The Khoisan
JF-Expert Member
- Jun 5, 2007
- 16,434
- 14,547
Well said .... Mkuu anaishiwa cha kuongea kila siku. .... Jana nimemuona anawambiwa watu ilani yetu iko humu huku akiwaonyesha kitabu cha kurasa 500. Sijui anategemea wapiga kura wataenda kukisoma au .... Mpaka sasa tunajua Chadema wao ni Haki, Uhuru na Maendeleo. ACT wao ni Kazi na Bata ..... Hivi CCM wao ni nini .....!!!!?Kitu ambacho narudia mara ya pili kikisisitiza, ni kwanini Mzee baba anafanya kazi ya kujibu hoja za Tundu ambaye ana akili nyingi sana na sasa ameshamjuia anacheza na milio ya midundo yake. Mimi nilisema mzee ajikite zaidi kuelezea anayotaka kuyafanya badala ya kuhangaika kumjibu Tundu, hii kazi ifanywe na kina Polepole. Hivi CCM mpya tuna shida gani tunakosa ubunifu sisi?
Tuelekeako mbele ya safari tutajikuta tunajibu hoja za Tundu tukasahau yaliyoko mbeleni. Huyu jamaa ana taarifa zote za mahali tunakoteleza, wapo watumishi wa umma wasio waaminifu wanatoa haya.Sasa tinavyozidi kumjibu ndivyo anavyozidi kuyatoa mengi ya ndani na sisi tutaendelea kumjibu.
Hawa jamaa ni wa ajabu sana, wameficha silaha zao pembeni za kampeni kama vile katibu mkuu na naibu wake, mwenyekiti wao pia wamemtangulizia Mgombea na mgombea mwenza na viongozi wa kikanda. Wanataka mwishoni watumalize sisi ambao kila safari tunaambatana timu yote.