Pre GE2025 CCM waweka ukomo nafasi za ubunge na udiwani viti maalum, waja na kauli mbiu mpya

Pre GE2025 CCM waweka ukomo nafasi za ubunge na udiwani viti maalum, waja na kauli mbiu mpya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huna hoja umejenga hapa badala yake umepost upuz wote walio ulioupitisha majiz I yale,,
 
Hiyo kauli mbiu ni ngumu kuitekeleza na itawapa wakati mgumu sana, anza na kazi mtaani kuna lundo la vijana ambao serikali ya CCM imegoma kuwaajiri toka 2015 na kila mwaka wanaongezeka kwenye kampeni watakuja na mkakati upi wa kuwapa ajira au kazi vijana hao ambao wengi wao ndiyo wapiga kura

Utu hapa napo ni kizingiti kingine maana kuna familia nyingi zenye makovu ya vijana wao waliotekwa na mpk leo hawajulikani mahali walipo na serikali iko kimya na hata wale waliotekwa na baadaye kupatikana au wengine kuuwawa bado serikali imebaki kimya ni utu gani utauhubiri ili wapiga kura wakuamini!?
 
Wakuu,

Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, imefanya kikao chake maalum jana tarehe 10 Machi, 2025 jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Katika kikao hicho, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imepokea na kujadili agenda kuu mbili kama zifuatazo:-

(i). Mapendekezo ya Marekebisho ya Kanuni za Uteuzi wa Wagombea Uongozi katika Vyombo vya Dola toleo la 2022 na

(ii). Rasimu ya Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa 2025-2030

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Kanuni za Uteuzi wa Wagombea Uongozi katika Vyombo vya Dola, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imeridhia mapendekezo ya marekebisho ya Kanuni hizo. Maeneo yaliyofanyiwa marekebisho ni kama ifuatavyo:-

1. Mchakato wa uchujaji na uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge, uwakilishi wa majimbo na udiwani wa kata/wadi.

2. Mchakato wa uchujaji na uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani wa viti maalum wanawake.

3. Upanuzi wa wigo wa idadi ya wajumbe wa vikao vya chama na jumuiya zake watakaopiga kura za maoni. Lengo la hatua hii ni kuimarisha misingi ya demokrasia, uwazi na kupanua uwakilishi wa wanachama wa CCM katika kuwapata wagombea wa nafasi za uongozi katika chaguzi za vyombo vya dola. Utaratibu utakuwa kama ifuatavyo:-

(a) Kwa upande wa wabunge wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) ngazi ya mikoa, kwa upande wa Tanzania Bara

Mkutano Mkuu Maalumu wa UWT wa Mkoa, ambao utakuwa na wajumbe wafuatao :-

(i) Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa UWT wa Mkoa (Kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za UWT).

(ii) Wajumbe wote wa Kamati za Utekelezaji wa UWT za Wilaya.

(iii) Wajumbe wote wa Kamati za Utekelezaji wa UWT za Kata.

Kwa upande wa Zanzibar Mkutano Mkuu Maalumu wa UWT wa

Mkoa, utakuwa na wajumbe wafuatao :-

(i) Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa UWT wa Mkoa.

(ii) Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Wilaya.

(iii) Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Jimbo.

(iv) Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Kata/Wadi.

(v) Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Matawi.

(b) Kwa upande wa Jumuiya ya UVCCM na WAZAZI

Kura za maoni kwa waombaji nafasi za Ubunge/Uwakilishi wa viti maalumu wanawake kupitia Jumuiya ya UVCCM na WAZAZI zitapigwa na wajumbe wa Mikutano Mikuu Maalumu ya Taifa, kwa utaratibu ufuatao:-

Mikutano Mikuu ya Taifa ya UVCCM/WAZAZI itakua na wajumbe Wanawake tu; wajumbe hao ni kama wafuatao

(i) Wajumbe wote wanawake wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa UVCCM/WAZAZI.

(ii) Wajumbe wote Wanawake wa Kamati za Utekelezaji za UVCCM/WAZAZI za Mikoa.

(iii) Wajumbe wote Wanawake wa Kamati za Utekelezai za Wilaya UVCCM/Wazazi.

