CCM watangaza kuvunja amani, mwanachama ahubiri kuwacharaza "Mboko" wapinzani

CCM watangaza kuvunja amani, mwanachama ahubiri kuwacharaza "Mboko" wapinzani

Kuna video clip inayosambaa ikimuonyesha mwanachama wa CCM akitangaza nia yake ya kuwapiga viboko viongozi wa upinzani huku akishangiliwa na wanachama wenzake.

Kitendo hiki na matukio mengine kama ya kushambuliwa msafara wa Lissu inaonyesha dhamira ya CCM kwenye uchaguzi huu.

Swali ninalojiuliza ni kwamba, je wapinzani wataendelea kuvumilia?

View attachment 1542604
Video: Mwanachama wa CCM akitangaza nia ya kuwashambulia wapinzani kwa viboko​
Intelijensia ya vigilantes imepata taarifa za awali kuhusu huyu kenge, taarifa za awali inasemekana anasoma cbe, dodoma, tunakamilisha profile yake tukamkatie bakora tumuanze yeye mboko, atakula bakora za kutosha, ulimi unamponza!
 
Katiba na sheria hazitambui matumizi ya lugha ya picha(Imagery na symbolism)
Mtu animalize form four na kufikiri anajua kila kitu
hahaha soma bandiko lako utajigundua wewe chama gani mkuu
Ukishatamka vitu hadharani, huna tena umiliki wa tafsiri ya kile ulichokitamka.

Uchaguzi sahihi wa maneno ni jambo la msingi sana.

Mdomo uliponza kichwa.
Siku zote mtu uhukumiwa kwa matendo yake, na matendo ya hao CCM kwa wapinzani hakuna asieyajua, usiwatetee hao wahuni, safari hii hakuna ataekubali kuonewa, ujinga wao sasa basi.
Muktadha wa mahali mhusika alipotolea hiyo kauli.
Kwani, Nape wakati ule, alipo tamka kuwa tutashinda hata kwa goli la mkono, alishutumiwa kwa kosa gani!?

Kama sio lugha ya picha ilitafsiriwa!?? Kwa hiyo bado pia matumizi ya lugha ya picha yana nafasi!

Ninacho maanisha hapa ni hiki, kwa nini Kwa kauli ya Nape itafsiriwe kwa lugha ya picha, na kauli ya huyo muhemshimiwa isitafsiriwe kwa lugha ya picha!??
 
Hawa malofa wa kijani wanazidi kujivua nguo hasa ktk kipindi hiki cha uchaguzi
 
Kuna video clip inayosambaa ikimuonyesha mwanachama wa CCM akitangaza nia yake ya kuwapiga viboko viongozi wa upinzani huku akishangiliwa na wanachama wenzake.

Kitendo hiki na matukio mengine kama ya kushambuliwa msafara wa Lissu inaonyesha dhamira ya CCM kwenye uchaguzi huu.

Swali ninalojiuliza ni kwamba, je wapinzani wataendelea kuvumilia?

View attachment 1542604
Video: Mwanachama wa CCM akitangaza nia ya kuwashambulia wapinzani kwa viboko​
Katika uchaguzi neno kumpiga au kupigwa humaanisha kumshinda mtu katika sanduku la kura!
 
Ukishatamka vitu hadharani, huna tena umiliki wa tafsiri ya kile ulichokitamka.

Uchaguzi sahihi wa maneno ni jambo la msingi sana.

Mdomo uliponza kichwa.
Mdomo ndio uliongea lakini kichwa ndio kikapigwa
 
Wahesabu idadi ya mboko upinzani umeshasema kitambo italipiza mara mbili kwa maana unapiga moja kwa moyo mkunjufu unarudishiwa moja na kuongezea bonasi moja. Pay one get two.
 
James Martin,

Mkuu, sorry.. mimi sio muumini wa masuala ya kisiasa.

Lakini nikuulize swali dogo sana, umepata kusoma fasihi kwenye kiswahili!??

Kuna kitu kinaitwa Lugha ya picha. Sasa neno "Mboko" laweza pia kuwa kimetumika kama lugha ya picha.

Inawezekana kabisa Muhusika akawa anamaanisha Mboko kwa maana ya kuwashinda au kuwaadhibu kupitia sanduku la kura.

Au pia yaweza kumaanisha kuwashinda kwa njia ya hoja dhabiti kabisa.

Hata hapa ndege imetumika kama lugha ya Picha.
JamiiForums-561822830_720x720.jpg
 
Ajaribu aone! wenzake waliporusha mawe tena mbele ya OCD kule Hai walipata kipondo hadi wakazimia. wajaribu watakutana na hasira za peoplezzzzzzzzzzzzzzz pawa
 
Kwani, Nape wakati ule, alipo tamka kuwa tutashinda hata kwa goli la mkono, alishutumiwa kwa kosa gani!?

