Tetesi: CCM wanapita vyuoni kuorodhesha UVCCM waliokosa mkopo

Tetesi: CCM wanapita vyuoni kuorodhesha UVCCM waliokosa mkopo

Victor wa happy

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2013
Posts
11,660
Reaction score
11,654
Viongozi wa UVCCM wameagizwa na viongozi wa CCM kupita kila chuo kuorodhesha wanachuo waliokosa mkopo ambao ni wana chama wa CCM

Zoezi hili linafanyika kwa siri, ili wanafunzi wasio wanachama wa CCM wasijue kinachoendelea

Ili uorodheshwe unatakiwa uonyeshe kadi ya CCM na registration number ya chuo

Zoezi hili limeanza wiki iliyopita mpaka mwishoni mwa juma
Rafiki yangu wakaribu ambaye ni UVCCM ameniambia wamehakikishiwa watapata mkopo

Nikarejea waziri wa elimu alisema atatoa mkopo kwa mwanafunzi wasiozid 25, 000 na hadi sasa wametoa kwa wanachuo 20, 000 tu

Ndio nchi yetu ilipofikia hapa, licha ya bwana mkubwa kuhubiri usawa but he doesn't walk his talk

Vijana wenzangu ambao sio makaada wa CCM wakipolisikia hili walitaharuki na kuanza kutafuta kadi za CCM ilimradi tu wawepo kwenye orodha ya CCM inayoratibiwa Lumumba

Poleni ndugu wanachuo msio CCM...
 
Vijana wa Ufipa hv mbowe anawalipa shilingi ngapi kwa uongo wa namna hii hv leo ukipelekwa mahakamani unao ushahidi wa upuuzi ulioandika hapa ???? au unadhani kutumia fake id hapa unaweza kuandika chochote tu ukitakacho?? na siku msitu huu ukifyekwa sijuh mtajificha wapi tena.
 
mie nimefunga ndoa ya kimila na nina watoto 6, sijafunga serikalini na wala kanisani au msikitini, hapa itakuwaje sasa, au ndoa ya mila haithaminiwi na kujulikana
 
Wewe huna macho y kuona tunakoelekea! Au umekalia kupingwax2 kila nachoambiwa! Dada badilika uache kutmika kama kalatsi ya chooni!
Leo ukiambiwa usibitishe alichokiandika mwenzio hapo juu unaweza au ndo una akili nyeusi kama kitako cha sufuria ????
 
Hii kweli wametusomesha. Asante sana CCM
 
Vijana wa Ufipa hv mbowe anawalipa shilingi ngapi kwa uongo wa namna hii hv leo ukipelekwa mahakamani unao ushahidi wa upuuzi ulioandika hapa ???? au unadhani kutumia fake id hapa unaweza kuandika chochote tu ukitakacho?? na siku msitu huu ukifyekwa sijuh mtajificha wapi tena.
Hakuna Linaloshindikana Chini Ya Jua Zaid ya Kifo
 
Vijana wa Ufipa hv mbowe anawalipa shilingi ngapi kwa uongo wa namna hii hv leo ukipelekwa mahakamani unao ushahidi wa upuuzi ulioandika hapa ???? au unadhani kutumia fake id hapa unaweza kuandika chochote tu ukitakacho?? na siku msitu huu ukifyekwa sijuh mtajificha wapi tena.
wewe endelea kujitoa ufahamu mengi yanakuja
 
Habari hii ni kweli ila pia chumvi imejazwa uvccm wanaandikisha majina kwa watoto wenye kundi maalum waliokosa mkopo tena napinga kabsa swala la eti ili uandikwe lazima uwe na kadi ya ccm kuna vijana wameandika majina yao ni yatima tena hawajaulizwa suala la kadi
 
Hii taarifa itakanushwa sasa hivi.....

Malaika wa ikulu sizani kama atakubali chama chake kuingia kwenye kashifa kama hii......
 
Back
Top Bottom