CCM tumshauri Rais Samia kuhusu Wabunge 19

CCM tumshauri Rais Samia kuhusu Wabunge 19

Paf

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2021
Posts
1,703
Reaction score
3,307
Ndugu katibu mkuu CCM,

Ndugu wanachama,

Ni dhahiri chama kinasimamia Serikali,

Wabunge 19 waliopo bungeni bila ridhaa ya Chadema ni mtaji kwa CCM kwa sasa. Madhara yake baadae ni makubwa.

Nashauri serikali iwasimamishie mishahara yao mara moja hawa waliingia kwa jinai bungeni kupitia Chadema)

Ikiwa hoja kubalance sheria za mabunge kimataifa tunao ACT Wazalendo

CCM tutaendelea kuthibitisha kuwa hata matokeo ya uchaguzi baadhi ya maeneo ni kweli tulifoji.

Chuki za Chadema na CCM zitadumu kwasababu hatuheshimu maamuzi ya taasisi ya Chadema.

Ile kauli ya nape bungeni iheshimiwe.
 
Wakifuata Vema shauri wako

Tunatakiwa tuitishe uchaguz tena upya.

Bunge unalotaka linapoteza kabisa credibility ya kuitwa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa sheria.
 
Waache waendelee kuwemo bungeni watateswa na dhamiri yao wakati wenzao wanapambania katiba mpya.

Huoni Halima Mdee aliyekuwa anaongoza ku tweet kawa siye yeye.

Frustrations zinawatesa na sintashangaa kusikia mmoja wao kapata pressure.
 
CCM wanaweza kubadilisha katiba/ sheria kwa kumuongezea Rais idadi ya wabunge anaoweza kuteua.

Mnaweza kuweka wabunge 35 wa kuteuliwa na Raisi. Baada ya hapo Raisi anaweza kuteua hawa 19 waliokuwa Chadema bila tatizo lolote.
 
Wewe mwanaufipa ya CCM yanakuhusu nini? Mama yetu anashugulika na mambo makubwa ya kitaifa, sio hizo mbwembwe zenu.
 
Kama nyie Chadema mlishawafukuza, kwa nini bado kuchwa kutwa hamlali wanaume wazima bado mnaendelea kuwafuata wanawake wawatu? Kama wako kimakosa, fungueni kesi mahakamaniii ilikielewekeee. Sasa hivi mnataka CCM iiingilie kati, itaanzia wapi zaidi yenu mliokuwa nao huko kwenye chama chenu?
 
Kiukweli kitendo cha mama kuendeleza kuidhinisha mishahara kwa wabunge wale feki Sio sawa kamwe, kinamshushia heshima zao. Maamuzi ya taasisi zingine yaheshimiwe.
 
Kiukweli kitendo cha mama kuendeleza kuidhinisha mishahara kwa wabunge wale feki Sio sawa kamwe, kinamshushia heshima zao. Maamuzi ya taasisi zingine yaheshimiwe.
ili hizo fedha wapewe akina nani? na ili hao wawakilishe nini? achia fursa za watu
 
Back
Top Bottom