King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 56,205
- 79,515
Mbona na yeye Bollen Ngetti kipindi cha Magu aliufyata?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama ni Mnafiki asipewe nafasi kusikilizwa.
Hatujui safari hii anakuja na mbinu ipi.
Ukishajipaka mavi tusitukaribie hata kama una Mkate. Umenajisikaaa
Hadi UOGE. kwanza Atubu kama ni mnafiki kweli. Ndio aje acheze na sisi
Sasa Uber inatumia mfumo wa kidijitali ungeonyesha details zote phone number ya travel requester pick up and dropping off locations car reg number timelines etc hence very easy to traceKwa hili nimeamini! Aliitwa usiku kwa masharti ya kupanda "Uber" na sio gari take! Ina maana angeenda peke take bila hata walinzi wake wala dereva wake.
Kingetokea nini usiku huo?? Duh Mungu anaipenda Tanzania sana
Membe Pamoja na Kwamba simkubali alimalizwa NGUVU pale Msasani Na hata dada mbeba makabrasha yake alizuiwa Mara kadhaa kumpelekea BAADHI ya NyarakaHapa Ngetti anataka kusema kuwa Mwendazake kwa kushirikiana na Uncle Tony walimtaka kum-suicide Mzee Member?
Aje usiku na "uber"! Ngeti akahojiwe na Polisi atakua anajua mengi
Kuna mtu alipigwa risasi 36 mchana kweupee na cctv camera zikaondolewa kuficha assassinsSasa Uber inatumia mfumo wa kidijitali ungeonyesha details zote phone number ya travel requester pick up and dropping off locations car reg number timelines etc hence very easy to trace
Jasusi mbobezi akapiga mbizi ya uhakika.Kwa mwendo huu, watatajana tu! Maana hapo anasema Membe alisubiriwa aingie kwenye 18 zao tu hahaahahah
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]Hapa Ngetti anataka kusema kuwa Mwendazake kwa kushirikiana na Uncle Tony walimtaka kum-suicide Mzee Member?
Aje usiku na "uber"! Ngeti akahojiwe na Polisi atakua anajua mengi
Hata mimi naanza kuliona hiliNimeona Boren Ngeti naye katapika Siri zote za Jiwe, Diallo, Membe.
Safi, tunakaribia, watamtaja aliyempiga risasi Lisu na kwa maagizo ya Nani. Hata Azory na Ben Saanane wanaweza kupata waliowaua/waliowapoteza au wako wapi
Teuzi za kimalaya malaya mlizozoea enzi za yule dhalim mwendazake awamu hii hazipoDK. ANTONY DIALO NI MNAFIKI SANA, MPUUZENI
Na Bollen Ngetti
NINAANDIKA makala haya nikiendelea na matibabu ya Covid-19 kwa siku ya 9 lakini nina amini nitapona. Upekee wa virusi hivi ni kwamba vinaathiri mfumo wa upumuaji lakini si nishati ya ubongo. Kwa mantiki hiyo nina akili safi ninapoandika juu ya unafiki na woga wa Diallo.
Niharakishe kusema kwamba "Uncle Tony" ni baba yangu kiumri. Ni rafiki yangu wa karibu. Kwa mara ya kwanza nilimfahamu 2015 baada ya kutambulishwa kwake na Bernard Membe wakati wa mchakato wa kumpata mgombea Urais ndani ya CCM.
Dk. Diallo alipewa fedha nyingi na Membe ili kushawishi wajumbe wa Kanda ya Ziwa wa Mkutano Mkuu kuja kumpitisha Membe. Mara nyingi tulifanya vikao nyumbani kwake Dodoma. Lakini binafsi tulikutana mara kadhaa kuweka mambo sawa kwa mgombea wetu. Hii ni kuonesha kuwa ninamfahamu vizuri Dk. Diallo ambaye hata hivyo PhD yake ina utata sawa na uraia wake.
Uncle Tony ni mtu wa maslahi zaidi kuliko utumishi kwa umma. Nimesikiliza mahojiano yake kupitia television yake ya Star. Baadaye akafanya maigizo ya kurekebisha aliyoita "makosa" lakini wanasaikolojia tunaamini sentensi au maelezo ya kwanza ndio yaliyo na ukweli.
Diallo anasema tuliwachagua watu wenye rekodi ya kutibiwa Mirembe kuchukua nchi hivyo tuwe makini tuendako. Wakati huo huo akiponda utawala wa awamu ya 5 ya Magufuli. Nani alichukua nchi kama si Magufuli? Waziri Mkuu anachukua nchi? Makamu wa Rais au baraza la Mawaziri wanachukua nchi? Sisi si watoto wa chekechea! Hakuna alitafsiri vibaya lakini kauli ilimnyooshea kidole Marehemu Magufuli.
