CCM Vipande vipande, waliotuhumiwa kuuza madawa ya kulevya awamu ya 5 wapanga kujiuzulu

Kama ni kweli wako sahihi kabisa
 
Wanatakiwa wakijiuzulu na wafe kabisa wasiwepo itakuwa furaha sana...hao ndio mafisadi na wanaoshirikiana na wakwepa kodi..hii nchi imechoka umaskini kwasababu yao.
 
Naona mmeshindwa kuwatuliza Lissu na Mbowe wakae chungu kimoja mnaunga unga vistori vyenu

Makonda amewapelekea moto sana hizi week mpaka mmesahau operesheni changia mwenyekiti
Acha ujinga, Makonda hawezi kuwa tatizo la Mbowe na Lissu hata kidogo

Tatizo la Lissu na Mbowe ni kuhusu uchaguzi ujao. Kuna mmoja anataka kwenda kwenye uchaguzi hata kama hakutapatikana tume huru ya uchaguzi na mwengine anaona kufanya hivyo ni kujilisha upepo

Kwahiyo wapo katka majadiriano na wala sio kwa huyo mpuuzi Makonda ambaye hajui hata anachokifanya.

Makonda sanasana ataikosti CCM maana hajui kutofautisha vyeo vya kiserikali na vyeo vya kichama na ndio maana anawakwaza sna wana ccm wanzake
 
CCM Ni moja na wana CCM Ni wamoja na tunasonga mbele kwa pamoja. Hakuna mgawanyiko wala migogoro ndani ya CCM na Ndani ya serikali yake.ndio maana shughuli za chama na serikali zinakwenda vizuri kabisa pasipo kukwama wala kusua sua.
 
Kwani teuzi ulifanyika bila ushirikishwaji wa wakuu hao wa idara?, maana nafasi hiyo ili kumpata anayefaa kikao hukaa ili kupima nani anafaa.
 
Inashangaza sana BASHITE kupewa Cheo utadhani Ccm haina watu makini wasio na Tuhuma

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
HAWAKUSINGIZIWA. UKIONA MTU HUYO AMEPEWA CHEO MAANA YAKE ALIKUWA SAHIHI. NA HAO WATU MBONA HAWAJAJIUZULU MPAKA SASA? SISI CHADEMA TULISEMA MAKONDA NDO ALIKUWA MUUAJI. LAKINI HAKUNA HATA KESI TULIENDA FUNGUA. MI NADHANI TUMUACHE AFANYE KAZI YAKE.
 
Nitashangaa sana wakijuzulu,kihekima kabisa walipaswa kukataa teuzi wakisema ni zamu ya vijana!!!!

Kupambana na madawa haukuwa mpango wa makonda Bali mfumo.na alifanikiwa.pakubwa sana!!

Check and Balance ni nzuri!!

Wajiuzulu waachiwe vijana hamna namna!!
 
Nilijua tu uchawa wako kwa Samia ni wa kutumwa...

Wanaokutuma ndio wanaommiliki bosi wako...

Eti unakumbuka ofisi ya masaki 2015!!!

Tatizo ccm mliingia kwa uchawa huku hamjui njia zake.
 
Yaani kidingii miaka 50+ unakuwa chawa wa the Bashite 🀭
 
Watu adui zako wanapata cheo. It's an every day thing. Kwa nini ujiuzulu?
Rais anapowapa wale watu vyei hakuulizi wewe maoni yako.
Hakuna ushahidi kwamba Makonda alimsingizia mtu yeyote. Makonda mwenyewe alisema alipoulizwa,mbona umeiacha hii kampeni dhidi ya madawa ya kulevya; Ah,bwana,wanasema niache,wanasema inaleta taharuki. "Huwezi hata kuamini ni nani wanaowafadhili hao watu"
Isipokuwa tu Makonda alipata matatizo mahakamani alipotaka kuwasaidia makahaba waliotelekezwa na watoto.
Nimemsikia dereva mmoja wa daladala(Musoma) anazungumza juzi.
Anasema,"Basi,bwana,wake wanawake wakaenda mahakamani kulalamika. Wakaitwa wazazi wa wale wanawake. Wakaulizwa mnawafahamu hawa jamaa wanaolalamikiwa? Wakasema hatujawaona hata siku moja. Basi,anasema,mahakama ikaamua,hayo mambo hayahusu mahakama,transactions za watu wanazofanya mitaani bila kuwashirikisha wazazi.
 
Naona mmeshindwa kuwatuliza Lissu na Mbowe wakae chungu kimoja mnaunga unga vistori vyenu

Makonda amewapelekea moto sana hizi week mpaka mmesahau operesheni changia mwenyekiti
Inaongelewa CCM, wewe umerukia CHADEMA. Kutoelewa kinachoongelewa ni ishara ya awali kabisa ya kukosa umakini. Na watu wa namna hii hata kwenye mitihani huambulia patupu. Unaulizwa kuhusu kilimo cha buni, wewe unaanza kuongelea mchezo wa mpira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…