Huwa najiuliza kwanini Tanzania na labda hata Africa tupo nyuma sana lkn kiukweli tuna watu wengi sana kama huyu Gwajima na hicho ni moja ya vielelezo vyetu ni kwa nini tupo gizani na mbaya ndo wanao tuongoza kuanzia ki imani/kiroho mpaka ktk Siasa /Serikali
Kujadili utimilifu wa Chanjo kwa uhasi au uchanya inaweza kuwa si kitu kibaya lkn kukataza Umma wa watu wote na bila kutoa mbadala wake kwa kigezo cha Mzungu hana nia nzuri na sisi (hapa tuseme kuna labda ukweli kwa ujumla) Lakini tunatumia karibu vitu vingi vya huyo mtu mweupe kwa asilimia kubwa sasa ujanja wetu upo wapi zaidi ya kuonyesha uzuzu wetu au kusema wakuu wa Nchi wamehongwa na kutoa tuhuma nzito kama hiyo ni kielelezo kingine cha hawa manabii au masheikh kutumia ushawishi wao ktk jamii kwa namna hasi (na baadhi yao utakuta wana tuhuma za wazi kabisa za uzinzi, ulawiti, ushirikina) lkn kwa kuwa tuna hofu na kuwapa imani na nguvu kubwa wanatugeuza wanavyotaka kwa ujinga na uzwazwa wetu na tunaona kama ni watu wenye utukufu fulani kumbe ni wajanja wajanja na wanatumia udhaifu wetu wa kupokea bila kuhoji mambo kwa mgongo wa Dini/Mungu
Na mbaya zaidi sie Waafrika tunaweza pinga mambo mengi ya watu weupe (Wazungu) japokuwa kiukweli hatuna hata mikakati ya kuwa na vya kwetu kama jamii zingine hasa za Asia lkn kwenye hizi dini zilizoletwa tena na huyo mtu mweupe tumefika mpaka tunamuona yeye ndo hamjui Mungu sie ndo tunamjua ( hapa tuliiga mpaka tumezidisha)
Israel ndo Taifa linalo ongoza kwa kuwapatia chanjo ya Covid kwa asilimia kubwa Raia wake,Papa kachanjwa , na huko Mecca hata kuhiji imekuwa tabu lkn Gwajima wa hapo sijui Kimara Baruti eti ndo mtaalam kuliko wengine dah inasikitisha sana
Watu wa aina hii ni kielelezo kwa zama hizi tunaishi ki primitive
Kujadili ufanisi wa chanjo sio shida bali kutoa suluhisho bila mbadala (sio nyungu maana kuna mazingira imeshindwa nayo) ni tatizo na ikizingatiwa ktk jamii yetu kuna wenzetu wamepoteza wapendwa wao kwa huu ugonjwa
Nimekusoma mkubwa na kuielewa concern yako...
Lakini mimi nina neno moja kwa namna ninavyolitazama jambo hili...
Kwamba, mara baada ya huyu mchungaji mwaka 2020 kutangaza kuingia ktk siasa za majukwaani moja kwa moja kupitia CCM na kugombea ubunge jimbo la Kawe, DSM nilishangaa sana na kuona sasa anapotea katika huduma ya kiroho...
Sasa bila shaka yoyote, nimetambua kuwa, kumbe I was wrong...!!
Nimetambua bila shaka yoyote kuwa, kumbe Bishop Rev. Josephat Gwajima yuko CCM na kupewa ubunge kwa kusudi maalumu la ki - Mungu..
Wote tunafahamu kuwa chini ya mfumo wetu utawala uliopo, watu wengi wanaingia ktk siasa na kuwania nafasi za uongozi wa kisiasa kama udiwani au ubunge kwa kutazamia kunufaika kimaslahi ya kimwili zaidi...
Lakini kwa Bishop Rev. Josephat Gwajima siyo kwani hahitaji fedha chafu za kisiasa. Tayari baba yake [Mungu Yehova] amempa na anampa fedha nyingi na utajiri usio wa kawaida kawaida..!!
That's to say, he is there for a special mission ambayo hata serikali na CCM hawaijui na hawakuweza kuijua kwa sababu mission hiyo inawalenga wao, ni rungu lao la kuwapiga...
Point yangu ni hii;
KWANZA, Rev. Gwajima hatabadili msimamo wake
PILI, kadiri watakavyoendelea kumsakama naye ndivyo atakavyoendelea kukusisitiza na kukandamiza anachokiamini tena kwa maneno makali zaidi yatakayowakera wenye mamlaka...
Wenye kumbukumbu rejeeni ishu ya mahakama ya kadhi mwaka 2012/2013 wakati wa Kikwete na mgogoro wa yeye na Paul Makonda aliyekuwa RC DSM few years ago...
TATU, Bishop Rev. Josephat Gwajima akiingia kwenye mgogoro na mamlaka za kidunia au serikali za kibinadamu aidha serikali nzima au kiongozi mmoja mmoja huwa HASHINDWI bali mara zote HUSHINDA...!
Na sababu ni moja tu: Yeye anatumikia ufalme wenye nguvu zaidi kuliko falme zote duniani wanaozitumikia hao anaoingia nao kwenye mgogoro...
Na ufalme anaoutumikia ni ule wa mbinguni na mfalme wake ni YESU KRISTO mfalme wa wafalme. Hakuna mfalme au ufalme ulio juu ya huu...!!!
WHAT THEY SHOULD TO DO?
1. AIDHA, wafuate ushauri na maelekezo yake kuhusu haya mambo huku wakijua kuwa asemaye ni "JITU LILILOTOKA MBINGUNI"
2. AMA, wapuuze na wamkabili kwa kutumia ushauri kama huu unaotolewa humu na mleta mada. Na wote tunaelewa ujinga wa utawala wa CCM. Hawataishia kumfukuza uanachama tu bali watajaribu hata kumdhuru ikiwemo kumuua....
What they don't know about this man is that, HE IS IMMORTA, he is indestructible...
WHAT I PERSONALLY SEE IS;
Possibility kubwa ni kutumia option namber two. Watamkabili na ikifanyika hili KUSUDI LA HUYU MTU KUWA MBUNGE WA CCM litakuwa wazi na litaanza kutekelezeka vigorously kinyume na matarajio ya serikali ya CCM kupitia mtu waliyemdhania yuko upande wao...!!
Ni mtazamo na maoni yangu tu haya