Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Mleta mada sijui una umri gani... mwaka 95 wapo walioamini huu ujinga kama ww, kuwa CCM imegawanyika na kwamba huo ndio mwanya wa mgombea uraisi wa kipindi hicho ndugu Augustino .L. Mrema kushinda uchaguzi. Cha kushangaza uchaguzi ulipofika wale waliogawanyika walikuwa upande wa adui yao (mgombea uraisi wa CCM) enzi hizo hayati Benjamini Mkapa na umoja huo ukachangia ushindi wa mgombea wao. Mwaka 2005 hivo hivo style ilikuwa ni ile ile ya kuanzisha zengwe baina yao ili kuwapoteza maboya wapinzani wao, na uchaguzi ulipofika wakawa kitu kimoja kumpigania mgombea wao hadi akapata ushindi wa kishindo ambao ulikuwa zaidi ya ule wa mwaka 95. Mwaka 2015 CCM ika change strategy kwa kuanzisha ugomvi ambao safari hii ulionekana kama vile ni wa mafahari wawili wasiotaka kukaa zizi moja (JK na Lowasa) Hii ikapelekea wapinzani kuingia mkenge na kujaribu kumkaribisha fahari mmoja katika zizi lao bila kujua hasa hatima ya mipango yao (CCM) kilichofatia kila mtu anakijua. Ushindi kwa kambi ya upinzani ukosekana na chama kikasambaratika, kwa fahari huyo kurudi alipotoka na mbaya zaidi akaondoka na wabunge, madiwani na viongozi wengine wa chama. Sasa safari hii wameanza tena mchezo ule ule afu mleta mada unakuja na kushauri watu ujinga kwa lengo wa kuliingiza tena mkenge kundi fulani.