MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Nataka niliseme hili na ninaomba tuweke kumbukumbu hii kwa rejea ya kesho muda ukifika.
Chama changu tulitaka kuungana pamoja na watanzania kuhusu suala la Tozo za kwenye simu baadaye tukaungana na serikali tikakaa kimya, mafuta yakapanda bei tupo kimya,vifaa vya ujenzi vipo juu tupo kimya, bei ya gesi ya kutumia majumbani ipo juu tumeganda kimya, sasa imekuja kodi Majengo ambayo ilikua ilikua ikilipwa na wamiliki moja kwa moja lakini serikali imeagiza kibao hicho kwa mpangaji ambaye ni mtu wa chini kabisa kupitia LUKU eti ukikatwa kodi hiyo nenda kaidai kwa mwenye nyumba(hii siyo sawa). Pamoja na ugumu wote huu wa maisha tunatumia mgongo wa uzalendo kuwaumiza wananchi wa hali ya chini tukidhani watesema kesho watasahsu.
Tukumbuke kua huu ndio uhalisia wa maisha ya sasa na tunawapa wapinzani agenda na sababu za kuongea, kama kweli wananchi wana maumivu makali sana juu ya haya wanatoyapitia tunawapa mwanya wa kuungana na wapinzani kuikataa CCM. Sasa wataungana nao kuidai katiba mpya wakiamini kua huenda ubovu wa katiba hii ndio chanzo cha maumivu yote haya. Tukae tukizipa masikio lakini iko siku utatokea msukumo mbaya toka kwa wananchi tutapoteana.
Chama changu CCM ki ashindwa kujitenga na serikali ispokua chenyewe ndio kimekua na kazi ya kuisemea na kuitetea serikali badala ya kuisimamia na kuishauri kutimiza ilani yake, matokeo yake mwishoni siyo mazuri na muda siyo mrefu tutazungumza.
Tutajivunia kuitumia serikali hiyo hiyo kulilinda chama lakini tunashindwa kuelewa kua wapinzani wetu nao wana akili timamu, tunashindwa kuelewa kua wananchi nao wanabadilisha na kua na uelewa mkubwa kupitia maumivu yanayopitia. Tusizibe masikio tusikilize maoni ya wananchi na siyo ya serikali tusiyapuuze.
Tunasikitika maamuzi ya viongozi wachache wasiokua na huruma wasiojua maumivu ya watu wa chini, mimi nikiwa kama mwanaccm siafiki kabisa hizo Tozo za simu na kodi za majengo tunalazimishwa kitu ambacho wananchi hawako tayari nacho, hii inagharama yake na tutalipa.