Kama sio lugha ya picha ilitafsiriwa!?? Kwa hiyo bado pia matumizi ya lugha ya picha yana nafasi!

Ninacho maanisha hapa ni hiki, kwa nini Kwa kauli ya Nape itafsiriwe kwa lugha ya picha, na kauli ya huyo muhemshimiwa isitafsiriwe kwa lugha ya picha!??
Wewe upeo wako uko chini sana, ama msukumo wa kiCCM umekuharibu akili.

Huwezi kuanza kutafsiri jambo kwa 'lugha ya picha' kabla ya kulitafsiri kwa 'lugha halisi' kwanza. Lugha halisi huanza kwanza, na ikiwa lugha halisi haitoshei basi lugha ya picha ndio hufuatia. Hiyo ni kanuni ya kudumu kwenye lugha zote duniani.

Mtu aseme wazi kabisa, wapinzani tutawachapa viboko, halafu wewe useme hiyo ni lugha ya picha. Picha gani tena hapo, wakati ni kauli halisi.

Kuhusu kauli ya Nape, alisema CCM mwaka 2015 iko tayari kushinda hata kwa goli la mkono. Sote tunajua hiyo kauli haitoshi kuwa 'kauli halisi', hivyo tafsiri ya lugha ya picha ikafuatia.
 
Kuna video clip inayosambaa ikimuonyesha mwanachama wa CCM akitangaza nia yake ya kuwapiga viboko viongozi wa upinzani huku akishangiliwa na wanachama wenzake.

Kitendo hiki na matukio mengine kama ya kushambuliwa msafara wa Lissu inaonyesha dhamira ya CCM kwenye Uchaguzi huu.

Swali ninalojiuliza ni kwamba, je wapinzani wataendelea kuvumilia?

View attachment 1542604
Video: Mwanachama wa CCM akitangaza nia ya kuwashambulia wapinzani kwa viboko​

Kamanda Siro, ungeonesha pia documentary ya Mkurugenzi wa Kinondoni kuzuia VITAMBULISHO VYA MAWAKALA ambapo ndiyo MSINGI WA VURUGU ZA KINONDONI.

UNGEONESHA PIA DOCUMENTARY YA WAKURUGENZI KUKIMBIA OFISI ZAO WAKATI WA KUTOA NA KUPOKEA FOMU ZA WAGOMBEA.

UNGETOA PIA DOCUMENTARY YA WANASIASA WA UPINZANI WALIVYOUAWA, UMIZWA NA KUBAMBIKWA KESI NA JINSI POLISI WALIVYO SHUGHULIKIA MATUKIO HAYO.

MFANO:-
WEKA DOCUMENTARY YA JINSI LISU ALIVYOSHAMBULIWA KWA RISASI KWENYE ENEO LENYE ULINZI NA KAMERA NYINGI BILA KUJALI WALIOMSHAMBULIA NI WENZAKE AU WAPINZANI WAKE KISIASA.

HAPO UNGEKUWA UMETUMIA MIZANIA YA HABARI KWA WEREDI WA HALI YA JUU.
 
Wewe upeo wako uko chini sana, ama msukumo wa kiCCM umekuharibu akili.

Huwezi kuanza kutafsiri jambo kwa 'lugha ya picha' kabla ya kulitafsiri kwa 'lugha halisi' kwanza. Lugha halisi huanza kwanza, na ikiwa lugha halisi haitoshei basi lugha ya picha ndio hufuatia. Hiyo ni kanuni ya kudumu kwenye lugha zote duniani.

Mtu aseme wazi kabisa, wapinzani tutawachapa viboko, halafu wewe useme hiyo ni lugha ya picha. Picha gani tena hapo, wakati ni kauli halisi.

Kuhusu kauli ya Nape, alisema CCM mwaka 2015 iko tayari kushinda hata kwa goli la mkono. Sote tunajua hiyo kauli haitoshi kuwa 'kauli halisi', hivyo tafsiri ya lugha ya picha ikafuatia.
Twende taratibu boss.

Kwani nini kazi ya lugha ya picha!??
 
Kwa kosa hapo ni lipi mkuu!?
Jana Siro ali-present paper yake ya usalama wakati wa uchaguzi ambapo alionesha Documentary ambayo ilikuwa na clips za wafuasi wa CHADEMA wakiwa wanaandamana. Naibu Katibu wa CHADEMA alishangaa kwa nini hajaonesha clips za vyama vingine? Ndiyo maana mchangiaji anafikiri kwamba hii clip ya CCM ya kutandika wapinzani viboko nayo ingeoneshwa na Siro kama mfano wa namna vurugu zinaweza kusababishwa na vyama vyote na si kukitazama chama kimoja tu kama mfano.
 
Back
Top Bottom