LGE2024 CCM: TAMISEMI itambue demokrasia yetu ni changa, ipuuze makosa madogomadogo katika hatua ya rufaa uchaguzi Serikali za mitaa

LGE2024 CCM: TAMISEMI itambue demokrasia yetu ni changa, ipuuze makosa madogomadogo katika hatua ya rufaa uchaguzi Serikali za mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Semeni wote walioomba wapitishwe kwa sababu wengi wenye ubora wameenguliwa, nao wameamua kutokata rufaa kwa sababu wanajua kifuatacho itv.
 

"Wapo Wanaccm waliowekewa mapingamizi, wapo wa ACT, wapo wa CHADEMA, na majibu ya mapingamizi yalitoka, lakini kwa hatua za rufaa kwa maelekezo ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ambaye ni Rais wa Tanzania nilipofanya naye mazungumzo, ambacho tumekiona wapo wagombea wengi sana wa vyama mbalimbali ambao waliwekewa mapingamizi katika hatua za awali.

Katika maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM, tumeelezana kuwa ni vizuri watu wapate nafasi, hivyo nitumie nafasi hii kutoa wito kwa waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa, tunatambua umefuata sheria lakini ni muhimu kukumbuka kwamba demokrasia yetu bado ni changa, ni muhimu tuzidi kukua.

Soma Pia:
Tunaziomba mamlaka hasa TAMISEMI, katika hatua ya mwisho za rufaa kuyapuuza makosa madogomadogo ili Watanzania wengi zaidi wapate nafasi ya kugombea. Yapo makosa makubwa, kwa mfano nafasi ni maalumu kwa wanawake lakini amejaza mwanaume"
Kila ukifika wakati wa uchaguzi demokrasia inadumaa, (inakuwa changa). Swali fikirishi ni nani anaidumaza demokrasia Tanzania?
 
...Tamisemi ni wizara iliyoko ndani ya Ofisi ya Raisi.

..sio wizara kamili kama Wizara ya Fedha, Mambo ya ndani, etc.

..kilichotokea ni Waziri wa Tamisemi kuiomba Tamisemi ....

..Nadhani MAKELELE yamekuwa mengi wanaona haya kuendelea na uchaguzi waliokuwa wamepanga.
Na yote yaliyofanyika ni wazi kabsa kulikuwa na maelekezo toka juu.
 
Sifa na pongezi zimfikie mwenyekiti wa CCM kwa kuamuru wapinzani walioenguliwa kwenye wagombea wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa warejeshwe, hata hivyo jambo hili lilitegemewa ili zile 4R zionekane bado zinanguvu.
Je, wapinzani watampongeza anayeandaa uchaguzi ambaye ndiye aliyewaengua kwa hila kwenye uchaguzi huo? Hebu tusubiri upande wa vile vyama vinavyozinduliwa wakati wa uchaguzi tu vitatoa sifa zipi.
 
Bado naendelea kusisitiza na kuwakumbusha wapinzani, Rais Samia ni muumini wa utawala wa sheria na katiba, haki na demokrasia. Anafanya kila linalowezekana kukuza demokrasia. Hata kama nabii hakubaliki kwao, mkubalini nabii huyu kwa maendeleo ya nchi yetu, mtabarikiwa sana.

Kuna siku naamini uzi huu wa huyu mdau utafunguliwa na kujadiliwa kwa kina Rais Samia ndio Magareth Thatcher wa leo, Mwanamapinduzi na Mwanamageuzi wa kweli
 
Lakini hata Vyama vya Upinzani ni Wazembe!
Kwa nini vyama visitoe elimu kwa wale wanaotia nia ya kugombea katika chaguzi hizo?
Lakini siyo hilo tu! Vyama vya Upinzani vingekuwa vinahakiki fomu zao kabla ya kuzirudisha!
Ndiyo maana CCM wanatumia mwanya huo wa uzembe wa vyama kama huu.
 
Kiongozi mwenye maono makubwa ya kuleta maendeleo hawezi kuuchekea huu upinzani wa wabembeleza Ruzuku

Hivi Vyama vya Upinzani viliundwa kwa hisani ya Mwalimu Nyerere kwa ajili ya kuombea misaada kwa Wazungu

We fikiria Chama Cha Upinzani kinaamrishwa na CCM kikate Rufaa na chenyewe kinakubali kama mazuzu vile 🐼

Yaani unakata Rufaa kwa CCM ile ile 😂😂😂

Bure Kabisa 🐼
 
Akili yako fupi, inaona nchi moja mbele.

Wenzako wanafuata taratibu zote ili mwisho wa siku wawe na uhalali wa katumia njia mbadala
 
BUNGE LOTE LAO WAMELETA NN ZAID YA UTEKAJI NA KUUZA BANDARI ZETU NAKUGAWA MAPORI KWA WAARABU KM PIPI?
 
Back
Top Bottom