CCM tuseme wazi kuwa tunaogopa katiba mpya, tuche visingizio vya kujenga uchumi kwanza

CCM tuseme wazi kuwa tunaogopa katiba mpya, tuche visingizio vya kujenga uchumi kwanza

Fundi Madirisha

Senior Member
Joined
Jun 30, 2020
Posts
184
Reaction score
1,000
Hii habari ya kusema eti kipaumbele ni kujenga uchumi kwanza wakati Magufuli pia alisema hivyo hivyo matokeo yake miaka mitano ikapita hajafanya lolote. Tusiwadanganye wananchi na wala tusitafute huruma yao, ni uchu wetu wa madaraka tu hakuna kiingine. Mnahisi na mnaufahamu udhaifu wa chama chetu kwa sasa kimebakia kukumbatiwa na dola hata JK aliwahi kutuambia hivyo. Chama chetu limekosa uhalali wa wananchi.

Katiba ya mzee Warioba na Inayopendekezwa zote hazitambui nafasi za Wakuu wa Mikoa na wilaya, iliondoa hicho cheo kwa sababu hawa ni viongozi Makada wa chama hawala na hapo hapo wanatakiwa kua fair kwa rais wote. Sasa hawa wakuu wa mikoa na wilaya ndio kwa sababu wanajua wako hatarini kupoteza nafasi zao, wao ndio wako mstari wa mbele kuzima mijadala ya katiba. Mpuuzi mmoja aliyekaa kiburi alisema atawasaga saga wanaojadili Katiba mpya.

Kwahiyo tuelewe kabisa na CCM tunajua kua hitaji la katiba ni mwiba kwetu, hatutapata pa kupumulia tusisubiribtusukumwe na maumivu makali kuipata katiba. Tusisukumwe na matukio mabaya kuipata katiba, tukikataa katiba kwa sasa halafu badae inapatikana kwa maumivu na matukio mabaya ndio utakua mwisho wa chama chetu. Hivi chama kinataka heshima gani zaidi ya katiba bora kwa wananchi?

WanaCCM twatambua kua tupo katika mfumo wa vyama vingi lakini mwongozo wa taifa ni wa enzi za chama kimoja, maana yake hatutaweza kwenda lazima mpya upatikane tusilazimishe mazingira haya dunia imebadilika.Katiba mpya haizuii kujenga uchumi tuache kuwahadaa wananchi, mijadala ya katiba inaweza kuendelea huku tunajenga uchumi.
 
Ukijitokeza wanakukamata were gaidi.Anza kuomba hifadhi nje,wenzio hawataki ukweli.Uchumi huku unatumia gharama kubwa kumkamata MTU mwenye taasisi badala yakumwandikia barua afike kituo Fulani Siku kwa mahojiano.
Demokrasia huanzia nyumbani
 
Waje kijiji kwetu Meatu wakikamatwa kwa kusema ukweli niko tayari. Hii dunia sote tunapita hata mnyanyasaji naye hufa
 
Shida ya haya mambo ni ule uchaguzi wa October 2020..
Wangebalance matokeo hata kuweka wabunge wa kuchaguliwa 20..
Kiufupi wapinzani walishinda majimbo mengi.. Zaidi ya 50 ...
Lakini waheshimiwa wetu wa chama tawala hawakutaka hivyo
 
liko wazi. Lakini wataogopa mpaka lini?? Better Early than Late.
 
CCM inajenga uchumi gani tena wakati ilishatangaza kuwa tupo uchumi wa kati?Wanataka tuwe developed country ndiyo waukubali mchakato wa katiba mpya?
 
Shida ya haya mambo ni ule uchaguzi wa October 2020..
Wangebalance matokeo hata kuweka wabunge wa kuchaguliwa 20..
Kiufupi wapinzani walishinda majimbo mengi.. Zaidi ya 50 ...
Lakini waheshimiwa wetu wa chama tawala hawakutaka hivyo
Wewe ndo umemaliza walifanya kosa kubwa saaana, yaani wangewaacha kina Mbowe,Lema,Heche,Sugu,msigwa na baadhi Kama 14,,, haya yote yasingetokea, ukweli ni kuwa hii ishu ni ngumu na wapinzani wako serious
 
Wizi na laana za magufuli za oktaba 2020 zitaqatesa sana hawa majizi wa kisiasa.
 
Wewe ndo umemaliza walifanya kosa kubwa saaana, yaani wangewaacha kina Mbowe,Lema,Heche,Sugu,msigwa na baadhi Kama 14,,, haya yote yasingetokea, ukweli ni kuwa hii ishu ni ngumu na wapinzani wako serious
Hii ngoma haitakaa iishe. Wananchi wanaelewa. Sio wale wa mwaka 1995
 
Hii ngoma haitakaa iishe. Wananchi wanaelewa. Sio wale wa mwaka 1995
Aisee hii ngoma ngumu yaani Jana tu dunia nzima imejua kuwa Tanzania watu wanaitaji katiba,, believe me Mbowe akikaza Samia atawaita kwenye drawing table
 
Aisee hii ngoma ngumu yaani Jana tu dunia nzima imejua kuwa Tanzania watu wanaitaji katiba,, believe me Mbowe akikaza Samia atawaita kwenye drawing table
Jiulize kilichomwondo Jiwe. Asifanye masihara na tanzania
 
Kipaumbele ni kuboresha maisha ya mtanzania kwa kukuza uchumi
 
Hao ni wapumbavu hawajielewi. Wacheni wanaonufaika nayo waipende. Mtu maskini anashabikia katiba iliyojaza mafisadi na majizi😅😅
Inasikitisha. Mbaya zaidi raisi na marafiki zake wanajijengea wigo eti wasishitakiwe kwa makosa waliyoyafanya wakiwa madarakani, huu Ni uhuni daraja la juu kabisa. Tunataka katiba moya Tena ile ya Warioba
 
Wana Ccm wengi hata hawaelewi wananchi wanalalamikia nini !!. Na history ya Africa inaonekana jambo hilo haliwezi kupatikana kwa amani.

Ccm na serikali zake za Tanganyika & Zanzibar hawako tayari kwa sababu tu ya uchu na ulevi wa madaraka. Hawakubali fair ground hasa katika swala la uchaguzi . Wanataka waingie kwenye uchaguzi wakiwa wamemkumbatia vyombo vya Dola
 
Back
Top Bottom