CCM waendelea kuvuana nguo, safari hii ni Bollen Ngeti

CCM waendelea kuvuana nguo, safari hii ni Bollen Ngeti

Tumewashika pabaya

IMG_20210714_123138.jpg
 
Tunachokosea ni kuangalia tabia ya mtu baada ya kuangalia alichokiongea ni kweli au ni uongo?

Tujifunze kuwa na vifua wakina Bush Marekani waliipa hasara sana za vita lakini hawakuacha kumkosoa Trump alivyokuwa madarakani na sasa yupo nje ya offisi.

All in all Diallo inawezekana ana makandokando lakini hoja yake ipo wazi kabisa inatakiwa kujibiwa kwa hoja zenye mashiko sio kumshambulia!!

Mtu kaongelea taasisi ya urais wewe unaleta mambo ya kuwa yeye sio Raia wa Tanzania? Nani wa kulaumiwa kama sio ccm ambayo ilimfanya kuwa mbunge waziri na mwenyekiti wa chama?

Magufuli mwenyewe uraia wake ulikuwa na utata halafu mkampa urais!! Shame.

Tujifunze kushindana na hoja ya mtu sio mambo yake binafsi au maisha yake nje ya alichokiongea

Haya yalitakiwa kuongelewa kabla ya Diallo ajaongea

Nasubiri mmtukane na mzee warioba aliyesema anataka katiba mpya.
Sidhani hapa kama kinachoongelewa ni tabia ya mtu bali kinachoongelewa ni unafiki wa mtu ambaye ndiye chanzo na msaada wa kuingia madarakani mtu ambaye leo tunaaminishwa alikuwa na cheti cha Milembe. Diallo kwa kauli yake anakili alishiriki Kampeni za Uchaguzi kupitia TV yake. Wafanyakazi wake walikuwa wakilipwa na CCM kwa kazi hiyo. Mwenyewe na kampuni wakiahidiwa kitita mambo yakikaa sawa. Leo unakuja kulalamika kuingia kwa kiongozi mwenye cheti cha Milembe?

Diallo ni Mjumbe wa Kamati kuu kwa nafasi yake. Ndani ya chama kuna taratibu za kuwasilisha malalamiko hata ushauri na mawazo ya mtu kama yeye katika vikao. Mwaka wa saba sasa anaingia na kutoka kwenye vikao vya Chama akiwa bubu. leo anatokea kwenye chombo chake cha habari na kutoa shutuma nzito kiasi hiki. Haiendani kabisa na miongozo na maadili ya chama chake. Hayo ya wanachama/viongozi kuropoka, CCM hawakuyazoea ni mambo ya upinzani ambapo kila mtu ni msemaji wa Chama.
 
Dialo ni imsukuma toka kijiji cha Seke jina lake halisi alikuwa naitwa Antony Ng'wandu sielewi jina la Dialo alilipachika toka wapi
ila si mtu mnyoofu fedha na utajiri wake inasadikiwa ni mchongo ulihusisha baadhi madeni ya vita vya Kagera ambayo yalisamahewa ila watu wakacheza dili na serikali kuwalipa wao
Asante kwa maelezo mkuu
 
Mimi kuhusu hayo mambo yake ya siasa na kufukuza wafanyakazi wake kazi,sina uelewa wa ndani lakini kuhusu uraia wake,na ohd yake nina uhakika wake 100 kwa 100,nakuomba umfuatilie kwenye vile vyuo alivyosoma utapewa facts kuwa kusoma kasoma

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Ni raia wa wapi?

Mnaficha nini kusema uraia wake mkuu
 
Kwenye uraia wa ANTONY NG'WANDU DIALLO Bollen Ngeti anapotosha,au makusudi au kwa kutoujua ukweli.

Uncle Tony ni msukuma original wa Ntunzu. Kwa sababu hiyo uraia wake hauna utata wowote. Ni mtanzania kabisa.
Kumbe NG'WANDU sasa hili jina la AFRIKA MAGHARIBI kalitoa wapi huyu NG'WANDU

Ila kama ameweza kuiba jina basi suala la utajiri wake kuwa una ukakasi linawezekana.
 
DK. ANTONY DIALO NI MNAFIKI SANA, MPUUZENI

Na Bollen Ngetti

NINAANDIKA makala haya nikiendelea na matibabu ya Covid-19 kwa siku ya 9 lakini nina amini nitapona. Upekee wa virusi hivi ni kwamba vinaathiri mfumo wa upumuaji lakini si nishati ya ubongo. Kwa mantiki hiyo nina akili safi ninapoandika juu ya unafiki na woga wa Diallo.

