CCM: Tumepokea kwa mstuko mkubwa taarifa za kifo cha Christina Kibiki aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiyojulikana

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
CHAMA CHA MAPINDUZI
TAARIFA KWA UMMA
Dodoma, Tanzania


Chama cha Mapinduzi, kimepokea kwa mstuko mkubwa taarifa za kifo cha Katibu wa CCM Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa, Bi Christina Kibiki aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiyojulikana.

Marehemu alikuwa anajindaa kuhudhuria Semina elekezi kwa Makatibu Mjini Dodoma kesho.

Chama Cha Mapinduzi kinatoa pole kwa familia, ndugu, viongozi na wanachama wa CCM Mkoa wa Iringa kufuatia kifo cha ghafla na cha kikatili.

Tunawaomba wanachama wetu wawe watulivu wakati vyombo vya dola vikifuatilia na kuchunguza tukio hili, ili wahusika waweze kufikishwa katika vyombo vya kisheria.

CPA. Amos Gabriel Makalla
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA,
ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO

13 Novemba,2024
Pia soma ~ Iringa: Katibu wa CCM Kilolo avamiwa na kuuawa na Watu wasiojulikana
 
Usalama wa Taifa imeshindikana kabisa kudhibiti haya matukio?
 
Drama
 
Tujifunze kuzoea vifo, vifo ni vya kawaida na hakuna atakayeishi milele.
 
RIP Kada wa chama cha Mapinduzi


Polisi watoa taarifa rasmi uchunguzi unaendelea kuwabaini watu waliotekeleza tukio hilo la kinyama.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…