Ukomo wa viti maalum

Kuweka ukomo wa vipindi viwili vya miaka mitano kwa nafasi za ubunge/uwakilishi na udiwani wa viti maalum wanawake. Ukomo huo utaanza kutumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2030.

Vilevile, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imepitisha Kauli Mbiu rasmi kwa ajili ya kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2025 isemayo;

"KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE"

Kauli mbiu hiyo inaakisi dhamira ya Chama ya kuendeleza juhudi za ujenzi wa Taifa lenye maendeleo jumuishi, mshikamano wa kitaifa na ustawi wa watu wenye kujali UTU.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Issa Haji Ussi (GAVU)
KATIBU WA NEC ORGANAIZESHENI
11 Machi, 2025​

Naona kama HILI la ukomo wa viti maalumu wamekopa kwa Tundu Antipas Lisu (TAL).alilizungumzia hili wakatinwa kuapishwa kwake
 
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC) imefanya mkutano muhimu chini ya Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan, kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na maendeleo ya chama na uchaguzi wa mwaka 2025.

Miongoni mwa masuala hayo ni ukomo wa viti maalumu, ambao umepewa kipaumbele na umezingatiwa kwa kina.

Katika mkutano huo, NEC ilitoa maamuzi magumu kuhusu ukomo wa muda kwa wale wanaoshikilia viti maalumu. Uamuzi huu unalenga kuhakikisha kuwa viongozi wanaingia katika nafasi hizo wanakuwa na mwendelezo wa uongozi wenye tija na ubunifu. Kwa mujibu wa uamuzi huo, viongozi watakaoshika viti maalumu wataruhusiwa kuhudumu kwa vipindi viwili tu, yaani miaka 10. Baada ya muda huo, wale waliohudumu zaidi ya vipindi viwili hawataruhusiwa kuchukua fomu za kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Uamuzi huu unakuja katika kipindi ambacho chama kinahitaji kujiimarisha na kuleta mabadiliko ya kweli katika uongozi. Ni dhahiri kwamba, kukithiri kwa viongozi wanaoshikilia nafasi hizo kwa muda mrefu kunaweza kuzuia nafasi mpya za uongozi na kuleta changamoto katika mabadiliko ya sera na mikakati ya maendeleo. Kwa hivyo, NEC imeona ni vyema kuweka ukomo huu ili kuhakikisha kuna uwanja mpana kwa viongozi wapya kuingia na kutoa mawazo mapya.

Aidha, uamuzi huu unalenga kuimarisha uwajibikaji miongoni mwa viongozi. Kwa kuweka ukomo wa muda, viongozi watahimizwa kufanya kazi kwa bidii na kuwajibika kwa wananchi, wakijua kuwa nafasi zao zinaweza kuchukuliwa na wengine baada ya muda fulani. Hii itawasaidia kuzingatia zaidi maslahi ya wananchi na siyo maslahi binafsi.

Wakati wa mkutano huo, NEC pia ilijadili masuala mengine muhimu, ikiwa ni pamoja na mikakati ya kuimarisha chama na kuandaa mkakati wa uchaguzi wa mwaka 2025. Mkutano huu ni sehemu ya maandalizi ya chama kuelekea uchaguzi huo, ambapo lengo ni kuhakikisha CCM inabaki kuwa chama chenye nguvu na kinachoheshimiwa na wananchi.

NEC ilisisitiza umuhimu wa umoja na ushirikiano ndani ya chama. Katika kipindi hiki, ni muhimu kwa wanachama wote kuwa na mshikamano ili kufanikisha malengo ya chama. Hali hii itasaidia katika kutengeneza mazingira mazuri ya uchaguzi, ambapo kila mwanachama atakuwa na nafasi ya kuchangia mawazo na mikakati ya chama.

Kwa upande mwingine, NEC ilisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano kati ya chama na wananchi. Chama kinatakiwa kuwasikiliza wananchi na kuelewa mahitaji yao ili kuweza kuwapatia suluhisho stahiki. Hii itasaidia katika kujenga imani na kuimarisha uhusiano mzuri kati ya viongozi na wananchi.

