Pre GE2025 CCM waanza kuzalisha bidhaa zinazomnadi Rais Samia kuelekea uchaguzi mkuu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ni hatari sana kuwa na Taifa lenye matangazo mengi ya kumtangaza mtu kuliko kutangaza utalii wa nchi husika!!
 
Hawajatengeneza t.paper zenye picha ya mama? Tunazihitaji sana hizo.
 
Ukiona hivyo ujue chama kimegeuka genge la walaji wanaojua fika kuwa hawaungwi mkono tena na wananchi. Ni hatari!
 

Chema chajiuza na kibaya chajitembeza!
 
Ni kwa sababu tu pumzi ya mwenyezi Mungu , vinginevyo nayo wangeweza iwekea kiperushi cha SSH
 
Duh
Kweli kua uyaone, mtu hai anasifiwa zaidi ya MAREHEMU kisa tu amepata Unyerere..hatari
 
Huyu dikteta wa kwanza mwanamke ana uchu wa kutisha wa madaraka, naamini kubwa hata akirudi madarakani hatakapiza miaka mitano madarakani. Utunze hii kwa ajili ya baadaye
 

Pesa za Wajomba hizo. Hakuna kinachouzwa hapo..... Yaani wagawe Bodaboda, Kinga. Vitenge na Tshirt bure halafu wakuuzie opener?
 
Bado hujasema, hadi useme😂
Niseme nini mbwembwe zote zile hadi leo mna milioni 64 za tone tone na huyo mzee tumbotumbo kaenda kuzitumbua Uganda? Nitasema nini mbele ya lile tumbo kubwa la Lissu na ule ulafi? Halafu mwambieni apunguze jazba mambo bado!
 
Kungekuwa na kampeni ya leta kanga, pesa, redio, viatu na mazaga yote ya mama tuvune ila KURA kwa CDM.
 
Wanafanya upuuzi huo wote halafu baadaye wanaiba na uchaguzi.Akili za Kima kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…