CCM "wakiharibu" wimbo wa Taifa: Jicho la Mutungi lina makengeza?

Sijui kwanini chadema huwa inafanya mambo yake kihuni namna hii
 
Hao vijana walikuwa wanaimba ndani ya tukio rasmi la shughuli za kichama kwa mujibu wa katiba yao?

Je, tulikemea jambo hili wakati huo? Au tuliacha ili nasi tuje kulipa kisasi kwa kurudia kosa?

Kama ni kulipiza, kwa hivyo huu ndio muelekeo wa serikali itakayoundwa ya visasi?

Visasi vitaliponya taifa na mgawanyiko unaolalamikiwa kuongezeka awamu hii?

Ushabiki na mahaba yakituisha kama pombe itokavyo kichwani kwa mlevi tutaanza kuona wapi tulisukumwa na upepo wa kishabiki na kiharakati.

Kuna siku watu watakuja kuamka na kutambua 'Alter Ego' wa shujaa wao ana tabia gani hasi ambazo hawazioni sasa, kwani yeye alipaswa awe wa kwanza kuwakumbusha watu ubaya wa jambo hili walilofanya wanachama.

Yeye ndiye anaenda kukabidhiwa kulinda tunu za taifa, kulinda sheria na katiba, kulinda tamaduni, desturi na maadili ya taifa letu.
 
Chadema inaonyesha inatafuta kwa udi na uvumba mchafuano na dola ili dola iwashugulikie na watumie hiyo kama mtaji wa kuthibitisha wanaonewa. (Lissu's idea)

Hata Mbowe anasema wanafanya siasa kwa maumivu makubwa lakini hawasemi sheria wanazo vunja kila kukicha.
 
Sijui kwanini chadema huwa inafanya mambo yake kihuni namna hii
Hakuna offence hapo msilete chuki zenu. Mara ngapi wimbo huo unaimbwa na kuongezewa maneno mengine? Mara ngapi unaboreshwa melody yake? Afrika Kusini na Zimbabwe wanatumia melody hiyo hiyo ya wimbo maneno ubeti wa kwanza sawa kwa asilimia kubwa lkn beti zonazofuata wanaongeza ya kwao. Wanavunja sheria yetu?
 
Suala ni kubadiri wimbo wa taifa au kuimba tofauti kwenye shughuli na tukio????

Kweli CCM mnatapatapa sana mwaka huu.
 
Hakuna ubaya kutumia melody ya wimbo wa taifa kuimba jambo zuri ulipendalo. Bongo fleva kuna mmoja aliweka kipande cha wimbo wa taifa, alivunja sheria? Mmekosa hoja
 
Mkuu utaelewa in due time.
Siyo kila mtu ataelewa sasa au ataelewa hapo baadaye hiki tunachoona hakipo sawa.
 
Thank you so much Mkuu for sharing this clip. 🙏🏽

 
Anga linazidi kuwakataa chama tawala, upepo unaenda kwa kasi wasiyoitarajia.

Mimi nasema hivi, Lissu akiwakosa 2020, 2025 anakaa IKULU.

Ikiwezekana awe Mwenyekiti wa Chama kabisa.
Lissu anaingia ikulu mwaka huu 2020. Amini nakwambia
 
Itakua hakuona hiii.......

Kesho ni lazima atatoa kalipio kali na azima ya kuifuta ccm...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…