Katika mkutano huo, Rais Samia Suluhu Hassan alisisitiza kwamba uongozi bora ni wa msingi katika maendeleo ya chama na nchi kwa ujumla. Alitoa wito kwa viongozi wote wa CCM kuzingatia maadili ya uongozi, ikiwa ni pamoja na uwazi, uwajibikaji, na kuheshimu sheria. Hali hii itasaidia katika kujenga chama chenye nguvu na chenye uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Kwa kumalizia, mkutano wa NEC umekuwa na umuhimu mkubwa katika kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2025. Uamuzi wa kuweka ukomo wa viti maalumu ni hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa kuna nafasi ya uongozi mpya na wa kisasa. Huu ni wakati wa mabadiliko na maendeleo, na CCM inakwenda katika mwelekeo sahihi wa kuhakikisha kuwa inabaki kuwa chama chenye nguvu na kinachowakilisha maslahi ya wananchi. Viongozi wanapaswa kuzingatia maamuzi haya na kufanya kazi kwa pamoja ili kufanikisha malengo ya chama na kuimarisha demokrasia nchini.
Unarudia nini Sasa? Taarifa imepostiwa huko juu unarudia kupost nini Sasa?
 
Labda kwa CCM maana ya utu ni uharamia. wanateka watu wanaomkosoa Rais, wanawapoteza watu wanaomkosoa Rais au Setikali yake, wanawaua wanaomkosoa Rais au Serikali yake, huo ndiyo utu wa CCM!!
 
Wakuu,

Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, imefanya kikao chake maalum jana tarehe 10 Machi, 2025 jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Katika kikao hicho, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imepokea na kujadili agenda kuu mbili kama zifuatazo:-

(i). Mapendekezo ya Marekebisho ya Kanuni za Uteuzi wa Wagombea Uongozi katika Vyombo vya Dola toleo la 2022 na

(ii). Rasimu ya Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa 2025-2030

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Kanuni za Uteuzi wa Wagombea Uongozi katika Vyombo vya Dola, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imeridhia mapendekezo ya marekebisho ya Kanuni hizo. Maeneo yaliyofanyiwa marekebisho ni kama ifuatavyo:-

1. Mchakato wa uchujaji na uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge, uwakilishi wa majimbo na udiwani wa kata/wadi.

2. Mchakato wa uchujaji na uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani wa viti maalum wanawake.

3. Upanuzi wa wigo wa idadi ya wajumbe wa vikao vya chama na jumuiya zake watakaopiga kura za maoni. Lengo la hatua hii ni kuimarisha misingi ya demokrasia, uwazi na kupanua uwakilishi wa wanachama wa CCM katika kuwapata wagombea wa nafasi za uongozi katika chaguzi za vyombo vya dola. Utaratibu utakuwa kama ifuatavyo:-

(a) Kwa upande wa wabunge wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) ngazi ya mikoa, kwa upande wa Tanzania Bara

Mkutano Mkuu Maalumu wa UWT wa Mkoa, ambao utakuwa na wajumbe wafuatao :-

(i) Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa UWT wa Mkoa (Kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za UWT).

(ii) Wajumbe wote wa Kamati za Utekelezaji wa UWT za Wilaya.

(iii) Wajumbe wote wa Kamati za Utekelezaji wa UWT za Kata.

Kwa upande wa Zanzibar Mkutano Mkuu Maalumu wa UWT wa

Mkoa, utakuwa na wajumbe wafuatao :-

(i) Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa UWT wa Mkoa.

(ii) Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Wilaya.

(iii) Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Jimbo.

(iv) Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Kata/Wadi.

(v) Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Matawi.

(b) Kwa upande wa Jumuiya ya UVCCM na WAZAZI

Kura za maoni kwa waombaji nafasi za Ubunge/Uwakilishi wa viti maalumu wanawake kupitia Jumuiya ya UVCCM na WAZAZI zitapigwa na wajumbe wa Mikutano Mikuu Maalumu ya Taifa, kwa utaratibu ufuatao:-

Mikutano Mikuu ya Taifa ya UVCCM/WAZAZI itakua na wajumbe Wanawake tu; wajumbe hao ni kama wafuatao

(i) Wajumbe wote wanawake wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa UVCCM/WAZAZI.

(ii) Wajumbe wote Wanawake wa Kamati za Utekelezaji za UVCCM/WAZAZI za Mikoa.

(iii) Wajumbe wote Wanawake wa Kamati za Utekelezai za Wilaya UVCCM/Wazazi.