Sasa, hoja yangu ni hii! Kwa nini alimfanyia kampeni kichaa ilhali akijua? Pili, Tony atoa mkataba aliyoingia na CCM kwamba Magufuli akishinda "atapoozwa" kwa malipo kwa kazi ya kampeni kupitia Star Tv. Kama hana akaye kimya aache unafiki.
Tatu, kwa nini kipindi hicho cha Mwendazake hakujitokeza iwe sirini au hadharani kukosoa hali ya mambo ndani ya chama na Serikali? Kwa nini alikaa kimya huku ni kiongozi tena wa Mkoa? Mbona wengine (nikiwemo) tulikosoa chama chetu hadharani bila kuogopa kutekwa, kuteswa na hata jela?
Nikukumbushe wewe Dk. Diallo unakumbuka ni wewe ulinipigia simu ukiniambia niache kumkosoa Magufuli maana una taarifa Vetting yangu imekamilika na soon nitateuliwa U-DC? Hii si kwamba ulimkubali Magufuli ambaye leo unamwita kichaa? Ieleweke simtetei Marehemu isipokuwa napinga unafiki wa Uncle Tony anayejua kwamba linapokuja suala la kusema ukweli hata malaika nitamwambia. Nitausema.
Nikukumbushe tena Dialo, unakumbuka 2017 siku ulipoitwa Ikulu ya Magogoni na JPM saa nne asubuhi ukapewa maelekezo ya namna ya kummaliza kisiasa Bernard Membe? Unakumbuka ilipofika saa 11 jioni ulimpigia simu Membe na kumuomba muonane nyumbani kwako giza likiingia? Unakumbuka Membe alikukatalia baada ya kuwa na taarifa kuwa ulishinda Magogoni na Mwendazake? Ukamsihi sana aje saa tano usiku kwa "Uber" na si gari lake? Hivi unajua mchezo wote tuliufahamu kwamba Membe angekuja kingetokea nini?
Hivi unajua kwa kushindwa kwako kummaliza kisiasa Membe ndicho kilichokugombanisha na Ngosha na kukuona huna maana? Hivi unakumbuka ulivyomtimua kazi Mtangazaji Yusuf Kamote na kumnyima stahiki zake kisa tu ni rafiki wa Membe kwa maagizo kutoka mawinguni?
Leo unalia lia na kuuficha ukweli uliokodoa macho hadharani. Huu ni unafiki na woga usio na maana kwa umri wako. Umesema utagombea tena uenyekiti mwakani. Nitashangaa sana kama wana CCM makini wa Mwanza watakurejesha madarakani mtu wa aina yako sawa na ninavyoshangaa Uhamiaji kukukalia kimya kuhusu uraia wako.
Ushauri wangu kwako baba yangu, rafiki yangu kaa kimya. Usijipendekeze kwa Rais Samia Suluhu Hassan ili usogelee meza ndefu ya chakula. Tulia ulelee wajukuu hizi sio enzi za unafiki tena. Ahsante kwa leo!
Maoni: 0683 226539
#MguseMamaNinuke
Muungwana akivuliwa nguo huchutama.Exactly. Huyu naye bomu tu sasa aliyoyaandika yanatuhusu nini
Dialo ni imsukuma toka kijiji cha Seke jina lake halisi alikuwa naitwa Antony Ng'wandu sielewi jina la Dialo alilipachika toka wapiDiallo si jina la west Africa jamii ya mandinga
Hii nchi ina 'umafia' .Uje usiku wa kiza kinene lakini pia uje na Uber.
Kuuumbeh
Dialo alikuwa mnafiki kwakuwa JPM alikuwa hachelewi kukupoteza mazima.DK. ANTONY DIALO NI MNAFIKI SANA, MPUUZENI
Na Bollen Ngetti
NINAANDIKA makala haya nikiendelea na matibabu ya Covid-19 kwa siku ya 9 lakini nina amini nitapona. Upekee wa virusi hivi ni kwamba vinaathiri mfumo wa upumuaji lakini si nishati ya ubongo. Kwa mantiki hiyo nina akili safi ninapoandika juu ya unafiki na woga wa Diallo.
Niharakishe kusema kwamba "Uncle Tony" ni baba yangu kiumri. Ni rafiki yangu wa karibu. Kwa mara ya kwanza nilimfahamu 2015 baada ya kutambulishwa kwake na Bernard Membe wakati wa mchakato wa kumpata mgombea Urais ndani ya CCM.
