CCM: Wananchi hawajawahi kudai Katiba mpya bali hilo ni takwa la wanasiasa kwa maslahi yao binafsi

Sawa, upo tayari upewe ukumbi wa kupigania hayo maslahi ya watanzania ewe shupavu miongoni mwa laki tano hadi milioni moja? Kuna namna inaweza fanyika ukaachana na porojo ukapigania hiyo katiba.
 
Naj
unajadiliana na mtu ambaye akili kazikabidhi kwa mama...chizi atakupotezea muda, ukijaribu kumwambia jalala ni chafu wakati mwenzio anajiona yupo KFC.
 
Sawa, upo tayari upewe ukumbi wa kupigania hayo maslahi ya watanzania ewe shupavu miongoni mwa laki tano hadi milioni moja? Kuna namna inaweza fanyika ukaachana na porojo ukapigania hiyo katiba.
Mbona tayari ukumbi mnauandaa wenyewe, au huna taarifa?
 
Naj

unajadiliana na mtu ambaye akili kazikabidhi kwa mama...chizi atakupotezea muda, ukijaribu kumwambia jalala ni chafu wakati mwenzio anajiona yupo KFC.
Najuwa.

Lakini huyu siyo chizi kama hawa wengi niliowahi waona hapa JF.

Huyu anaelewa wazi linalokuja kuwafyekea mbali CCM, anajikaza tu kuendeleza gumzo hapa.
 
Alituuliza lini kama tunahitaji tume huru na katiba mpya tukamwambia hatutaki? CCM iache tabia ya kuwa msemaji wa wananchi. Hii nchi tuachwe huru wananchi tuamue tunachotaka.
Brother, wale wahariri wa gazeti la Uhuru waliochapisha, mpaka likaingia mitaani, tayari wameshaonyesha wazi wazi kuwa wanataka Katiba mpya. Time will tell.
 
Mbona tayari ukumbi mnauandaa wenyewe, au huna taarifa?
Unakwepa kwepa, hata hivyo Ukumbi wa kumpigania jabali la siasa za upinzani mwenyekiti hujautumia hata ukitengenezewa ukumbi wa aina gani inaonekana mapambano yataishia humu humu kwa max.
 
Kama Katiba mpya ingekuwa kipaumbele Cha wananchi walio wengi kama tunavyoambiwa basi hao wananchi wangeiweka madarakani CDM ambayo katika chaguzi zote imekuwa ikiahidi hili.

Inakuwaje ishinde CCM isiyoahidi katiba mpya kama kweli ni kipaumbele chao.

NB:Mimi ni muumini wa kilichopo kwenye "Scoreboard" kwa hiyo kama mnaibiwa kura na mnashindwa kuchachamaa ili mbadili kilichopo kwenye ubao hizo kelele za kuibiwa kwangu ni porojo tu.
 
Mwambieni huyo chongo lao kwamba, maoni yaliyowekwa kwenye rasimu yalikusanywa kwa wananchi pia wanasiasa ni wanachi Tena siku wananchi wakianza kuidai katiba huo ukatibu utakuwa mchungu
 
CCM naehani safari hii wana katibu mwenye upungufu labda wa akili au kumbukumbu.

Report ya Jaji Warioba ilisema wananchi wanataka nini? Kama chama kama CCM kinakuwa na KM ambaye hana hata kumbukumbu ya mambo ya wazi namna hiyo, hivi huyu uwezo wake wa akili utakuwa unaishia wapi?
 
kubali usikubali huo ndiyo ukweli ila hamtaki kuukubali wanasiasa wanataka katiba mpya kwaajili ya kipengele cha tume huru tu ambayo wanayoitumiani wana siasa mwananchi wa kawaida inamhusu nini?
Wewe ni boya hasa maana huelewi chochote kuhusiana na report ya Jaji Warioba. Akili yako huenda inaishia kwenye kuutambua tu mdomo wako upo wapi.
 
Mimi si mwana siasa wala sitakuwa mwanasiasa.Suala la katiba ni takwa la wananchi siyo la wanasiasa.Kuna mambo mengi tunayashuhudia yanafanyika kutokana na katiba yetu isiyokithi mahitaji ya wakati huu.Tukumbuke katiba iliyopo sasa ni ya mfumo wa chama kimoja.CCM wanaonekana kupinga takwa la katiba mpya kwasababu wanajua waziwazi ikija katiba mpya kuna uwezekano wa kuangushwa katika chaguzi mbalimbali.Maendeleo na katiba vinakwenda pamoja.Leo tunashuhudia viongozi kama miungu watu.Uvunjaji wa haki unaathiri wanasiasa na wasio wanasiasa.Kwanini ccm mnakataa katiba mpya? Kimsingi sisi wananchi tunasemewa na wanasiasa na kama hatukubalini nao inadhihirika katika chaguzi.Lakini kwasasa hatuna chaguzi huru kutokana na haki kuminywa.Sasa nani watusemee wananchi? Wananchi ndiyo tulitoa maoni juu ya haja ya kuwa na katiba mpya kupitia tume ya jaji Warioba.
 
Makofi kwako tafadhali [emoji1319][emoji1319][emoji1319][emoji1319][emoji1319]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini tume ya Warioba ilichukua maini ya wananchi wasioelewa wanachodai?
 
Bwashee kama upo Dodoma wahi hapo Mirembe ngoja mimi niitishe kikao cha ukoo tuje kukugharamia.
 
Unakwepa kwepa, hata hivyo Ukumbi wa kumpigania jabali la siasa za upinzani mwenyekiti hujautumia hata ukitengenezewa ukumbi wa aina gani inaonekana mapambano yataishia humu humu kwa max.
Wewe kumbe ni mpuuzi!

Subiri hivyo hivyo kwa matumaini ya kuzima mabadiliko yanayoendelea.

Ndio, Mbowe ni sehemu na yumo ndani ya mapambano ya kuleta mabadiliko hadi sasa, hata kama kuwemo kwake huko halikuwa lengo lake na chama chake tokea huko mwanzo. Wapenda haki watamtumia kama mmoja wa viongozi wanaotafuta haki ndani ya nchi yetu.

Watu kama wewe mliolaza akili, msioona chochote kuhusu manyanyaso wanayofanyiwa watu kwa sababu mnafaidika na unyanyasaji huo, huwezi kuona na hata ukiona huwezi kuamini kwamba nchi yetu Tanzania tayari tunaekekea kwenye ukombozi toka kwa mkoloni mweusi chini ya CCM.
Subiri, utakapotikiswa ndipo utajuwa tayari ukombozi wa nchi yetu umekwishaanza na unaendelea, hakuna wa kuuzuia tena.
 
kubali usikubali huo ndiyo ukweli ila hamtaki kuukubali wanasiasa wanataka katiba mpya kwaajili ya kipengele cha tume huru tu ambayo wanayoitumiani wana siasa mwananchi wa kawaida inamhusu nini?
Kuna tatizo hapa...

Hujui bado madahara ya mwanasiasa katika maisha yako ya kila siku..

Ni bora pia ungepitia ripoti ya Warioba ungejua wanaichi wanataka nini katika katiba mpya. usipende kusikiliza wanasiasa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…