Ukomo wa viti maalum

Kuweka ukomo wa vipindi viwili vya miaka mitano kwa nafasi za ubunge/uwakilishi na udiwani wa viti maalum wanawake. Ukomo huo utaanza kutumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2030.

Vilevile, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imepitisha Kauli Mbiu rasmi kwa ajili ya kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2025 isemayo;

"KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE"

Kauli mbiu hiyo inaakisi dhamira ya Chama ya kuendeleza juhudi za ujenzi wa Taifa lenye maendeleo jumuishi, mshikamano wa kitaifa na ustawi wa watu wenye kujali UTU.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Issa Haji Ussi (GAVU)
KATIBU WA NEC ORGANAIZESHENI
11 Machi, 2025​
Chama kinatapatapa pa kushika hakuonekani ,Mungu uyu
 
Kauli Mbiu rasmi ya CCM kwa ajili ya kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2025

"KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE"
20250312_011317.jpg
 
Kwanini tunapenda kushtukizwa? Ndio maana hata leo Mhe Rais kawaambia wateule wake "kama unautaka kule sema mapema tujue" maana yake uelewa wa jambo mapema inatoa mwanya wa ufahamu, na kutoa maoni kwa mstakbali mwema wa maendeleo. Ni muda sahihi mimi naona kwa mtazamo wangu
 
Naona kama HILI la ukomo wa viti maalumu wamekopa kwa Tundu Antipas Lisu (TAL).alilizungumzia hili wakatinwa kuapishwa kwake
Kazi ya chama tawala ndio hiyo.pia kuchukua mawazo mazuri toka chanzo chochote iwe mwananchi wa kawaida au vyama vya upinzani na kuyafanyia kazi kikiona yana mashiko
 
Tundu Lisssu alisema kwamba atahakikisha anaweka ukomo wa viti Maalum.

Punde si punde nyinyiemu nao wakasema nao wamechoka viti Maalum.

Siku zote Tundu Lissu yupo Mbele. Ni kama maji. Usipoyanywa, utayaoga

Pre GE2025 - Lissu: Tutaweka ukomo Ubunge Viti Maalum isiwe kikundi cha wale wale miaka yote

Tarehe 23 Desemba 2025 Tundu Lissu ambaye sasa ni Mwenyekiti wa CHADEMA alisema;

"Tutaweka ukomo wa Ubunge wa Viti Maalum ili wanawake wengi wanaokipigania Chama wapate fursa na isiwe kikundi cha watu wale wale miaka yote".
View attachment 3267166
Dar/Dodoma. Mjadala wa kuitaka ukomo wa udiwani na ubunge wa viti maalumu ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) umepata majibu baada ya chama hicho kuridhia vipindi visivyozidi viwili (miaka 10).

Kumekuwa na sauti za makada ndani ya nje ya chama hicho, zitaka uwekwe ukomo kwenye nafasi hizo ili kuondoa tabia ya wachache kung’ang’ania nafasi hizo na kutoa fursa kwa wanawake wengi kupata uzoefu huo.
View attachment 3267168
Tindu kuongea hajambo kutekeleza yuko zero

Mbona hadi lro hajaweka huo ukomo wala kuitisha kamati kuu iweke huo ukomo? Anaongea vitu utekelezaji hamna kitu

Yeye mwenyewe alisema wataweka ukomo wa nafasi ya Mwenyekiti hiyo yake hadi.lro yuko kimya haongelei hilo tena baada ya kuchaguliwa
 
Ukomo wa viti maalum

Kuweka ukomo wa vipindi viwili vya miaka mitano kwa nafasi za ubunge/uwakilishi na udiwani wa viti maalum wanawake. Ukomo huo utaanza kutumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2030.
Viti maalumu na viti vyote viwe na ukomo ka ilivyo kwa Rais
 
Ni wazo la chadema wamesoma upepo.Unajua kwa nini wanaogopa chadema wakiambiwa hawana akili utumia wasiojulikana na mwisho ujiona akili zimekosekana wanaamua kufata ya chadema ili wasishitukiwe.
Chadema washindwe kufanya kwao ndio CCM iige nini? Nyumbu kweli wewe. Kina Grace Kiwelu, Suzan Lymo wamekaa tangia lini ndani ya chadema?
 
Back
Top Bottom