Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.

28 October 2023
Pemba, Zanzibar
MATOKEO YA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA MTAMBWE PEMBA, ACT-WAZALENDO WAIBUKA KIDEDEA
View attachment 2795951
Picha: Dr. Mohamed Ali Suleiman wa ACT-Wazalendo akizungumza wakati wa kampeni.
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mtambwe Pemba Zanzibar , leo tarehe 28 oktoba 2023 amtangaza Dr. Mohamed Ali Suleiman mgombea wa ACT Wazalendo yaliyevuna kura 2449 kuwa mshindi huku mgombea Hamad Khamis wa CCM akiambulia kura 1531.
TOKA MAKTABA : MOTO WA UCHAGUZI
Historia ya jimbo la Mtambwe ambalo linatambulika ni jimbo mama waanzilishi wa siasa za uchaguzi wa vyama vingine, na ushindi utapeleka ujumbe Tanzania nzima na kote ulimwengu kuhusu ukubwa wa Mtambwe katika siasa za Zanzibar
View: https://m.youtube.com/watch?v=hkc5D3Q6XKY
11 October 2023
Habari za figisu na Matukio ya majaribio ya kumuengua mgombea wa ACT Wazalendo asiwe mgombea uchaguzi mdogo.
TUME YAKUBALI RUFAA YA UTENGUZI ACT WAZALENDO.
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imetengua uamuzi wa kumtengua Mgombea wa Chama cha ACT Wazalendo kwa nafasi ya Uwakilishi kwa Chama hicho ndugu. Mohammed Ali Suleiman katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Mtambwe.
![]()
Akitoa taarifa ya maamuzi ya rufaa kwa Vyombo vya Habari katika Afisi ndogo ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar iliyopo Chakechake kusini Pemba tarehe 10 Oktoba 2023, baada ya Chama cha ACT Wazalendo kukata rufaa kwa Tume hiyo, Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ndugu. Thabit Idarous Faina amesema,
“katika hatua za Uteuzi wa Wagombea Uchaguzi wa Jimbo la Mtambwe, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mtambwe alipokea pingamizi mbili (2) zilizowekwa na Wagombeawa CCM na ACT Wazalendo Uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi katika pingamizi hizo ulikuwa kama ifuatavyo,alimteuwa Mgombea wa CCM kwa kuamini kuwa ana sifa zote za kuteuliwa kisheria kuwa Mgombea na hakumteua mgombea wa ACT Wazalendo baada ya kujiridhisha kwamba hakutimiza sifa za kuteuliwa kwa mujibu masharti ya kifungu cha 51 (1) Sheria ya Uchaguzi Namba 4 ya mwaka 2018, Kufuatia uamuzi huo Mgombea wa ACT Wazalendo Ndg. Mohammed Ali Suleiman amekata Rufaa kwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa kufuata masharti ya kifungu Nam 52 (1) cha Sheria ya Uchaguzi Nam 4 ya mwaka 2018”
Akielezea uamuzi wa rufaa hiyo baada ya kuzijadili hoja za utenguzi kwa pande zote mbili Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Zanzibar alisema
“Kuhusu Rufaa ya kupinga Uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi kumtengua Mgombea wa CCM Ndg Hamad Khamis Hamad kuwa Mgombea kwa sababu ya kutokukamilisha Fomu ya Uteuzi katika Kiambatanisho cha Fomu ya wadhamini ambayo ilijenga hoja ya kuwa taarifa zake haziwezi kumtambua Mgombea chini ya kifungu cha 51 (1) (a) Tume imeamua kwamba Msimamiziwa Uchaguzi alishindwa kuzingatia Kanuni ya 13 (8) ya kanuni za Uchaguzi ya mwaka 2020 ambayo inamtaka msimamizi wa Uchaguzi kuhakikisha kwamba Fomu anayopokea iwe imejazwa kwa ukamilifu kwa kuwa Msimamizi alishindwa kuzingatia matakwa ya Kanuni hiyo, halikuwa kosa la Mgombea kwa hivyo Tume ya Uchaguzi imetupilia mbali Rufaa hiyo na kuthibitisha kuwa Ndg Hamad Khamis Hamad anazo sifa za kugombea katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Mtambwe”
