CCM tumfukuze uanachama Askofu Gwajima, hana busara

CCM tumfukuze uanachama Askofu Gwajima, hana busara

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,252
Reaction score
8,003
Kama ambavyo tumekuwa tukiimba kwa katiba bora yetu ya Chama kuliko vyama vyote nchini na Afrika,ni wazi kabisa kua Askofu Gwajima ameleta sintofahamu kubwa sana nchini huku akijua kitendo kile kilikua ni cha uchochezi wa makusudi na alidhamiria.

Mwanachama mzima wa CCM huwezi kusimama uansuambia umma kwanini Corona imeibuka baada ya Magufuli kufa, huwezi kumwambia Mkuu wa nchi anashadadia misaa ya Bilgate ili wananchi wachomwe chanjo ya Corona wafe, huu ni upotoshaji, udhalilishaji wa viongozi wa nchi na ni uchochezi mkubwa sana si wa kufumbia macho.Hivi kweli Mhe Rais anaweza kuwaongoza wananchi wake kwenye kifo?

WITO KWA CCM: Naomba Askofu Gwajima achukuliwe hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kumfuta uanachama ili arudi Kanisani kwake akaendelea kupotosha watu na kuhubiri uongo wake. Jimbo liwekwe wazi kuna wanaccm safi Kawe ni imani yangu kua tukirudia uchaguzi tutashinda tena na tutapata mwakilishi mzuri.

Matamshi ya Gwajima si ya bahati mbaya bali ni kusudi la kutaka kuleta mpasuko wa kitaifa ambao mpaka sasa kuna chuki kubwa sana umejengeka miongoni mwa wananchi.Damage ya matamshi yake ni kubwa sana si wa kuachwa.Amedhalilisha mamlaka za nchi kwa kiasi kikubwa sana.
 
Huwa najiuliza kwanini Tanzania na labda hata Africa tupo nyuma sana lkn kiukweli tuna watu wengi sana kama huyu Gwajima na hicho ni moja ya vielelezo vyetu ni kwa nini tupo gizani na mbaya ndo wanao tuongoza kuanzia ki imani/kiroho mpaka ktk Siasa /Serikali

Kujadili utimilifu wa Chanjo kwa uhasi au uchanya inaweza kuwa si kitu kibaya lkn kukataza Umma wa watu wote na bila kutoa mbadala wake kwa kigezo cha Mzungu hana nia nzuri na sisi (hapa tuseme kuna labda ukweli kwa ujumla) Lakini tunatumia karibu vitu vingi vya huyo mtu mweupe kwa asilimia kubwa sasa ujanja wetu upo wapi zaidi ya kuonyesha uzuzu wetu au kusema wakuu wa Nchi wamehongwa na kutoa tuhuma nzito kama hiyo ni kielelezo kingine cha hawa manabii au masheikh kutumia ushawishi wao ktk jamii kwa namna hasi (na baadhi yao utakuta wana tuhuma za wazi kabisa za uzinzi, ulawiti, ushirikina) lkn kwa kuwa tuna hofu na kuwapa imani na nguvu kubwa wanatugeuza wanavyotaka kwa ujinga na uzwazwa wetu na tunaona kama ni watu wenye utukufu fulani kumbe ni wajanja wajanja na wanatumia udhaifu wetu wa kupokea bila kuhoji mambo kwa mgongo wa Dini/Mungu

Na mbaya zaidi sie Waafrika tunaweza pinga mambo mengi ya watu weupe (Wazungu) japokuwa kiukweli hatuna hata mikakati ya kuwa na vya kwetu kama jamii zingine hasa za Asia lkn kwenye hizi dini zilizoletwa tena na huyo mtu mweupe tumefika mpaka tunamuona yeye ndo hamjui Mungu sie ndo tunamjua ( hapa tuliiga mpaka tumezidisha)

Israel ndo Taifa linalo ongoza kwa kuwapatia chanjo ya Covid kwa asilimia kubwa Raia wake,Papa kachanjwa , na huko Mecca hata kuhiji imekuwa tabu lkn Gwajima wa hapo sijui Kimara Baruti eti ndo mtaalam kuliko wengine dah inasikitisha sana

