CCM tumfukuze uanachama Askofu Gwajima, hana busara

Chama cha Mataahira. mnafukuza wenye akili mbaki na sometimes YES sometimes NO
 

Chanjo kutokuwa na ufanisi na hata watu kukataa sio kitu kibaya kama kitabaki kwa muhusika mwenyewe lkn kukata watu kupata chanjo bila kuwa na mbadala na baadhi yetu wanapoteza maisha na kupoteza wapendwa wao hiyo si sawa

Huu ugonjwa bado upo kwenye hatua ya utafiti na kama ni kutapa tapa ni watu wote na races zote sio eti sababu Mzungu anataka kutumaliza sijui sie ni matajiri sana au kuna watu serikalini wamehongwa na mambo kama hayo

Bado chanjo ndo njia inayoonekana at least inafaaa hata kama kuna mapungufu yake na ibaki suala la mtu binafsi na familia yake kuamua kuchanja au hapana
 
AFRIKA UKIONGEA UKWELI UNACHUKIWA,VISA DHIDI YAKO VITAANZA!!!
 


Hapana Gwajima asifukuzwe kwani nimejaribu kutafakari kwa kina na kugundua kuwa Gwajima ni MwanaCCM halisi kama walivyo wakina Sabaya ,Makonda, Musukuma , DC Kheri, Polepole, RPC wa Kinondoni, RPC wa Mwanza, Mrundi Bashiru na Warundi Wengine.
CCM ni Chama Kinachotegemea watu wenye Roho Mbaya au Wanafiki au Wapenda mdaraka au Wakabila kama Gwajima na S. Gang wenzake wanaoiyumbisha nchi.

Mwenda Zake alipiga mzinga wa Nyuki mawe sasa nyuki wamesambaa wanauma watu ovyo. Ukabila kwa miaka mitano ulijengwa kisawasawa. Gwajima kwenye nchi inayojipambanua kuwa ni nchi isiyo na dini hakustahili kupewa Ubunge kabla ya kutangaza kuwa ameacha kazi za madhebahuni.
Bila shaka aliruhusiwa kuchanganya dini na siasa kutokana na kabila lake.
Gwajima ni bilionea anayemiliki Kanisa lake hakupaswa kuwa mbunge tena kwa wizi wa kura.
Gwajima anashangaa kuwa chanjo ni ya wazungu wakati anatumia ndege ya mzungu na vipaza sauti vya wazungu na magari ya wazungu na TV na simu za wazungu.


Mungu anauchukia unafiki wa Waafrika kuliko ujanja wa wazungu.
Unafiki ni dhambi, uzinzi ni dhambi, wizi ni dhambi ,uuaji ni dhambi ubaguzi ni dhambi, kushitaki mtu kwa uongo ni dhambi,ushahidi wa uongo ni dhambi, dhulma ni zambi, uroho wa mali na fedha ni dhambi, kupotosha ukweli wa kura ni dhambi, chuki ni dhambi, kiburi ni dhambi, uonevu ni dhambi , kukiuka kiapo ni dhambi, ulevi ni dhambi, kutoa unabii wa uongo ni dhambi, kupora wake za watu ni dhambi, kutumia madhebahu kujitajirisha kupita kiasi ni dhambi.
CCM wote na Gwajima wana Sifa na madhambi yote hayo. Kumfukuza Gwajima ni kuhadaa umma.

Gwajima na wanaCCM wenzake ni Watu wenye roho Mbaya wanaofurahi mateso ya Watu wema yanayofanywa kwa manufaa ya Watawala walioshiba kwa dhulma.

Alikaa kimya Akwiline alipopasuliwa kichwa risasi za CCM ili tu Mgombea wa Chadema asipigiwe kura halali akamshinda yule muovu wa CCM.
Laana kwa Afrka na TZ imetokana na Viongozi wa Dini walioshikamana na Watawala Waovu kwa sababu ya fedha.

Gwajima atubu na kuhubiri toba kwa watanzania vinginevyo anajifariji tu kwani upanga umeshawekwa juu ya waovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…