Pre GE2025 CCM waweka ukomo nafasi za ubunge na udiwani viti maalum, waja na kauli mbiu mpya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

IMG-20250311-WA0000.jpg
IMG-20250311-WA0001.jpg
IMG-20250311-WA0002.jpg

TAARIFA KWA UMMA

Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, imefanya kikao chake maalum jana tarehe 10 Machi, 2025 jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Katika kikao hicho, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imepokea na kujadili agenda kuu mbili kama zifuatazo:-

(i). Mapendekezo ya Marekebisho ya Kanuni za Uteuzi wa Wagombea Uongozi katika Vyombo vya Dola toleo la 2022 na

(ii). Rasimu ya Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa 2025-2030

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Kanuni za Uteuzi wa Wagombea Uongozi katika Vyombo vya Dola, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imeridhia mapendekezo ya marekebisho ya Kanuni hizo. Maeneo yaliyofanyiwa marekebisho ni kama ifuatavyo:-

1. Mchakato wa uchujaji na uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge, uwakilishi wa majimbo na udiwani wa kata/wadi.

2. Mchakato wa uchujaji na uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani wa viti maalum wanawake.

3. Upanuzi wa wigo wa idadi ya wajumbe wa vikao vya chama na jumuiya zake watakaopiga kura za maoni. Lengo la hatua hii ni kuimarisha misingi ya demokrasia, uwazi na kupanua uwakilishi wa wanachama wa CCM katika kuwapata wagombea wa nafasi za uongozi katika chaguzi za vyombo vya dola. Utaratibu utakuwa kama ifuatavyo:-

(a) Kwa upande wa wabunge wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) ngazi ya mikoa, kwa upande wa Tanzania Bara

Mkutano Mkuu Maalumu wa UWT wa Mkoa, ambao utakuwa na wajumbe wafuatao :-

(i) Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa UWT wa Mkoa (Kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za UWT).

(ii) Wajumbe wote wa Kamati za Utekelezaji wa UWT za Wilaya.

(iii) Wajumbe wote wa Kamati za Utekelezaji wa UWT za Kata.

Kwa upande wa Zanzibar Mkutano Mkuu Maalumu wa UWT wa

Mkoa, utakuwa na wajumbe wafuatao :-

(i) Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa UWT wa Mkoa.

(ii) Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Wilaya.

(iii) Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Jimbo.

(iv) Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Kata/Wadi.

(v) Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Matawi.

(b) Kwa upande wa Jumuiya ya UVCCM na WAZAZI

Kura za maoni kwa waombaji nafasi za Ubunge/Uwakilishi wa viti maalumu wanawake kupitia Jumuiya ya UVCCM na WAZAZI zitapigwa na wajumbe wa Mikutano Mikuu Maalumu ya Taifa, kwa utaratibu ufuatao:-

Mikutano Mikuu ya Taifa ya UVCCM/WAZAZI itakua na wajumbe Wanawake tu; wajumbe hao ni kama wafuatao

(i) Wajumbe wote wanawake wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa UVCCM/WAZAZI.

(ii) Wajumbe wote Wanawake wa Kamati za Utekelezaji za UVCCM/WAZAZI za Mikoa.

(iii) Wajumbe wote Wanawake wa Kamati za Utekelezai za Wilaya UVCCM/Wazazi.

Ukomo wa viti maalum

Kuweka ukomo wa vipindi viwili vya miaka mitano kwa nafasi za ubunge/uwakilishi na udiwani wa viti maalum wanawake. Ukomo huo utaanza kutumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2030.

Vilevile, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imepitisha Kauli Mbiu rasmi kwa ajili ya kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2025 isemayo;

"KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE"

Kauli mbiu hiyo inaakisi dhamira ya Chama ya kuendeleza juhudi za ujenzi wa Taifa lenye maendeleo jumuishi, mshikamano wa kitaifa na ustawi wa watu wenye kujali UTU.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Issa Haji Ussi (GAVU)
KATIBU WA NEC ORGANAIZESHENI
11 Machi, 2025​
 
Attachments

  • ccm kauli mbiu.png
    ccm kauli mbiu.png
    477.6 KB · Views: 1
Wakuu,

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kauli mbiu yake itakayotumika kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, 2025.

Kauli mbiu hiyo ya Kazi na Utu, Tunasonga Mbele imepitishwa kwenye Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) iliyoketi jijini Dodoma Jumatatu Machi 10, 2025.

Katika uchaguzi wa Mwaka 2020, kauli mbiu ya CCM iliyokuwa ikinadiwa na mgombea urais wake, Hayati John Magufuli ni Kazi Iendelee huku ile aliyoanza nayo 2015 ilikuwa ni ‘Hapa Kazi Tu’.

