GE2025 CCM: Watu milioni 14 wamejitokeza kwenye kampeni, milioni 31 wametazama kupitia vyombo vya habari

GE2025 CCM: Watu milioni 14 wamejitokeza kwenye kampeni, milioni 31 wametazama kupitia vyombo vya habari

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Wakuu,

Kwa hiyo kati ya hawa watu Milioni 40 hakuna hata mmoja anayejitokeza kuwatetea mtandaoni maana mtandaoni kote ni wanapigwa spana tu na wananchi? Hawa watu Milioni 40 mbona hatuwaoni huku mitaani?

==============================

Katibu wa Uenezi na Itikadi CCM Kenani Kihongosi amesema kuwa tangu kuanza kwa mikutano ya kampeni za Urais kupitia CCM kwa mgombea wake Rais Samia Suluhu tayari zaidi ya wananchi milioni 45 wameshiriki kikamilifu kwa kufuatilia mikutano yake ikiwa milioni 14.6 wameshiriki mikutanoni na milioni 31.6 wamefuatilia kupitia vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya kijamii.

kihongosi.png
 
Hii ni trela picha kamili ni siku ya kutangaza matokeo. Tutapigwa na butwaa lakini hatutashangaa, tutakwazika lakini hatutafanya chochote. Hii ndio CCM ya wanamtandao. Wao wanachojali ni maslahi yao tu si kitu kingine

Vituo vya kupigia kura vitakuwa empty lakini takwimu mtakazosomewa zitakuwa za ajabu sana. Rejea yangu ni ule uchaguzi wa serikali za mitaa. Kama ulikuwa hufuatilii au haukushiriki huwezijua kilichofanyika

Hivi ndivyo wanamtandao hupenda. Yaani hata mkisusa wao hawajali kwasababu wanajua watafanya yao na mtakaa kimya na mtasahau

Kumbukeni kiongozi wao anamsemo wake maarufu yakuwa "ni upepo tu, yatapita"
 
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Kenani Kihongosi amesema kuwa tangu kuanza kwa mikutano ya kampeni za Urais kupitia CCM kwa mgombea wake Samia Suluhu Hassan tayari zaidi ya wananchi milioni 45 wameshiriki kikamilifu kwa kufuatilia mikutano yake ikiwa milioni 14.6 wameshiriki mikutanoni na milioni 31.6 wamefuatilia kupitia vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya kijamii.

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 5 Oktoba 2025 katika ukumbi wa mikutano wa CCM ofisi kuu Jijini Dodoma, Mwenezi Kenani amesema CCM ilifanya uzinduzi wa kampeni zake wa kihistoria pale Kawe Jijini Dar es salaam tarehe 28 Agosti 2025 kwakuwa ilivunja rekodi ya maudhurio na shamrashamra tangu kuasisiwa kwake.

"Zaidi ya watu milioni 14.6 wamejitokeza kwenye mikutano [ya CCM] ya moja kwa moja. Lakini zaidi ya watu milioni 31.6 wamefuatilia kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii." - Kenan Kihongosi, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM.
Mwehu kweli huyu
 
Hivi uwanjani kwenye kampeni idadi ya watu unaijuaje?

Tufanye mna uwezo wa kujua, sasa mtu mmoja akienda kwenye mikutano mitatu tofauti mnajuaje ili kutomuhesabu mara 3?
 
 
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Kenani Kihongosi amesema kuwa tangu kuanza kwa mikutano ya kampeni za Urais kupitia CCM kwa mgombea wake Samia Suluhu Hassan tayari zaidi ya wananchi milioni 45 wameshiriki kikamilifu kwa kufuatilia mikutano yake ikiwa milioni 14.6 wameshiriki mikutanoni na milioni 31.6 wamefuatilia kupitia vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya kijamii.

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 5 Oktoba 2025 katika ukumbi wa mikutano wa CCM ofisi kuu Jijini Dodoma, Mwenezi Kenani amesema CCM ilifanya uzinduzi wa kampeni zake wa kihistoria pale Kawe Jijini Dar es salaam tarehe 28 Agosti 2025 kwakuwa ilivunja rekodi ya maudhurio na shamrashamra tangu kuasisiwa kwake.

"Zaidi ya watu milioni 14.6 wamejitokeza kwenye mikutano [ya CCM] ya moja kwa moja. Lakini zaidi ya watu milioni 31.6 wamefuatilia kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii." - Kenan Kihongosi, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM.
Methodology- umefikiaje hao 14 million?
 
Asilimia kubwa ni wenyewe ccm.
 

Attachments

  • IMG_20251004_175743_841.jpg
    IMG_20251004_175743_841.jpg
    719.2 KB · Views: 21
  • IMG_20251004_175742_023.jpg
    IMG_20251004_175742_023.jpg
    721.6 KB · Views: 19
Back
Top Bottom