 
Huu ni utawala ambao unajitahidi kila raia wake awe masikini na kwakweli unafanikiwa sana,jiwe anajigamba kupokea mshahara 9m na anaiona ndogo sana,Ingekuwa vema tungejua na allowance zake kwa mwezi hapa ndio kwenye kipimo sio mshahara.
Mara nyingi tawala zakibabe huwa zinaongoza sana kwa ufisadi,muda ni hakimu mzuri wacha tusubiri.
 
Suala la kupunguza salary siungi mkono but rather Government wangeongeza mshahara kwa hao Maboss wa Time ya Madini
 
Mtoa mada nikuambie tu kwamba mliishi kwa mazoea huyu Rais ndio anafaa kwa Tanzania hii.
 
Magufuli anapanga mpaka mishahara ya Watu na kila kitu ndani ya Nchi.
Kwani nini maana ya kuwa Rais, hujui kwamba tuko kwenye matengenezo baada ya mifumo ya nchi kuoza kwa rushwa, ufisadi na vyeti fake. Ili kujenga lazima uvunje, uharibu na kuangamiza. Usiishi kwa mazoea
 
Endeleeni na matusi lakini kumbuka mtaendelea kutawala humu JF lakini si kuingia Ikulu ya Chamwino.
Ukiona mtu anajiita Jiwe, mara Jembe, unadhani utamshauri nini?
Mtu anayemgawa mama yake kwa malipo ya jogoo
 
Hafai ? Wakati tumemchagua wenyewe. Wewe unayefaa uko wapi sasa tukuone.
Rais mwenye majina mengi ujue hafai na dikteta. Hivyo Idi Amin, Kamuzu Banda, et al walikuwa na majina mangapi kila mmoja? Tena majina ya hovyooo. Wengine waliitwa Dada (Idd Amin), kuku (Kamuzu) na sasa nasi tuna Jiwe!!!.
 
Wengi wetu wabongo tuna tabia ya kufurahia tukisikia ndugu zetu yanawafika majanga. Hii ni hulka mbaya sijui ni wivu, roho mbaya au malovelence au tuko sadistic sijui ni pepo au shetani gani.

Baadhi ya ambayo tumejukuta tunashangilia kimkumbo mkumbo huku wengine wakiumia ni:

1. Watu wakitumbuliwa hadharani bila kupewa nafasi ya kujitetea. Wakati mwingine kwa hisia tu au majungu yaliyopenya hadi kwa watumbuaji. Akina Mkurugenzi wa Jiji Kabwe (Mungu amrehemu kwani alifariki mara)

2. Kufukuzwa kazi kwa watumishi wa umma ambao wengine wamelitumikia taifa kwa zaidi ya miaka 20 kwasababu ya vyeti. Walimu, manesi, madereva nk

3. Wananchi wenzetu kuvunjiwa nyumba na serikali kuachwa homeless. Ubungo Morogoro Road

4. Wananchi kukamatwa na kutiwa ndani kwa amri za wenye mamlaka bila kufuata haki na sheria.

5. Wanasiasa wa upinzani kuonyeshwa cha mtema kuni.

6. Watu kutekwa, kupotezwa, kupigwa risasi na hata kuuwawa. MO

7. Watu kukamatwa kuwekwa korokoroni kubambikiwa kesi za uongo. Masheikh wa Zanzibar.

8. Wafanya biashara kuporwa fedha zao benki.

Na mengine mengi!!

Sisi wananchi wakati mwingine bila kutafakari nakujiuliza vizuri tumekurupuka na tumeshangilia na kufurahia haya yakitendeka ilimradi hayatugusi sisi binafsi!

Sasa hivi hawa watumishi wa TMA tumeshawahukumu kuwa ni wakosaji tushangilia kama mazuzu eti wapunguziwe mishahara kinyume na sheria sababu tu kiongozi ameituhumu tume iliyokuwa imewaajiri zamani hizo.

Tunataka wapunguziwe mishahara bila kujali madeni na commitment walizoingia kwa kutegemea kulipa kupitia mishahara yao!
Tunasema acha nao walipate joto la jiwe, acha nao wateseke, wapate presha na sukari au hata kufa na wafilie mbali tu. Kwani nini bwana.

Sisi tunaofurahia mateso haya kwa wengine ni sisi tunaojiita wacha Mungu, wazalendo, tuaoipenda Tz, wapenda maendeleo!!

Tumwombe Mungu atubadilishe, tuwe na upendo, huruma, subra, tuipende haki na tuchukie dhuluma. Haya ndiyo maamrisho ya Mola wetu.

Muda wa kuishi ni mfupi tutendeane yaliyo mema na tuitende iliyo hakhi!!

Haki huliinua Taifa.
Tupendane tustahiane.
Huo ni wimbo tulishauchoka. Tafuteni mwalimu mpya wa kwaya yenu atunge nyimbo zingine. CCM hii kwa upinzani wa nchi hii itatawala mpaka ichoke yenyewe.
 
Kituko mbele ya watu gani ? Wewe na wapinzani wenzio uchwara ndio kituko katika nchi hii
Nyie ndiyo mnamponza jiwe mpaka anaonekana kituko mbele ya watu(wanaojielewa lakini wewe haumo).
 