Niharakishe kusema kwamba "Uncle Tony" ni baba yangu kiumri. Ni rafiki yangu wa karibu. Kwa mara ya kwanza nilimfahamu 2015 baada ya kutambulishwa kwake na Bernard Membe wakati wa mchakato wa kumpata mgombea Urais ndani ya CCM.

Dk. Diallo alipewa fedha nyingi na Membe ili kushawishi wajumbe wa Kanda ya Ziwa wa Mkutano Mkuu kuja kumpitisha Membe. Mara nyingi tulifanya vikao nyumbani kwake Dodoma. Lakini binafsi tulikutana mara kadhaa kuweka mambo sawa kwa mgombea wetu. Hii ni kuonesha kuwa ninamfahamu vizuri Dk. Diallo ambaye hata hivyo PhD yake ina utata sawa na uraia wake.

Uncle Tony ni mtu wa maslahi zaidi kuliko utumishi kwa umma. Nimesikiliza mahojiano yake kupitia television yake ya Star. Baadaye akafanya maigizo ya kurekebisha aliyoita "makosa" lakini wanasaikolojia tunaamini sentensi au maelezo ya kwanza ndio yaliyo na ukweli.

Diallo anasema tuliwachagua watu wenye rekodi ya kutibiwa Mirembe kuchukua nchi hivyo tuwe makini tuendako. Wakati huo huo akiponda utawala wa awamu ya 5 ya Magufuli. Nani alichukua nchi kama si Magufuli? Waziri Mkuu anachukua nchi? Makamu wa Rais au baraza la Mawaziri wanachukua nchi? Sisi si watoto wa chekechea! Hakuna alitafsiri vibaya lakini kauli ilimnyooshea kidole Marehemu Magufuli.

Sasa, hoja yangu ni hii! Kwa nini alimfanyia kampeni kichaa ilhali akijua? Pili, Tony atoa mkataba aliyoingia na CCM kwamba Magufuli akishinda "atapoozwa" kwa malipo kwa kazi ya kampeni kupitia Star Tv. Kama hana akaye kimya aache unafiki.

Tatu, kwa nini kipindi hicho cha Mwendazake hakujitokeza iwe sirini au hadharani kukosoa hali ya mambo ndani ya chama na Serikali? Kwa nini alikaa kimya huku ni kiongozi tena wa Mkoa? Mbona wengine (nikiwemo) tulikosoa chama chetu hadharani bila kuogopa kutekwa, kuteswa na hata jela?

Nikukumbushe wewe Dk. Diallo unakumbuka ni wewe ulinipigia simu ukiniambia niache kumkosoa Magufuli maana una taarifa Vetting yangu imekamilika na soon nitateuliwa U-DC? Hii si kwamba ulimkubali Magufuli ambaye leo unamwita kichaa? Ieleweke simtetei Marehemu isipokuwa napinga unafiki wa Uncle Tony anayejua kwamba linapokuja suala la kusema ukweli hata malaika nitamwambia. Nitausema.

Nikukumbushe tena Dialo, unakumbuka 2017 siku ulipoitwa Ikulu ya Magogoni na JPM saa nne asubuhi ukapewa maelekezo ya namna ya kummaliza kisiasa Bernard Membe? Unakumbuka ilipofika saa 11 jioni ulimpigia simu Membe na kumuomba muonane nyumbani kwako giza likiingia? Unakumbuka Membe alikukatalia baada ya kuwa na taarifa kuwa ulishinda Magogoni na Mwendazake? Ukamsihi sana aje saa tano usiku kwa "Uber" na si gari lake? Hivi unajua mchezo wote tuliufahamu kwamba Membe angekuja kingetokea nini?

Hivi unajua kwa kushindwa kwako kummaliza kisiasa Membe ndicho kilichokugombanisha na Ngosha na kukuona huna maana? Hivi unakumbuka ulivyomtimua kazi Mtangazaji Yusuf Kamote na kumnyima stahiki zake kisa tu ni rafiki wa Membe kwa maagizo kutoka mawinguni?

Leo unalia lia na kuuficha ukweli uliokodoa macho hadharani. Huu ni unafiki na woga usio na maana kwa umri wako. Umesema utagombea tena uenyekiti mwakani. Nitashangaa sana kama wana CCM makini wa Mwanza watakurejesha madarakani mtu wa aina yako sawa na ninavyoshangaa Uhamiaji kukukalia kimya kuhusu uraia wako.

