Huwa najiuliza kwanini Tanzania na labda hata Africa tupo nyuma sana lkn kiukweli tuna watu wengi sana kama huyu Gwajima na hicho ni moja ya vielelezo vyetu ni kwa nini tupo gizani na mbaya ndo wanao tuongoza kuanzia ki imani/kiroho mpaka ktk Siasa /Serikali
Kujadili utimilifu wa Chanjo kwa uhasi au uchanya inaweza kuwa si kitu kibaya lkn kukataza Umma wa watu wote na bila kutoa mbadala wake kwa kigezo cha Mzungu hana nia nzuri na sisi (hapa tuseme kuna labda ukweli kwa ujumla) Lakini tunatumia karibu vitu vingi vya huyo mtu mweupe kwa asilimia kubwa sasa ujanja wetu upo wapi zaidi ya kuonyesha uzuzu wetu au kusema wakuu wa Nchi wamehongwa na kutoa tuhuma nzito kama hiyo ni kielelezo kingine cha hawa manabii au masheikh kutumia ushawishi wao ktk jamii kwa namna hasi (na baadhi yao utakuta wana tuhuma za wazi kabisa za uzinzi, ulawiti, ushirikina) lkn kwa kuwa tuna hofu na kuwapa imani na nguvu kubwa wanatugeuza wanavyotaka kwa ujinga na uzwazwa wetu na tunaona kama ni watu wenye utukufu fulani kumbe ni wajanja wajanja na wanatumia udhaifu wetu wa kupokea bila kuhoji mambo kwa mgongo wa Dini/Mungu
Na mbaya zaidi sie Waafrika tunaweza pinga mambo mengi ya watu weupe (Wazungu) japokuwa kiukweli hatuna hata mikakati ya kuwa na vya kwetu kama jamii zingine hasa za Asia lkn kwenye hizi dini zilizoletwa tena na huyo mtu mweupe tumefika mpaka tunamuona yeye ndo hamjui Mungu sie ndo tunamjua ( hapa tuliiga mpaka tumezidisha)
Israel ndo Taifa linalo ongoza kwa kuwapatia chanjo ya Covid kwa asilimia kubwa Raia wake,Papa kachanjwa , na huko Mecca hata kuhiji imekuwa tabu lkn Gwajima wa hapo sijui Kimara Baruti eti ndo mtaalam kuliko wengine dah inasikitisha sana
Watu wa aina hii ni kielelezo kwa zama hizi tunaishi ki primitive
Kujadili ufanisi wa chanjo sio shida bali kutoa suluhisho bila mbadala (sio nyungu maana kuna mazingira imeshindwa nayo) ni tatizo na ikizingatiwa ktk jamii yetu kuna wenzetu wamepoteza wapendwa wao kwa huu ugonjwa