Dk. Diallo alipewa fedha nyingi na Membe ili kushawishi wajumbe wa Kanda ya Ziwa wa Mkutano Mkuu kuja kumpitisha Membe. Mara nyingi tulifanya vikao nyumbani kwake Dodoma. Lakini binafsi tulikutana mara kadhaa kuweka mambo sawa kwa mgombea wetu. Hii ni kuonesha kuwa ninamfahamu vizuri Dk. Diallo ambaye hata hivyo PhD yake ina utata sawa na uraia wake.
Uncle Tony ni mtu wa maslahi zaidi kuliko utumishi kwa umma. Nimesikiliza mahojiano yake kupitia television yake ya Star. Baadaye akafanya maigizo ya kurekebisha aliyoita "makosa" lakini wanasaikolojia tunaamini sentensi au maelezo ya kwanza ndio yaliyo na ukweli.
Diallo anasema tuliwachagua watu wenye rekodi ya kutibiwa Mirembe kuchukua nchi hivyo tuwe makini tuendako. Wakati huo huo akiponda utawala wa awamu ya 5 ya Magufuli. Nani alichukua nchi kama si Magufuli? Waziri Mkuu anachukua nchi? Makamu wa Rais au baraza la Mawaziri wanachukua nchi? Sisi si watoto wa chekechea! Hakuna alitafsiri vibaya lakini kauli ilimnyooshea kidole Marehemu Magufuli.
Sasa, hoja yangu ni hii! Kwa nini alimfanyia kampeni kichaa ilhali akijua? Pili, Tony atoa mkataba aliyoingia na CCM kwamba Magufuli akishinda "atapoozwa" kwa malipo kwa kazi ya kampeni kupitia Star Tv. Kama hana akaye kimya aache unafiki.
Tatu, kwa nini kipindi hicho cha Mwendazake hakujitokeza iwe sirini au hadharani kukosoa hali ya mambo ndani ya chama na Serikali? Kwa nini alikaa kimya huku ni kiongozi tena wa Mkoa? Mbona wengine (nikiwemo) tulikosoa chama chetu hadharani bila kuogopa kutekwa, kuteswa na hata jela?
Nikukumbushe wewe Dk. Diallo unakumbuka ni wewe ulinipigia simu ukiniambia niache kumkosoa Magufuli maana una taarifa Vetting yangu imekamilika na soon nitateuliwa U-DC? Hii si kwamba ulimkubali Magufuli ambaye leo unamwita kichaa? Ieleweke simtetei Marehemu isipokuwa napinga unafiki wa Uncle Tony anayejua kwamba linapokuja suala la kusema ukweli hata malaika nitamwambia. Nitausema.
Nikukumbushe tena Dialo, unakumbuka 2017 siku ulipoitwa Ikulu ya Magogoni na JPM saa nne asubuhi ukapewa maelekezo ya namna ya kummaliza kisiasa Bernard Membe? Unakumbuka ilipofika saa 11 jioni ulimpigia simu Membe na kumuomba muonane nyumbani kwako giza likiingia? Unakumbuka Membe alikukatalia baada ya kuwa na taarifa kuwa ulishinda Magogoni na Mwendazake? Ukamsihi sana aje saa tano usiku kwa "Uber" na si gari lake? Hivi unajua mchezo wote tuliufahamu kwamba Membe angekuja kingetokea nini?
Hivi unajua kwa kushindwa kwako kummaliza kisiasa Membe ndicho kilichokugombanisha na Ngosha na kukuona huna maana? Hivi unakumbuka ulivyomtimua kazi Mtangazaji Yusuf Kamote na kumnyima stahiki zake kisa tu ni rafiki wa Membe kwa maagizo kutoka mawinguni?
Leo unalia lia na kuuficha ukweli uliokodoa macho hadharani. Huu ni unafiki na woga usio na maana kwa umri wako. Umesema utagombea tena uenyekiti mwakani. Nitashangaa sana kama wana CCM makini wa Mwanza watakurejesha madarakani mtu wa aina yako sawa na ninavyoshangaa Uhamiaji kukukalia kimya kuhusu uraia wako.
Ushauri wangu kwako baba yangu, rafiki yangu kaa kimya. Usijipendekeze kwa Rais Samia Suluhu Hassan ili usogelee meza ndefu ya chakula. Tulia ulelee wajukuu hizi sio enzi za unafiki tena. Ahsante kwa leo!
Maoni: 0683 226539
#MguseMamaNinuke
Huo ndio UKWELI...lakin haisaidiiCcm hapa wamediverge ishu ya katiba mpya