Ushauri wangu kwako baba yangu, rafiki yangu kaa kimya. Usijipendekeze kwa Rais Samia Suluhu Hassan ili usogelee meza ndefu ya chakula. Tulia ulelee wajukuu hizi sio enzi za unafiki tena. Ahsante kwa leo!
Maoni: 0683 226539
#MguseMamaNinuke
Ishu ya msingi hapa ni ule ukweli kwamba jamaa alikuwa mwehu, na yeye mwenyewe aliwahi kusema hivyo. Hayo mambo yenu mengine mpigiane simu msutane
 
Naona akapimwe mirembe tuone kinachomsibu. Unasubiri mtu afariki ndio umshambulie!
 
Tunachokosea ni kuangalia tabia ya mtu baada ya kuangalia alichokiongea ni kweli au ni uongo?

Tujifunze kuwa na vifua wakina Bush Marekani waliipa hasara sana za vita lakini hawakuacha kumkosoa Trump alivyokuwa madarakani na sasa yupo nje ya offisi.

All in all Diallo inawezekana ana makandokando lakini hoja yake ipo wazi kabisa inatakiwa kujibiwa kwa hoja zenye mashiko sio kumshambulia!!

Mtu kaongelea taasisi ya urais wewe unaleta mambo ya kuwa yeye sio Raia wa Tanzania? Nani wa kulaumiwa kama sio ccm ambayo ilimfanya kuwa mbunge waziri na mwenyekiti wa chama?

Magufuli mwenyewe uraia wake ulikuwa na utata halafu mkampa urais!! Shame.

Tujifunze kushindana na hoja ya mtu sio mambo yake binafsi au maisha yake nje ya alichokiongea

Haya yalitakiwa kuongelewa kabla ya Diallo ajaongea

Nasubiri mmtukane na mzee warioba aliyesema anataka katiba mpya.
Tatizo la wanaCCm wengi hawana uwezo wa kujibu hoja. Kwa hiyo wanakimbilia personal issues.
 
Ungeugua covid19 wakati wa Magufuli hata kusema unaugua covid usingesema ili kumfurahisaha.
 
Hawawezi kumuua kirahisi hivyo jasusi mbobezi.. Mzee wa " niguse ninuke"
CCM Wana mbinu za kishamba sana.
Unamuambia mtu aje usiku wa kiza kinene Tena asije na gari lake, utafikiri anamuamrisha mke wa mtu anaetaka kuzini nae.
Damu ya mtu sio kitu Cha mchezo, unaona Sasa wanayaanika hadharani. Na bado.
Kuna atakayesema walivyopanga kumuua Lissu na hata walikompeleka Saanane.
 
Kwenye uraia wa ANTONY NG'WANDU DIALLO Bollen Ngeti anapotosha,au makusudi au kwa kutoujua ukweli.

Uncle Tony ni msukuma original wa Ntunzu. Kwa sababu hiyo uraia wake hauna utata wowote. Ni mtanzania kabisa.
Je,Luna mnyantuzu mwenye Nina DIALLO? Labda tuanzie hapo.
 
Computer servers za Uber ziko overseas utadelete vip tracking records
Kwani nani angejua kuwa katumia Uber? Ukumbuke Huyo Huyo anayetegemewa kufanya uchunguzi ndio Huyo Huyo anayeseti mambo! Just a simple Logic. Kuna jambo ningeliweka kama mfano ila wacha nikae kimya
 
Tunachokosea ni kuangalia tabia ya mtu baada ya kuangalia alichokiongea ni kweli au ni uongo?

Tujifunze kuwa na vifua wakina Bush Marekani waliipa hasara sana za vita lakini hawakuacha kumkosoa Trump alivyokuwa madarakani na sasa yupo nje ya offisi.

All in all Diallo inawezekana ana makandokando lakini hoja yake ipo wazi kabisa inatakiwa kujibiwa kwa hoja zenye mashiko sio kumshambulia!!

Mtu kaongelea taasisi ya urais wewe unaleta mambo ya kuwa yeye sio Raia wa Tanzania? Nani wa kulaumiwa kama sio ccm ambayo ilimfanya kuwa mbunge waziri na mwenyekiti wa chama?

Magufuli mwenyewe uraia wake ulikuwa na utata halafu mkampa urais!! Shame.

Tujifunze kushindana na hoja ya mtu sio mambo yake binafsi au maisha yake nje ya alichokiongea

Haya yalitakiwa kuongelewa kabla ya Diallo ajaongea

Nasubiri mmtukane na mzee warioba aliyesema anataka katiba mpya.
Bollen Ngetti Ni walewale Sema Nini Watanzania Siyo watu was Kumbukumbu pia siyo wasomaji.. mhariri wa Sauti Huru Miaka Hiyo
 
Mwingine ajitokeze kumjibu Boleni panoge zaidi.
 
Back
Top Bottom