Umeandika malalamiko yako mengi kisa tu umeshushiwa Mshahara, simple tu,achana na hiyo kazi ya Mshahara mdogo nenda tafute kazi ya Mshahara Mkubwa! Na Kama kuna Watumishi wanaofanya Mambo ya hovyo huko Ma officine naomba waache Mara moja! Utumishi wa Umma siyo sehemu ya kujitajirisha,ni sehemu ya kuhudumia Wananchi kwa Uzalendo Mkubwa wa hali ya Juu sana! Siyo msubiri hadi Magufuli aje awafundishe Majukumu yenu,saa zingine mnaboa sana,acha Chuma Cha Moto kiwaanyooshe labda mtatia akili!!
Naam. Waambie ndugu yangu
 
Hata yeye aliyetoa hyo maagizo hakuzingatia kanuni za utumishi wa uma.
Ndo maana tukahoji nguvu yakubadiri kanuni ili kumkomoa mtu au kikundi.
Wafanyakazi wangapi aliowatumbua , je nao walibadirishiwa kanuni? Ili mshahara wao ushushwe??
Na je! Wote walikuwa wabaya??
Huyo ni mkuu wa nchi. Hujui kuwa Rais ndiye mkuu wa Utumishi wa umms ?
 
Tukikosa mtu mbadala ataendelea aendelee kuinyoosha nchi
Wanachotakiwa kumshauri ni kujiandaa kutoka madarakani baada ya 2025 maana kashajipanga kuchezea katiba yetu na kuwa kama best yake mseven
 
Mbona wenye vyeti fake waliendelea kuongezeka nchii hii, Rais aliyekuwepo hakujua ? Mwacheni RAIS wetu achape kazi na kuondoa uozo wote. Mlizoea vya kunyonga vya kuchinja hamuviwezi.
Kiujumla hawakufanya kazi ya hovyo, nawangefanya ya hovyo nadhani Rais aliyekuwepo asingeacha iwe ya hovyo.

Ila kwa maono yake ilikuwa niya hovyo! Is fine , hivyo alivyokuja! Alitakiwa tu aboreshe kwa kuwatumia waajiriwa hao hao na kuwatumbua sasa wakiwa hapo hapo!! Maana alishasema huwezi kumuhamisha mtu aliyefanya madudu.

Kumbuka kuwa ...uongozi ni VISION hakika hatata yeye akumbuke alikuwa ktk serikari hyo hyo wakati ule, hivyo hata yeye akitoka Rais atakae kuja atakuja na Vision yake!

Sasa nikuulize swali, Rais ajaye naye akisema wafanyakazi wa TRA wanamshahara mkubwa nao wabadirishiwe kanuni ili wapunguziwe km hawataki waache kazi hyo itakuwa nisawa???

Mfano!
Wakati anamtoa kichele TRA kwenda kuwa Ras nae alimpunguzia mshahara??

Wakati anamtoa Andengenyee pale fire kwenda kigomaa kuwa arac je! Nae alimbadirishia mshahara?
Alitoa wengi, je nao aliwapunguzia mshahara??? Au TMAA walimkosea nini??

Au hajui kuwa kabla ya TMAA kulikuwepo na Arexstuwart ambao walikuwa wakilipwa kwa Dolla???
Haoni kuwa TMAA hata hyo mishahara nikama waliipunguza kuliko ya Arexstuwart?

Haya sasa!! TRA amekiri kuwa hata yy wanamzidi mshahara!! Kwani wao sio watanzania?? Mbona hajataka wapunguziwe??
Kazi za TMAA au wizara ya madini, hazina tofauti na za TRA, maana nao wanakusanya kodi na kulinda napato yatokanayo na madini!!

Hatutaacha kuusema ukweli maana msema kweli ni mpenzi wa mungu.
 
CCM hii ya mmaamuma watu wanamsujudu mtu wanajuwa ana file milembe zile sehemu za madini amewaweka watoto wa dada zake wajineemeshe tu fedha wNawatajirisha warundi na wanyarwanda wanakowekeza CCM ni wapuuzi wamemuweka mtu kuwa mwenyekiti wa chama chao wakijuwa anafile milembe ni psycho kabisa na ndio maana amekiuwa chama amebaki na genge la usalama wataifa huku wenyewe wakianza kuuwana hivi dhahabu kweli tangu inavyochimbwa nchi nzima siingekuza pato la taifa na kuwa namva moja mbona ni korosho sasa anabwabwaja tu maana hana sera yeyote ya maana ya uchumi kuukuza
Hiyo CHADEMA ya wajanja iko wapi ? Usituletee ugali uliochacha hapa siye tuko busy kuijenga nchi.
 
Ujue ili iweje ? Huo mshahara tu wa Mbowe huko CHADEMA huujui sembuse wa mkuu wa nchi ili uufanyie nini ?
Huu ni utawala ambao unajitahidi kila raia wake awe masikini na kwakweli unafanikiwa sana,jiwe anajigamba kupokea mshahara 9m na anaiona ndogo sana,Ingekuwa vema tungejua na allowance zake kwa mwezi hapa ndio kwenye kipimo sio mshahara.
Mara nyingi tawala zakibabe huwa zinaongoza sana kwa ufisadi,muda ni hakimu mzuri wacha tusubiri.
 
Watu walipwe kulingana na uzalishaji wao, kwa vile waliboronga kazi basi ni busara wapunguziwe mshahara kufidia hasara waliolisababishia taifa na tena walipaswa kustaafishwa kabisa, rais ana huruma.
Kiwango chao cha kuboronga wakijua au?
Waliboronga vipi na kwa nini?
Mambo mengine utakuta yalikuwa nje ya uwezo wao.
 
Back
Top Bottom