CCM tumepoteana; tunasapoti Jambo dakika moja viongozi wanatugeuka!

CCM tumepoteana; tunasapoti Jambo dakika moja viongozi wanatugeuka!

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
761
Reaction score
6,985
Wana CCM tunawakati mgumu sana mitandaoni na hata maskani tunapokaa, tumekosa confidence yakusimamia mijadala kwa sababu hatujui msimo wa chama na serikali ni upi.

Leo hii kila mada inayoibuliwa tukaitetea mwisho wa siku tunaumbuka, tumekuwa watu wakudelete posts zetu kuepusha fedhea.

Mifano michache Ni hi ifuatayo

Tulishabikia mfumo wa ukusanyaji Kodi nakuwaita wapinzani vibaraka wa mabeberu ila Leo hii clip zetu zinasambazwa mitandaoni tuonekane viongozi wetu si Wazalendo. Upepo umebadilika.

Tumetoka muda mfupi kusimama na serikali yetu na chama kuhusu vifurushi, nakuwakashfu sana wananchi. Chini ya saa 24 Makamu wa Rais na TCRA wamekuja na ujumbe wakusitisha huduma mpya za vifurushi, tumebaki kimya hata kwenye familia tunaonekana waongo. Hii ya vifurushi tulisimama na Ndugulile toka February Leo wanyonge wamepiga kelele tumeachwa na viutetezi uchwara vyetu.

Tulishadadia kwa nguvu kamata kamata na makesi ya uhujumu uchumi, juzi mama kasema kinyime kabisa na misimamo yetu nakutufanya tuonekane tulitetea mateso ya wasio na hatia.

Kwa mifano hii michache nakubaliana na wale wanaosema njia ya mwongo ni fupi , pia nawaunga mkono wanaosema mwenye nacho amjui mwenye njaa. Wana CCM tumeacha kufikiri nakuona tumebaki kuwa watu wakufikirishwa na kuonyeshwa.

Tutalisaidia Taifa pale tutakapoamua kusimama na wananchi nakuacha kabisa kusimama na viongozi. Misimamo na mitazamo ya viongozi inabadilika kulingana na upepo wa ulaji uliopo lakini matatizo ya wananchi na shida zao siku zote zinabaki zilezile. Mahitaji ya wananchi yatabaki kuwepo bila kujali kauli za viongozi waliopo. Tubadilike tumechoka kuonekana mazumbukuku kwa werevu.
 
 
Juzi nime delete post mbili...
Hii inaonyesha hamna msimamo ninyi kama ninyi ila mnasubiri serikali imamue ndo muunge tela. Ni sawa na ile katuni ya gado iliyoonyesha kuwa, oli uwe mwana ccm kamili lazima uutoe ubongo wako na kuanza kutumia ubongo wa mwenyekiti wa chama.

Jifunzeni kukisimamia kile mnachokiamini.

CCM OYEEE
 
Back
Top Bottom