DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Kenani Kihongosi amesema kuwa tangu kuanza kwa mikutano ya kampeni za Urais kupitia CCM kwa mgombea wake Samia Suluhu Hassan tayari zaidi ya wananchi milioni 45 wameshiriki kikamilifu kwa kufuatilia mikutano yake ikiwa milioni 14.6 wameshiriki mikutanoni na milioni 31.6 wamefuatilia kupitia vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya kijamii.
Akizungumza na wanahabari leo tarehe 5 Oktoba 2025 katika ukumbi wa mikutano wa CCM ofisi kuu Jijini Dodoma, Mwenezi Kenani amesema CCM ilifanya uzinduzi wa kampeni zake wa kihistoria pale Kawe Jijini Dar es salaam tarehe 28 Agosti 2025 kwakuwa ilivunja rekodi ya maudhurio na shamrashamra tangu kuasisiwa kwake.
"Zaidi ya watu milioni 14.6 wamejitokeza kwenye mikutano [ya CCM] ya moja kwa moja. Lakini zaidi ya watu milioni 31.6 wamefuatilia kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii." - Kenan Kihongosi, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM.