CCM tulifanya kosa kubwa sana 2015, tusirudie tena. Chuki iliyopo ni kubwa sana

Umegusia karibu kila mahali japokuwa umesahau kuua biashara bandiko Bora kabisa hongera sana mkuu
 
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji44]uko sahihi kabisa
 
Ni dhahiri wale wengi waliokuwa wakiubatiza hata uovu wa magufuli kuwa wema sasa kwa mbaali ubinadamu umeanza kuwarudia.

Nawashukuru wapinzani hawajawahikufikiria bado kurudisha visasi zaidi ya kudeal na kukata mirija yao nje kwa kuyasema maovu yao.

Wapo wanaochukizwa kwa kuikata mirija hii huko nje wakiona si uzalendo kwa sababu tu ya matumbo yao(pesa kuzibwa)

Lakini hapo hapo hawauoni uzalendo mkubwa wa kweli wa wapinzani kutetea damu ya watanzania wanyonge wanaouwawa kwa kupaza sauti kutetea haki zao za msingi.

Yaani ukitetea haki za msingi Tanzania wewe unakuwa mnyarwanda.

Ndio mataga na akili za kimagufuli hizo.
Binafsi wanaopata akili kama wewe muandishi sina kinyongo nawe japo mkumbuke tunakoelekea watanzania hatutakuwa wapole na wenye huruma tena.

Itakuwa ni jino kwa jino, katiba ya kikondoo haitatutosha. Na ccm ndiyo itakuwa imetufikisha hapo.
 
Chuki iliyopo ndio freshi, acha impe somo delila...
 
Hizi blah blah tu.
Tunataaka mama atupatie katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ili tuwaondoe kabisa ccm, hatuwezi kung'ang'ania majaambazi, kama mmeweza kufanya hayo yote huku tunapoelekea si mnatuua wote kabisa?
Ccm hata shetani anawaogopa, sina urafiki wala undugu na mwanaccm yeyote, mmeyataka wenyewe, akifa ccm kwetu sisi ni bia na nyama choma tunasherehekea
 
Nilimpenda Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa Kujenga Misingi hasa ya Kiuchumi, Utaratibu na Kurejesha tu Nidhamu iliyopotea kwa muda mrefu Serikalini.

Ila Sikumpenda Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa tabia yake ya ' Kuwalea ' na kuwapa ' Viburi ' hawa ' Intarahamwe ' Watatu akina Sabaya, Makonda na Mnyeti.

Nimeenda mbali zaidi na kuhisi kuwa huenda hata Yeye Hayati Rais Dkt. Magufuli nae alikuwa na hizi Roho za hawa ' Intarahamwe ' Watatu aliowapenda mno na kuwapa ' Viburi ' vyote vya ' Kimamlaka ' katika Tanzania yetu hii.

CCM ( Chama Changu Shabikia ) nitoe RAI Kwenu kuwa Siku zingine mkiwa mnafanya ' Michakato ' yenu ya Kumpata Mgombea Urais zingatieni sana Kigezo cha Kumpima Akili huyo Mgombea lakini pia angalieni Rekodi zake za nyuma ( hasa Kimaadili ) kama hakuwahi hata Kuvuta Bange / Bangi au Kunusa Petroli.

Kwa haya ' Mabaya ' yote yaliyofanywa ndani ya Serikali ya Hayati Rais Dkt. Magufuli na hawa ' Intarahamwe ' wake Watatu Sabaya, Makonda na Mnyeti ( kwa Uratibu wa karibu kabisa wa Mpwa wake Dotto James ) CCM tusikwepe ' Lawama ' hizi na badala yake tukiri tulifanya Makosa na ikitupendeza ( japo nadhani ni Muhimu na kuna Ulazima ) basi Chama kiwaombe Radhi ( Msamaha ) Wananchi na hasa hasa wale Wahanga wa ' Madhila ' yote na ' tutubu ' pia Dhambi zetu kwa Mwenyezi Mungu.
 
Kuna mambo yenye uharisia na fake hapa.

Tafadhari, ukiandika vitu ujitahidi kuandikaa vyenye uharisia tu. na kama ni vya uongo basi vyote viwe vya uongo. Ukivichanganya tu vyote vinakuwa vya uongo.
 
Wakati utafika kuna watu watawajibika kwa yaliyotokea kuanzia Samia, JK na wengine. Nani angeamini kwamba Sabaya angefungwa pingu na maaskari waliokuwa wakimpigia saluti?
 
Wanasiasa na wana CCM walioiva na kukomaa kisiasa kama wewe ni wachache sana...wamebaki lundo la wajinga na wafata mkumbo. Na Waimba mapambio
 
"Mungu tu ndo anajua corona imeondoka na nani"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…