Utu gani wkt watu wanatekwa na wengi kupotezwa! Ndio utu huo!?
 
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC) imefanya mkutano muhimu chini ya Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan, kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na maendeleo ya chama na uchaguzi wa mwaka 2025.

Miongoni mwa masuala hayo ni ukomo wa viti maalumu, ambao umepewa kipaumbele na umezingatiwa kwa kina.

Katika mkutano huo, NEC ilitoa maamuzi magumu kuhusu ukomo wa muda kwa wale wanaoshikilia viti maalumu. Uamuzi huu unalenga kuhakikisha kuwa viongozi wanaingia katika nafasi hizo wanakuwa na mwendelezo wa uongozi wenye tija na ubunifu. Kwa mujibu wa uamuzi huo, viongozi watakaoshika viti maalumu wataruhusiwa kuhudumu kwa vipindi viwili tu, yaani miaka 10. Baada ya muda huo, wale waliohudumu zaidi ya vipindi viwili hawataruhusiwa kuchukua fomu za kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Uamuzi huu unakuja katika kipindi ambacho chama kinahitaji kujiimarisha na kuleta mabadiliko ya kweli katika uongozi. Ni dhahiri kwamba, kukithiri kwa viongozi wanaoshikilia nafasi hizo kwa muda mrefu kunaweza kuzuia nafasi mpya za uongozi na kuleta changamoto katika mabadiliko ya sera na mikakati ya maendeleo. Kwa hivyo, NEC imeona ni vyema kuweka ukomo huu ili kuhakikisha kuna uwanja mpana kwa viongozi wapya kuingia na kutoa mawazo mapya.

Aidha, uamuzi huu unalenga kuimarisha uwajibikaji miongoni mwa viongozi. Kwa kuweka ukomo wa muda, viongozi watahimizwa kufanya kazi kwa bidii na kuwajibika kwa wananchi, wakijua kuwa nafasi zao zinaweza kuchukuliwa na wengine baada ya muda fulani. Hii itawasaidia kuzingatia zaidi maslahi ya wananchi na siyo maslahi binafsi.

Wakati wa mkutano huo, NEC pia ilijadili masuala mengine muhimu, ikiwa ni pamoja na mikakati ya kuimarisha chama na kuandaa mkakati wa uchaguzi wa mwaka 2025. Mkutano huu ni sehemu ya maandalizi ya chama kuelekea uchaguzi huo, ambapo lengo ni kuhakikisha CCM inabaki kuwa chama chenye nguvu na kinachoheshimiwa na wananchi.

NEC ilisisitiza umuhimu wa umoja na ushirikiano ndani ya chama. Katika kipindi hiki, ni muhimu kwa wanachama wote kuwa na mshikamano ili kufanikisha malengo ya chama. Hali hii itasaidia katika kutengeneza mazingira mazuri ya uchaguzi, ambapo kila mwanachama atakuwa na nafasi ya kuchangia mawazo na mikakati ya chama.

Kwa upande mwingine, NEC ilisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano kati ya chama na wananchi. Chama kinatakiwa kuwasikiliza wananchi na kuelewa mahitaji yao ili kuweza kuwapatia suluhisho stahiki. Hii itasaidia katika kujenga imani na kuimarisha uhusiano mzuri kati ya viongozi na wananchi.

Katika mkutano huo, Rais Samia Suluhu Hassan alisisitiza kwamba uongozi bora ni wa msingi katika maendeleo ya chama na nchi kwa ujumla. Alitoa wito kwa viongozi wote wa CCM kuzingatia maadili ya uongozi, ikiwa ni pamoja na uwazi, uwajibikaji, na kuheshimu sheria. Hali hii itasaidia katika kujenga chama chenye nguvu na chenye uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Kwa kumalizia, mkutano wa NEC umekuwa na umuhimu mkubwa katika kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2025. Uamuzi wa kuweka ukomo wa viti maalumu ni hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa kuna nafasi ya uongozi mpya na wa kisasa. Huu ni wakati wa mabadiliko na maendeleo, na CCM inakwenda katika mwelekeo sahihi wa kuhakikisha kuwa inabaki kuwa chama chenye nguvu na kinachowakilisha maslahi ya wananchi. Viongozi wanapaswa kuzingatia maamuzi haya na kufanya kazi kwa pamoja ili kufanikisha malengo ya chama na kuimarisha demokrasia nchini.
 
Ni wazo la chadema wamesoma upepo.Unajua kwa nini wanaogopa chadema wakiambiwa hawana akili utumia wasiojulikana na mwisho ujiona akili zimekosekana wanaamua kufata ya chadema ili wasishitukiwe.
 
Dah Mungu kasikia kilio changu aisee Hawa watu siwapendinwako wanataka kuishi milele
 
Back
Top Bottom