Uchaguzi 2020 CCM tuwe wakweli, mpaka mwisho wa kampeni tunaweza tukashindwa vibaya sana

Well said .... Mkuu anaishiwa cha kuongea kila siku. .... Jana nimemuona anawambiwa watu ilani yetu iko humu huku akiwaonyesha kitabu cha kurasa 500. Sijui anategemea wapiga kura wataenda kukisoma au .... Mpaka sasa tunajua Chadema wao ni Haki, Uhuru na Maendeleo. ACT wao ni Kazi na Bata ..... Hivi CCM wao ni nini .....!!!!?
 
KWA akili zangu timamu upinzani unge waachia KILA kitu CCM
Serikali za mitaa,udiwani, Ubunge na urais Ingenoga sanaa.
Inafikirisha....
Ifikapo 2025 tuwapime.
Yaani wewe huja wapima tuu miaka 60 waliyo tutesa na kuifanya hii nchi takataka? Una taka uwapime kwa miaka mitano? Are you serious??? Mungu akusamehe maana hukui hatma ya maisha yako.
 
Watumishi ndio hao mnawasema hawawaongezei kitu kwenye kura zenu kwa sababu ni wachache. Kumbe hamkujua wana umuhimu mwingine
 
Ahaa wewe jamaa unatoa historia nusunusu ili ufunike kombe mwanaharamu apite.
Wakurdi walishika silaha wakitaka kuimega sehemu ya Iraq,Uturuki,Syria na Iran ili kuundaa taifa lao la Kurdistan.
mara kadhaa washapanga mipango ya kumuuwa Sadam.
Mataifa yote hayo niliyoyataja washatembeza kichapo kwa jamii ya wakurdi.
Sasa watu wenye nia ya kuimega nchi na kutaka kumuuwa Rais wa nchi unataka wapewe aiskrimu na keki za mayai?
 
Sikio la kufa halina dawa. Ccm ni KANU tarajiwa.
 
Hoja ya kuigawa nchi katika majimbo ndiyo hiyo unasema. duuuuuuuuuuuuuuuuuu
Hiyo hoja ya majimbo ipo vizuri tena sana, Hata ukiamua kuipotosha kama CCM wanavyojaribu kufanya lakini haipotosheki! Huwezi kusema eti mkiigawa nchi katika majimbo basi mtaleta mfarakano na mgawanyiko, hii kauli nyepesi sana! Hebu tupe mfano wa nchi iliyokuwa katika mfumo wa majimbo kukatokea mfarakano na kwasababu au mazingira yapi? Mbona Marekani ambao ni taifa kubwa na lilioendelea duniani ndio mfumo wao wa kiutawala wanaoutumia siku zote na hatujaona mifarakano wala migawanyiko! Hapo ni suala, la sera , sheria na miongozo ya kusimamia utaratibu huu, hayo yakiwekwa vizuri lazima tutavuka tu! Ni bora tukajaribu mfumo mpya wa kiutawala kuliko kuendelea kung'ang'ania mfumo ulioshindwa!
 
" wapo watumishi wa umma wasio waaminifu wanatoa haya"Lissu ongeza dozi
 
Hili swali nilijiuliza baada ya kuona mabango na mabendera ya CCM yanalazimishwa kila kona mpaka maeneo ambayo hayastahili.

Nikajiuliza kwa muda ambao CCM imetawala walikuwa hawana hata haja ya kuvaa sare wala kutumia wasanii na nguvu kubwa kiasi hicho,

Ukiona nguvu kubwa inatumika ujue hawakubaliki na wao wanatambua hivyo.
 
Mimi ni Chadema ila Ilani yetu hailewek i ya ubabaishaji mno.suala la majimbo limetuvua nguo
Wewe umevuliwa nguo na mashabibi acha kusingizia Ilani....Kam huelewi hoja ya Majimbo...mamlaka kwa wananchi nashauri uendelee kuvuliwa nhuo hukohuko!
Na natumaini utazoea tu!
 
Ukweli ni kwamba Campaign Team ya CCM bado haijajipanga. Hawa wasanii wanatoa a misleading message.

Ni ngumu kujua Kama kweli mnaungwa mkono au watu wanafwata wasanii. Kwa Hali ilivyo ni ngumu kufanya tathmini ya kweli ya namna mnavyokubalika wkt muda wooote mnazungukwa na mamia ya wasanii.

Tathmini ya Hali halisi ingesaidia kufanya maboresho ya mtindo wa kwenda nao kufikia ushindi.
 
Uelewa wako ni mdogo sana.. huwezi kuwa kwenye chama cha chadema.. wwe ni mamluki tu..
Wananchi hatuna haja na ilani za kwenye makaratasi TAL tunamwelewa sana,akiongea hayohayo anayoongea tunaelewa mno
 
Pumzi meko imekata,hata nusu ya kampeni hajafika keshataga,tiss,policeccm ndio tegemeo lake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…