CCM wanatumia gharama kubwa kutafuta wananchi huku wananchi wanatumia gharama kubwa kumtafuta Lissu

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2011
Posts
3,882
Reaction score
5,896
Karibu kila chombo cha Habari kinaonekana kupigia chapuo chama cha Mapinduzi. Gharama Kubwa inaonekana kutumika kwa CCM kutafuta wananchi watakaoipigia Kura CCM.

Kinyume chake naona wananchi wanatumia gharama kubwa kumtafuta Lissu popote alipo hasa mitandaoni.

Ukikuta Kikundi cha watu kikao makini kinaangalia YouTube video sasa watakuwa wanamuangalia Lissu. Watu wananunua mabando ili wasikie lissu kasemaje na sio CCM wamesema walifanya nini.

Hili liwasaidie wanamikakati a CCM kuna wajipangeje katika hilo. Na iwasaidie wanamikakati wa CHADEMA kutengeneza Clips fupifupi zenye "nitche" ambazo zitakuwa viral kwenye social media.

Mpambano bado mbichi.
 
Miaka mitano hata wakizindua mtaro wako live. Ukimtesa au kumsumbua mtu unamuongezea umaarufu. Mseveni kamsumbua sana Bobby Wine leo anajuta kukabiliana naye
Kila kinachosemwa kilionyeshwa live. Bunge lilikuwa gizani bali serikali na maendeleo yake yalikuwa live kila siku. Hivyo hata vijijini wanajua. Sasa inaboa kuambiwa kitu ambavyo tayari anayekuambia ameshakuambia tena Mara nyingi.

Ni vizuri CCM waahidi na mambo Mapya yenye kuibua hisia za wafuatiliaji wao
 
Sifa pekee iliyobakia kwa CCM ni kama tu mfano wa "latrine" iliyojaa mikojo na vinyesi, ambapo mtu hulazimika kwenda humo kwa muda mfupi iwezekanavyo akiwa tu amezingirwa na faragha itokanayo na "call of nature". Mtu mwenye akili timamu hawezi kwenda humo kukesha na kulala kwa mategemeo ya kupata hewa safi na salama kwa afya ya mwili wake.
 
CCM wamelikoroga kwa kuwa na Mwenyekiti dikteta na mwenye akili ndogo. Sasa walinywe. Mahaba yapo magharibi. Jua limetua na watu hawakitaki tena hiki chama na Jiwe wao.
 
Wewe maccm yatakulaani??
 
Njooni mitaani huku kuna watu wanaipenda ccm mpaka unajiuliza hawa watu wana matatizo gani? Watu wananunua T shirt na madela ya ccm ili kwenda kampeni.

Na wote hao wanakubali kuwa kipindi hiki cha Magufuli maisha yamekuwa magumu ila bado wanaishabikia ccm.
 
Saccos hamna hoja, saccos hamuwezi fanya lolote maana hata sehemu kwenye wabunge wenu ni vioja vutupu. Hamna ilani, ni magumashi tu. Hamna viongozi weledi, wenye kuaminika zaidi ya wapigaji tu. Watanzania wawachague kwa kipi?.
 
Ile 5000 tunayolipwa kwa kuhudhuria kampeni za CCM huwa tunamchangia Tundu Lissu mafuta .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…