CCM tulifanya kosa kubwa sana 2015, tusirudie tena. Chuki iliyopo ni kubwa sana

π™½πšŠπš˜πš–πš‹πšŠ πš”πšžπšŽπš•πš’πš–πš’πšœπš‘πš πšŠ! π™·πš’πšŸπš’ 𝙲𝙲𝙼 πš’πš–πšŠπš›πšŠ πš—πš’ πš‘πš’πš™πš’? πšŠπš—πš£πš’πšŠ πšŠπš πšŠπš–πšž 𝚠𝚊 πš”πš πšŠπš—πš£πšŠ πš–πš™πšŠπš”πšŠ 𝚒𝚊 5 𝙲𝙲𝙼 πš‘πš’πš™πš’ πš’πš•πš’πš”πš πšŠ πš’πš–πšŠπš›πšŠ πšŒπš‘πš’πš—πš’ 𝚒𝚊 πš–πš πšŽπš—πš’πšŽπš”πš’πšπš’ πš’πšžπš™πš’?
 
Subiri mataga waje watamtukana balaa.
Ukisema Mataga unakosea,,sema genge" kwani mataga wengi waliishi kinafki lakini hawakupenda tabia za jiwe. Mataga imegawanyika kuna ambao wapo na mama na wale wa legacy[emoji3].
Hawa wa legacy ndiyo mashabiki wa , makonda ,sabaya ,musiba na wengine sampuli hizo.
 
Yule bwana tangu day one sikuwahi kumkubali. Hua natafakari sana kama nchi tulikofikia lkn watu wakaamua kukaa kimya na kama sio zawadi ya kifo aliyoitoa Mungu kwa mwanadamu sijui ingekuwaje.
 

Ni maoni yako, hongera, nitayaheshimu licha ya kuwa sikubaliani nayo. maana yamejikita kwenye upande mmoja tu wa pande mbili za binadamu. kwa asili binadamu hakosi udhaifu, lakini pia hakosi uhodari.
Hili andiko, binafsi naona kama ni namna ya kueneza chuki dhidi ya rais aliyeondoka. Ambalo linajaribu kumuua Magufuli, lakini nieleze kwa kifupi tu, "wanaotaka kumuua Magufuli hawatafanikiwa".
 
Hata siku moja hatakuja rais aliyekamilika. Tukipata mwanadiplomasia mzuri atakuwa na sifa fulani ya uvivu. Huyo JK CCM ambako ndiko nyumbani palipomkuza mpaka akawa maarufu palielekea kumshinda mpaka ukaandaliwa mkakati maalum wa kumtumia Asha Migiro na Mzee Kinana ili waende wakapige magoti kwa wananchi, walitumia mkakati wa 'kuangukia' watu waliokuwa wamechoshwa na madudu.

JPM alifanya kazi ngumu ya kufufua ATCL huku akilazimika kuwa mkali ili wale waliozoea kufanya kazi kizembe waweze kuchangamshwa.

Kufufua shirika la reli ambalo JK na BWM walilishindwa kabisa haikuwa kazi ndogo, alihitajika JPM asiyecheka na kima ili safari ya treni iweze kufika Moshi baada ya miaka 25.

JPM hakuwa mwanadiplomasia, hakuwa na nguvu ya ushawishi ambayo ni sifa ya kawaida ya mwanasiasa mwenye kuongoza nchi, alijaaliwa uwezo mkubwa wa kusimamia wote waliokuwa chini yake.

Tumuongelee JPM kwa udhaifu aliokuwa nao lakini JPM baada ya kuondoka JKN alipaswa kuwa rais wa pili. Nchi yetu ambayo ndio inakaribia kufikisha umeme katika vijiji vyote ilimhitaji kiongozi mchapakazi wa kweli mwaka 1985, leo hii tungekuwa tumeshaweza kufanya mengi makubwa.

Hivyo ushawishi wa JK wa awamu hii ya sita bado hauna nguvu ya kuweza kuwasahaulisha watu udhaifu wa awamu yake.
 
Subiri mataga waje watamtukana balaa.
Dk aliong'olewa meno Kwa plaizi lini, mwandishi wa mbeya alitumbuliwa utumbo lini?,kiufupi serikali zote no dhalimu ukiwasumbua wanakukili.
 
Wewe hujitambui na huijui CCM ya 2015 ilikuwaje. Wewe ungeweza kupita Kariakoo na gwanda la CCM? Makosa yalizoeleka ndani ya CCM kiasi bado mtu kama wewe unatamani kurudi kwenye ushenzi tuliofanyiwa kabla ya hapo.
 
Natamani Kikwete asome uzi huu!!na Nape,kinana!!wajue mwendazake katufanya wazee kabla ya wakati!!ona sura za vijana zilivyokunjamana!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…