CCM tumshauri Rais Samia asigombee 2025

Mleta mada sijui una umri gani... mwaka 95 wapo walioamini huu ujinga kama ww, kuwa CCM imegawanyika na kwamba huo ndio mwanya wa mgombea uraisi wa kipindi hicho ndugu Augustino .L. Mrema kushinda uchaguzi. Cha kushangaza uchaguzi ulipofika wale waliogawanyika walikuwa upande wa adui yao (mgombea uraisi wa CCM) enzi hizo hayati Benjamini Mkapa na umoja huo ukachangia ushindi wa mgombea wao. Mwaka 2005 hivo hivo style ilikuwa ni ile ile ya kuanzisha zengwe baina yao ili kuwapoteza maboya wapinzani wao, na uchaguzi ulipofika wakawa kitu kimoja kumpigania mgombea wao hadi akapata ushindi wa kishindo ambao ulikuwa zaidi ya ule wa mwaka 95. Mwaka 2015 CCM ika change strategy kwa kuanzisha ugomvi ambao safari hii ulionekana kama vile ni wa mafahari wawili wasiotaka kukaa zizi moja (JK na Lowasa) Hii ikapelekea wapinzani kuingia mkenge na kujaribu kumkaribisha fahari mmoja katika zizi lao bila kujua hasa hatima ya mipango yao (CCM) kilichofatia kila mtu anakijua. Ushindi kwa kambi ya upinzani ukosekana na chama kikasambaratika, kwa fahari huyo kurudi alipotoka na mbaya zaidi akaondoka na wabunge, madiwani na viongozi wengine wa chama. Sasa safari hii wameanza tena mchezo ule ule afu mleta mada unakuja na kushauri watu ujinga kwa lengo wa kuliingiza tena mkenge kundi fulani.
 
Mimi simpendi Mama na sijali kama ataongoza kipindi kimoja au viwili. Ninachojali chama changu cha CCM kipo madarakani.
 

Kwani mwenyewe si kasema 2025 rais si mwanamke ambaye ndiyo yeye?

Hiiiiii bagosha!
 
Waambie Polepole na Bashiru (maana tunajua ndio waliokutuma) Mama hatoki hadi 2030 watake wasitake kama vipi wahamie Burundi.
 
Mpuuzi wewe, misukule ya magufuli mtapata tabu Sana, hizo chuki zenu za kidini na ukanda zitawaghalimu
 
Dah ila Africa sijui nani atakuja kutupandikiza akili timamu, kiongoz msomi anafanya mambo usiyoyatarajia,

Wenzetu wanazid kufanya maendeleo kitechnolojia sisi tunapambana na wapinzani. Sijui ni lini tutapambana na ujinga.
 
Napendekeza badala yake Dudumizi apitishwe kuwa mgombea pekee,tena Bila kupingwa.
 
Mkimshauri msimshauri ,CCM sahauni kushinda uchaguzi halali wa nchi hii,sahauni kama mlivyosahaulishwa kule Pemba kwenye kisiwa cha karafuu.
 
Hahahaha sasa ni vibaya chadema wakishinda 2025? Ama ajira yako ni siasa itapotea?
 
Tufanye ni kweli CHADEMA wana wanachama mil. 6
Una uhakika gani kwamba wote wako LOYAL kwa chama chao? Mnapoitisha maandamano, mbona hawajitokezi?
Mh. Mbowe alipoitaka serikali itamke chanjo ya uviko 19 iwe lazima kwa kila mtz mbona wanaCHADEMA hawajajitokeza kuchanja kwa wingi? (Ushahidi ni huu: Miezi miwili tangu chanjo iletwe waliochanja hawazidi laki 5. Wafuasi wa CHADEMA kama wangejitokeza wote kuchanja dozi mil 1 zingekuwa zimeshaisha).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…