CCM: Tutamjadili kwanza Benard Membe

CCM: Tutamjadili kwanza Benard Membe

Etwege

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2018
Posts
7,207
Reaction score
17,674
Chama cha Mapinduzi kimemjibu aliyekuwa mgombea urais wa Act Wazalendo mwaka 2020 na baadae kutangaza kujitoa kwenye chama hicho, na sasa ametangaza safari ya kurudi CCM chama chake kilichomlea na baadae kumfukuza kutokana na utovu wa nidhamu kuwa kitamjadili kwanza ili wamuone kama wamkubalie kurudi CCM au la.

CCM yazungumzia kauli ya Membe

=======

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema yuko njiani kurudi mahali fulani akishamaliza kusikiliza uamuzi wa shauri lake lililopo mahakamani Oktoba 12, mwaka huu.

Licha ya Membe kutoweka wazi mahali atakaporudi lakini inaonekana atarejea Chama cha Mapinduzi (CCM) alikovuliwa uanachama Februari 28, 2020 kwa madai ya kukiuka maadaili na mwenendo usioridhisha tangu mwaka 2014

Jana akiwa kwenye mkutano wa ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Membe alisema anamuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan na yupo tayari kumpigia kampeni katika Uchaguzi Mkuu 2025.

Hata hivyo, Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM, Kanali Ngemela Lubinga alisema kama alivyoondoka, akiomba kurejea atajadiliwa.

“Akiomba vikao vinavyohusika vitamjadili, vinaweza kumpokea au kumkataa. Aliondoka na anataka kurudi, basi kuna taratibu na kanuni. Ataomba, atajadiliwa, akionekana ana sifa za kurudi basi atarudi. Asipofikia kiwango atakataliwa,” alisema Lubinga alipozungumza na Mwananchi kwa njia ya simu.

Julai, 2020 Membe alijiunga na chama cha ACT Wazalendo na baadaye aliteuliwa kuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu akichuana na John Magufuli (CCM) na Tundu Lissu (Chadema) na wagombea wengine.
 
Chama cha Mapinduzi kimemjibu aliyekuwa mgombea urais wa Act Wazalendo mwaka 2020 na baadae kutangaza kujitoa kwenye chama hicho, na sasa ametangaza safari ya kurudi ccm chama chake kilichomlea na baadae kumfukuza kutokana na utovu wa nidhamu kuwa kitamjadili kwanza ili wamuone kama wamkubalie kurudi ccm au la.

CCM yazungumzia kauli ya Membe | Mwananchi - CCM yazungumzia kauli ya Membe
Maghayo soma hapa.
 
Imeisha hiyo, Lubinga usitupotezee muda, Membe anarudi tu!
 
Kwa watu wenye akili timamu, ukimuangalia Membe kwa matendo yake yanayonekana hana sifa ya kuwa kiongozi kwenye Taifa, hapo hujaingia ndani kuangalia matendo yaliyo nyuma ya pazia. Yeye ni mfano wa viongozi wengi tulionao sasa serikalini. Hawana maono yoyote kwa taifa, zaidi ya kusuka mitandao ya kubaki hapo walipo na kuzidi kupiga pesa. Tanzania imekwama na inazidi kuchakaaaaaaa.
 
Msaliti lazima ajadiliwe
Mkuu membe anakutesa sana!!zile zilikuwa chuki binafsi za jiwe, sasa hayupo na jamaa anarudi kwa kishindo, mwendazake masalia mtapiga kelele sana lakini ni machozi ya samaki!!unadhania jana kwenye mkutano wa PM, alijipeleka tu, hukumuona nape alivyokuwa anatabasamu kwa pembeni!!jamaa lilikuwa na siasa za kishamba sana toka tumepata uhuru.MUNGU FUNDI
 
Waweke tu hiko kikao cha kupoteza muda na kudanya umma, lakini ninachojua hawana ubavu wa kumkatalia mwanadiplomasia huyo na shujaa wa awamu ya 5 !
 
Back
Top Bottom