Sambamba na hilo ameongeza kuwa kuhusu Rufaa ya kutoteuliwa kuwa Mgombea wa ACT Wazalendo Mohammed Ali Suleiman, kwa kutoa taarifa za uongo katika Fomu ya Uteuzi chini ya kifungu cha 51 (1) (b), Tume imebaini kuwa ushahidi uliowasilishwa kujenga hoja hiyo haukujitosheleza na hivyo imetengua uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi na kumteua Mohammed Ali Suleiman wa Chama cha ACT Wazalendo kuwa Mgombea wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Mtambwe kupitia Chama hicho
Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mtambwe unatarajia kufanyika tarehe 28 Oktoba mwaka huu ambapo vyama vinne vya Siasa ambavyo ni ACT Wazalendo, Chama cha Wananchi CUF, Chama cha Mapinduzi (CCM) na CHAUMMA vimeteuliwa kushiriki katika Uchaguzi huo. Source : https://www.zec.go.tz/index.php/habari/matukio/135-wasimamizi-wasaidizi-watakiwa-kusimamia-maadili
Kuna jimbo lina wapiga kura 320 tu, chezea znz weweHuko walikuwa wanafanya uchaguzi au maigizo ya uchaguzi?
Halafu inakuwaje mshindi wa jimbo anapata kura 2500 na kuwa mbunge wakati Tanganyika hizo ni kura za mshindi wa mwenyekiti wa kijii au mtaa?
Kweli hii nchi huliwa na wajanja huku wajinga wakilalamika badala ya kuchukua hatua.
Ndio gharama za muungano wa kulazimisha hizo.Kuna jimbo lina wapiga kura 320 tu, chezea znz wewe
Kwanini Zanzibar yote usiwe mkoa mmoja badala ya kuita cnhi.Kwenye uchaguzi wa ubunge majimbo mengi hizo ndo huwa total votes
Sidhani kama hata kodi wanayolipa inatosha kulipa mshahara wa Mbunge, watu 4000???Mkuu wew ulitaka apate kura ngapi ?
wee ni mzazibar?Huko walikuwa wanafanya uchaguzi au maigizo ya uchaguzi?
Halafu inakuwaje mshindi wa jimbo anapata kura 2500 na kuwa mbunge wakati Tanganyika hizo ni kura za mshindi wa mwenyekiti wa kijii au mtaa?
Kweli hii nchi huliwa na wajanja huku wajinga wakilalamika badala ya kuchukua hatua.
28 October 2023
Pemba, Zanzibar
MATOKEO YA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA MTAMBWE PEMBA, ACT-WAZALENDO WAIBUKA KIDEDEA
Picha: Dr. Mohamed Ali Suleiman wa ACT-Wazalendo akizungumza wakati wa kampeni.
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mtambwe Pemba Zanzibar , leo tarehe 28 oktoba 2023 amtangaza Dr. Mohamed Ali Suleiman mgombea wa ACT Wazalendo yaliyevuna kura 2449 kuwa mshindi huku mgombea Hamad Khamis wa CCM akiambulia kura 1531.
TOKA MAKTABA : MOTO WA UCHAGUZI
Historia ya jimbo la Mtambwe ambalo linatambulika ni jimbo mama waanzilishi wa siasa za uchaguzi wa vyama vingine, na ushindi utapeleka ujumbe Tanzania nzima na kote ulimwengu kuhusu ukubwa wa Mtambwe katika siasa za Zanzibar
View: https://m.youtube.com/watch?v=hkc5D3Q6XKY
11 October 2023
Habari za figisu na Matukio ya majaribio ya kumuengua mgombea wa ACT Wazalendo asiwe mgombea uchaguzi mdogo.
TUME YAKUBALI RUFAA YA UTENGUZI ACT WAZALENDO
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imetengua uamuzi wa kumtengua Mgombea wa Chama cha ACT Wazalendo kwa nafasi ya Uwakilishi kwa Chama hicho ndugu. Mohammed Ali Suleiman katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Mtambwe.
