CCM "wakiharibu" wimbo wa Taifa: Jicho la Mutungi lina makengeza?

Anga linazidi kuwakataa chama tawala, upepo unaenda kwa kasi wasiyoitarajia.

Mimi nasema hivi, Lissu akiwakosa 2020, 2025 anakaa IKULU.

Ikiwezekana awe Mwenyekiti wa Chama kabisa.
Hapana its now or never..!!!
 
Ikiundwa serikali ya visasi kutakuwa na Jambo jipya hapo? Tusaidie kuelewa manji Yuko wapi au jengo la Tenesco ubungo liko wapo Kama hatuna serikali ya visasi?
 
Ukisoma huyu muhuni alivyo andika ndio utajua fika chadema kamwe hawagusi ikulu ...angalia anavyo andika! Hivi kosa lq chadema ndio sio kosa kwa sababu lilishafanywa na wanao jiita CCM?
Hivi mwenye hati miliki ya wimbo wa taifa ni Nani?je ni serikali,je ni mtu aliyeutungs?je ni watanzania,je ni Serikali au CCM? Na nikitaka kuunakili au kufanya remix naomba kibari kwa Nani?
 
Hivi mwenye hati miliki ya wimbo wa taifa ni Nani?je ni serikali,je ni mtu aliyeutungs?je ni watanzania,je ni Serikali au CCM? Na nikitaka kuunakili au kufanya remix naomba kibari kwa Nani?
Wakikujibu hili swali nitag. Mtu akibadiri wimbo wa Taifa amevunja kifungu gani cha sheria???
 
Jaji Mutungi inaelekea haijui asili ya wimbo huu tunaouita wa taifa, kwa watu wa nchi za kusini mwa Tanzania tyuni ya wimbo huu huimbwa makanisani na Afrika Kusini wao wameitumia kwa nchi yao. Tanzania hawezi kumzuia mtu yoyote kutumia tyuni ya huu wimbo kwani nasi tuliiga, hatua zozote anazochukuliwa mtu kwa kutumia tyuni ya wimbo wa kanisa na kusema kuwa ni wake ni kujimilikisha kitu ambacho wewe haujakitunga.
 
Mutungi ameropoka. Amejiaibisha. Kwa mantiki hiyo, basi pia Tanzania imeunajisi wimbo wa Taifa wa South Africa.
Afrika Kusini nao wametumia tyuni ya wimbo wa kikristu ambao huimbwa kwenye makanisa yao.
 
Kinachoongelewa ni kwanini Jaji hakuwaonya hawa wa kwanza, hawa wa pili wasingefanya kosa hilo tusingemsikia Jaji.
 
Mutungi ni kimeo 🤣
 
Mutungi ni kimeo 🤣
 
Ikiundwa serikali ya visasi kutakuwa na Jambo jipya hapo? Tusaidie kuelewa manji Yuko wapi au jengo la Tenesco ubungo liko wapo Kama hatuna serikali ya visasi?
Ikiwa CDM wanataka nchi ili waendelee kutugawa na kulipiza kisasi basi CDM wanaenda kuongeza ubaya kwenye mapungufu wanayolalamikia sasa.
CDM watakuwa wana nia tofauti na yale anayoongea mgombea wake, Lissu anaongea kuja kuliunganisha taifa na kuleta utawala wa haki na sheria vitu ambavyo ni kinyume kabisa na visasi.

Yaonekana wewe kweli haujijui unataka nini huko CDM na haujui kabisa CDM inataka nini, unafanya siasa ushabiki kama wa soka la Tanzania (Yanga na Simba).
 
Rais aliwaumbua TAKUKURU kuwa wanajipendekeza kwake kujifanya wanaipendelea Chato. Sasa msajili wa vyama awe makini sana. Tumemsikia kuhusu swala la wimbo wa Taifa akiwasema CHADEMA ila wale wasanii wa CCM aaa yuko kimya.

Taasis zote za serikali pamoja na Rais mwenyewe wanapaswa kujua upendeleo wowote kwa Rais msimu huu wa uchaguzi haumjengi bali unamuongezea chuki kwa wananchi na visasi kwenye sanduku la kura.

Tumeona hasira za wajumbe wa CCM kwa Rais tusitafute kuona na hasira za wananchi siku chache zijazo. Rais wangu kuwa makini na hawa wanaowachochea wananchi wakuchukie. Tuache uwanja huru kila mgombea ajipiganie.
 
waambie labda watakusikiliza wewe hao opportunist
 

Chadema wanazingua yani wanatafuta kiki kwenye kuchokonoa sheria. Naona lissu karudi kisharishari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…