LGE2024 CCM: TAMISEMI itambue demokrasia yetu ni changa, ipuuze makosa madogomadogo katika hatua ya rufaa uchaguzi Serikali za mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Ccm wanajitekenya na kucheka wenyewe.
 
Yaani ccm ni washiriki wa uchaguzi halafu ndiyo wasimamizi wa uchaguzi huo huo !!

Huo ni utapeli na dharau ya hali ya juu sana dhidi ya wananchi.
Tlaatlaah Lucas Mwashambwa
 
Safi sana CCM baba wa siasa
Hapa ni ile unatengeneza tatizo na unajaribu kuwaonyesha watu kwamba unalitatua tatizo hilo ,kinacho endelea katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa ni AIBU kwa Taifa, wasimamizi wa uchaguzi walianza kwa kufunga na kukimbia ofisi ili wapinzani wasichukue wala kurejesha fomu, wachache walifanikiwa kuchukua na kurudisha , majina yao yalikatwa, wakati wa kukata rufaa, wamekimbia tena na kufunga ofisi ili wapinzani wasirudishe rufaa zao.

Kama ccm wanataka kujisafisha wamweleze waziri wa TAMISEMI ajiuzulu kwa kuvuruga uchaguzi. Vinginevyo tutajua amevuruga kwa maelekezo yao.

Sijui udhalimu huu utaisha lini nchi hii, halafu watu na akili zao timamu anafurahia udhalimu katika uchaguzi, sasa MTU akivuruga uchaguzi kwa makusudi ataweza vipi kusimamia barabara ijengwe kwa viwango!? Atafamya kwa kiwango cha kuchakachua kama walivyo chakachua uchaguzi
 
Kwa maana hiyo nchi imethibitika kabisa kuwa haiendeshwi kwa sheria tena, bali kwa utashi wa rais!!!
Kama watu wameenda kinyume na sheria,iweje warudishwe!!??

Hii imenipa wasiwasi mkubwa wa kuwa matendo ya wasimamizi wa uchaguzi ni maagizo kutoka juu,na sio kweli kuwa sheria, taratibu na kanuni zimetumika.
 
Watapojua democrasia Imekula watatafutana maana Nchi imedumaa baada ya kunyoma watu elimu ya uraia
 
Huu uchaguzi haupaswi kugharamiwa na serikali hata shilingi moja. Ni mambo madogo sana ambayo wananchi wenyewe kupitia watendaji kata/kijiji/ mtaa wangeratibu na kusimamia kuchaguana.
Tena hii unaitishisha mkutano mmoja tu hapi, kila mgombea anawepewa dk 15 za kujieleza nabkujibu maswali kisha uchaguzi na majibu yanatolewa.
 
Je sheria isifuate mambo yaende kiholela!

..hata utenguaji umefanyika kiholela.

..na sheria iliyopo ni ya kihuni ambayo imekataliwa na wadau.

..yanayoendelea ni jitihada za Mama Abduli kuiba uchaguzi ila makelele yamezidi.
 

..huu ni upumbavu.

..Waziri wa Tamisemi ni Rais Samia mwenyewe.

..Mchengerwa sio Waziri kamili, ni Waziri wa Nchi ofisi ya Raisi Tamisemi.
 
Your browser is not able to display this video.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeiomba Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kuwaelekeza wasimamizi Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kupuuza makosa madogo madogo yaliyotokea, ili kuruhusu wagombea wengi kushiriki uchaguzi huo.

Akizungumza na wahariri na waandishi waandamizi wa vyombo vya hahari nchini, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametoa mfano wa makosa hayo yanayostahili kupuuzwa ni pamoja na wagombea kukosea herufi.

Kupitia mkutano huo uliofanyika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam, leo Novemba 12, 2024, Balozi Nchimbi amesema ni vyema TAMISEMI ikaangalia uwezekano wa kuwarudisha wagombea wote walioenguliwa kutokana na makosa hayo madogo madogo ili kuhamasisha ukuaji wa demokrasia kwenye uchaguzi huo.

Aidha, kuhusu sehemu kubwa ya malalamiko mengi ya kuenguliwa kuonekana ni ya wagombea wa vyama vya upinzani, Balozi Nchimbi amewatoa shaka Watanzania kuwa, si kweli kwamba wagombea walioenguliwa ni wale wa vyama vya upinzani pekee, bali pia hata wagombea wa CCM wapo waliowekewa mapingamizi ya kugombea.

“Waziri wa TAMISEMI tunajua anafuata sheria, lakini ni muhimu kutambua demokrasia yetu hii bado ni changa hivyo tunahitaji muda wa kuendelea kujiífunza…tunaziomba mamlaka hasa TAMISEMI katika nyakati za mwisho za rufaa kuyapuuza makosa madogo madogo ili watu wengi wapate nafasi ya kugombea", alisema Dkt. Nchimbi.

#Ends
 
Sasa CHADEMA ata wagombea hawana ila wanataka kujitoa kutafuta huruma hii ni akili kubwa sana ya CCM
 
Tunatengeneza tatizo na tunatafuta credit kuliondoa.
Ikiwa sheria,kanuni na taratibu zinafuatwa yanini matamko na maelekezo?
Hii nchi........Mh.
 
hivyo nitumie nafasi hii kutoa wito kwa waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa, tunatambua umefuata sheria
Mstari huo (tunatambua waziri Mchengerwa unefuata sheria) una uvundo
 
Mimi napata tabu Sana, hv tume ya uchaguzi ni ccm? Yaan ishu za rufaa wanatangaza ccm, sababu za kukatwa zinademwa na ccm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…