![]()
Akitoa taarifa ya maamuzi ya rufaa kwa Vyombo vya Habari katika Afisi ndogo ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar iliyopo Chakechake kusini Pemba tarehe 10 Oktoba 2023, baada ya Chama cha ACT Wazalendo kukata rufaa kwa Tume hiyo, Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ndugu. Thabit Idarous Faina amesema,
“katika hatua za Uteuzi wa Wagombea Uchaguzi wa Jimbo la Mtambwe, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mtambwe alipokea pingamizi mbili (2) zilizowekwa na Wagombeawa CCM na ACT Wazalendo Uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi katika pingamizi hizo ulikuwa kama ifuatavyo,alimteuwa Mgombea wa CCM kwa kuamini kuwa ana sifa zote za kuteuliwa kisheria kuwa Mgombea na hakumteua mgombea wa ACT Wazalendo baada ya kujiridhisha kwamba hakutimiza sifa za kuteuliwa kwa mujibu masharti ya kifungu cha 51 (1) Sheria ya Uchaguzi Namba 4 ya mwaka 2018, Kufuatia uamuzi huo Mgombea wa ACT Wazalendo Ndg. Mohammed Ali Suleiman amekata Rufaa kwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa kufuata masharti ya kifungu Nam 52 (1) cha Sheria ya Uchaguzi Nam 4 ya mwaka 2018”
Akielezea uamuzi wa rufaa hiyo baada ya kuzijadili hoja za utenguzi kwa pande zote mbili Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Zanzibar alisema
“Kuhusu Rufaa ya kupinga Uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi kumtengua Mgombea wa CCM Ndg Hamad Khamis Hamad kuwa Mgombea kwa sababu ya kutokukamilisha Fomu ya Uteuzi katika Kiambatanisho cha Fomu ya wadhamini ambayo ilijenga hoja ya kuwa taarifa zake haziwezi kumtambua Mgombea chini ya kifungu cha 51 (1) (a) Tume imeamua kwamba Msimamiziwa Uchaguzi alishindwa kuzingatia Kanuni ya 13 (8) ya kanuni za Uchaguzi ya mwaka 2020 ambayo inamtaka msimamizi wa Uchaguzi kuhakikisha kwamba Fomu anayopokea iwe imejazwa kwa ukamilifu kwa kuwa Msimamizi alishindwa kuzingatia matakwa ya Kanuni hiyo, halikuwa kosa la Mgombea kwa hivyo Tume ya Uchaguzi imetupilia mbali Rufaa hiyo na kuthibitisha kuwa Ndg Hamad Khamis Hamad anazo sifa za kugombea katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Mtambwe”
Sambamba na hilo ameongeza kuwa kuhusu Rufaa ya kutoteuliwa kuwa Mgombea wa ACT Wazalendo Mohammed Ali Suleiman, kwa kutoa taarifa za uongo katika Fomu ya Uteuzi chini ya kifungu cha 51 (1) (b), Tume imebaini kuwa ushahidi uliowasilishwa kujenga hoja hiyo haukujitosheleza na hivyo imetengua uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi na kumteua Mohammed Ali Suleiman wa Chama cha ACT Wazalendo kuwa Mgombea wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Mtambwe kupitia Chama hicho
Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mtambwe unatarajia kufanyika tarehe 28 Oktoba mwaka huu ambapo vyama vinne vya Siasa ambavyo ni ACT Wazalendo, Chama cha Wananchi CUF, Chama cha Mapinduzi (CCM) na CHAUMMA vimeteuliwa kushiriki katika Uchaguzi huo. Source : https://www.zec.go.tz/index.php/habari/matukio/135-wasimamizi-wasaidizi-watakiwa-kusimamia-maadili
Ndokashinda sasa nahao ndiowapiga kura kunanchi ukishinda kura zajumla bado wewe sio mshindi ilajamaa akishinda kura za viongozi ambao niwachache kuliko wananchi anakuwa kiongozi huwa tunaelezwa ndio baba democrasiaHuko walikuwa wanafanya uchaguzi au maigizo ya uchaguzi?