Watu wa aina hii ni kielelezo kwa zama hizi tunaishi ki primitive

Kujadili ufanisi wa chanjo sio shida bali kutoa suluhisho bila mbadala (sio nyungu maana kuna mazingira imeshindwa nayo) ni tatizo na ikizingatiwa ktk jamii yetu kuna wenzetu wamepoteza wapendwa wao kwa huu ugonjwa
 
Kama ambavyo tumekuwa tukiimba kwa katiba bora yetu ya Chama kuliko vyama vyote nchini na Afrika,ni wazi kabisa kua Askofu Gwajima ameleta sintofahamu kubwa sana nchini huku akijua kitendo kile kilikua ni cha uchochezi wa makusudi na alidhamiria....
Timueni kule yule mwongo na mlaghai
 
Kama ambavyo tumekuwa tukiimba kwa katiba bora yetu ya Chama kuliko vyama vyote nchini na Afrika,ni wazi kabisa kua Askofu Gwajima ameleta sintofahamu kubwa sana nchini huku akijua kitendo kile kilikua ni cha uchochezi wa makusudi na alidhamiria...
CCM siyo kama CHADEMA haikurupukii mambo! Ina strategy zake! CCM itaenda inamfyonza Gwajima taraaatibu akisha dhoofu kabisa ndo inamtema!
 
Hana maadili ya uongozi, CCM ifuate mfano wa klabu ya simba kumtimua Manara
 
Mawazo ya kidikiteta haya. Si mwenyekiti wa CCM keshasema chanjo ni hiari? Gwajima anapita mulemule. Una haki ya kumsikiliza na kumuamini 'askofu' Gwajima, Dr. Gwajima au Samia Suluhu. Jifunzeni kuwa wavumilivu kusikia vitu msivyovipenda

Gwajima amekataa unafiki na ile tabia ya woga/kufuata mkumbo.
 
Kama ambavyo tumekuwa tukiimba kwa katiba bora yetu ya Chama kuliko vyama vyote nchini na Afrika,ni wazi kabisa kua Askofu Gwajima ameleta sintofahamu kubwa sana nchini huku akijua kitendo kile kilikua ni cha uchochezi wa makusudi na alidhamiria...
PERSECUTIONS.

Angalua gwajima anatetea maslahi ya taifa. Ninyi majizi mliojichotea mafedha baada ya kufa Magufuli, mnaotaka kumkwamisha Rais na kurejesha ufisadi wa awamu ya nne, mnawezaje kuwa na uajsiri huu?

Ni upumbvu ulioje kuanza kuwa persecute wenye mawazo tofauti na ninyi ambao wanatoa hoja zao binafsi nje ya ulingo wa siasa? Au mnataka kum kolimba nayeye? Pumbavu sana
 
Huwa najiuliza kwanini Tanzania na labda hata Africa tupo nyuma sana lkn kiukweli tuna watu wengi sana kama huyu Gwajima na hicho ni moja ya vielelezo vyetu ni kwa nini tupo gizani na mbaya ndo wanao tuongoza kuanzia ki imani/kiroho mpaka ktk Siasa /Serikali....
Umeandika paragraph nyingi ugoro mtupu
 
Pombe akiwa anaigiza na Gwajima, ccm kama ibilisi
 

Attachments

  • VID-20210728-WA0040.mp4
    1.5 MB
CCM siyo kama CHADEMA haikurupukii mambo! Ina strategy zake! CCM itaenda inamfyonza Gwajima taraaatibu akisha dhoofu kabisa ndo inamtema!
Askofu Rashid Gwajima ameishika CCM na Serikali yake pabaya wamebakia kubweka bweka tu lakini hawana cha kumfanya. Gwajima huyu ana watu, wakimgusa anakinukisha ile mbaya.
 
Taifa ili liendelee linahitaji fikra mbali mbali.

Hivyo basi sio sahihi kuzodoana mtu anapotoa maoni yake ambayo unafikiri hayaendani na yako.

Ndio Mungu katuumba namna hiyo hatuwezi fanana wote namna ya kufikiri.
 
Back
Top Bottom