Pre GE2025 CCM waweka ukomo nafasi za ubunge na udiwani viti maalum, waja na kauli mbiu mpya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Naonaa CCM wanapanga mbinu yakugawana ulaji tuu
 
Wakuu,

Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, imefanya kikao chake maalum jana tarehe 10 Machi, 2025 jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Katika kikao hicho, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imepokea na kujadili agenda kuu mbili kama zifuatazo:-

(i). Mapendekezo ya Marekebisho ya Kanuni za Uteuzi wa Wagombea Uongozi katika Vyombo vya Dola toleo la 2022 na

(ii). Rasimu ya Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa 2025-2030

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Kanuni za Uteuzi wa Wagombea Uongozi katika Vyombo vya Dola, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imeridhia mapendekezo ya marekebisho ya Kanuni hizo. Maeneo yaliyofanyiwa marekebisho ni kama ifuatavyo:-

1. Mchakato wa uchujaji na uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge, uwakilishi wa majimbo na udiwani wa kata/wadi.

2. Mchakato wa uchujaji na uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani wa viti maalum wanawake.

3. Upanuzi wa wigo wa idadi ya wajumbe wa vikao vya chama na jumuiya zake watakaopiga kura za maoni. Lengo la hatua hii ni kuimarisha misingi ya demokrasia, uwazi na kupanua uwakilishi wa wanachama wa CCM katika kuwapata wagombea wa nafasi za uongozi katika chaguzi za vyombo vya dola. Utaratibu utakuwa kama ifuatavyo:-

(a) Kwa upande wa wabunge wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) ngazi ya mikoa, kwa upande wa Tanzania Bara

Mkutano Mkuu Maalumu wa UWT wa Mkoa, ambao utakuwa na wajumbe wafuatao :-

(i) Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa UWT wa Mkoa (Kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za UWT).

(ii) Wajumbe wote wa Kamati za Utekelezaji wa UWT za Wilaya.

(iii) Wajumbe wote wa Kamati za Utekelezaji wa UWT za Kata.

Kwa upande wa Zanzibar Mkutano Mkuu Maalumu wa UWT wa

Mkoa, utakuwa na wajumbe wafuatao :-

(i) Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa UWT wa Mkoa.

(ii) Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Wilaya.

(iii) Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Jimbo.

(iv) Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Kata/Wadi.

(v) Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Matawi.

(b) Kwa upande wa Jumuiya ya UVCCM na WAZAZI

Kura za maoni kwa waombaji nafasi za Ubunge/Uwakilishi wa viti maalumu wanawake kupitia Jumuiya ya UVCCM na WAZAZI zitapigwa na wajumbe wa Mikutano Mikuu Maalumu ya Taifa, kwa utaratibu ufuatao:-

Mikutano Mikuu ya Taifa ya UVCCM/WAZAZI itakua na wajumbe Wanawake tu; wajumbe hao ni kama wafuatao

(i) Wajumbe wote wanawake wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa UVCCM/WAZAZI.

(ii) Wajumbe wote Wanawake wa Kamati za Utekelezaji za UVCCM/WAZAZI za Mikoa.

(iii) Wajumbe wote Wanawake wa Kamati za Utekelezai za Wilaya UVCCM/Wazazi.

Ukomo wa viti maalum

Kuweka ukomo wa vipindi viwili vya miaka mitano kwa nafasi za ubunge/uwakilishi na udiwani wa viti maalum wanawake. Ukomo huo utaanza kutumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2030.

Vilevile, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imepitisha Kauli Mbiu rasmi kwa ajili ya kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2025 isemayo;

"KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE"

Kauli mbiu hiyo inaakisi dhamira ya Chama ya kuendeleza juhudi za ujenzi wa Taifa lenye maendeleo jumuishi, mshikamano wa kitaifa na ustawi wa watu wenye kujali UTU.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Issa Haji Ussi (GAVU)
KATIBU WA NEC ORGANAIZESHENI
11 Machi, 2025​
Wanavyuo na neto wapate wawakirishi a.s.a.p
 
Kwa kuwa jambo hilo linatakiwa liingie kwenye Katiba ya chama,kwa Sasa yanabaki kama mapendekezo ya Halmashauri Kuu kwenda kwenye Mkutano Mkuu.
 
Ccm yakubali mapendekezo ya kuweka ukomo wa viti maalum, mihula miwili kuanzia 2030.
 
Marekebisho ya Kanuni za Uteuzi wa wagombea uongozi katika Vyombo vya Dola? Dola ipi hiyo?

Harafu, ukomo kwenye viti maalum ulipaswa kuanza kuhesabiwa kuanzia kwaka 2025 na sio 2030 na wale wamama waliokaa Bungeni tangu 2005 kwa tiketi za Viti Maalumu wazuiwe kugombea tena
 
Safi sana kwa kuweka Ukomo wa viti maalumu.

"KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE"
 
Ni wazo la chadema wamesoma upepo.Unajua kwa nini wanaogopa chadema wakiambiwa hawana akili utumia wasiojulikana na mwisho ujiona akili zimekosekana wanaamua kufata ya chadema ili wasishitukiwe.
Chadema kuna nini cha kujifunza ? Katiba yenu haina ukomo wa cheo cha mwenyekiti wala wajumbe nyie.mnaongea mawazo tu msiyoyafanyia kazi

Lisu alitumia tu hiyo kama gia ya kupata uongozi alivyoshika umesikia akiongelea ukomo wa cheo chake au kuitisha kikao cha kamati kuu wabadili ukomo kwenye katiba?

Kaufyata kimya anawaimbisha wimbo wa kuwapotezea msahau alichoahidi kukifanyia anawaimbisha wimbo wa no reform no election

Keshawapotezea porini huko.mnaimba kama wehu.mumesahau hiyo agenda
 
Back
Top Bottom