Pre GE2025 CCM waweka ukomo nafasi za ubunge na udiwani viti maalum, waja na kauli mbiu mpya

Pre GE2025 CCM waweka ukomo nafasi za ubunge na udiwani viti maalum, waja na kauli mbiu mpya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ingekuwa jambo la maana kama wangeweka ukomo wa utawala wao kama wangeshindwa kihalali na upinzani..Haya mengine ni mbwwmbwe tu!
 
Kuweka ukomo wa vipindi viwili vya miaka mitano kwa nafasi za ubunge/uwakilishi na udiwani wa viti maalum wanawake. Ukomo huo utaanza kutumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2030.

Hii kauli ni hatari,na Haina ukweli na ikianza kutumika,Kuna uwezekano waliokuwa wabunge awali kuchukua Tena fomu kugombea, ili waweze kuanza mfumo huo mpya! CCM hapana😳
 
Hii CCM ya miaka hii, sijui iko wapi tu, mtaani huku husikii watu wakiiongelea kwa madaha au kuipigania, kimekua chama cha vikao vya ndani ndani huko na wanachama wao wakiishi kwa usiri, mtu ana kadi lkn hata mkewe hajawahi itia machoni.Wanaovaa nguo za kijani kwa kujiachia mtaani unakuta ni wale waliojichokea wanavaa sababu walipewa na hawana mavazi ya kutosha.
CCM isome alama za nyakati - hata uwe mzuri vipi watu watakuchoka, ndo hulka ya ubinadamu hiyo--
 
Wakuu,


Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, imefanya kikao chake maalum jana tarehe 10 Machi, 2025 jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Katika kikao hicho, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imepokea na kujadili agenda kuu mbili kama zifuatazo:-

(i). Mapendekezo ya Marekebisho ya Kanuni za Uteuzi wa Wagombea Uongozi katika Vyombo vya Dola toleo la 2022 na

(ii). Rasimu ya Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa 2025-2030

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Kanuni za Uteuzi wa Wagombea Uongozi katika Vyombo vya Dola, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imeridhia mapendekezo ya marekebisho ya Kanuni hizo. Maeneo yaliyofanyiwa marekebisho ni kama ifuatavyo:-

1. Mchakato wa uchujaji na uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge, uwakilishi wa majimbo na udiwani wa kata/wadi.

2. Mchakato wa uchujaji na uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani wa viti maalum wanawake.

3. Upanuzi wa wigo wa idadi ya wajumbe wa vikao vya chama na jumuiya zake watakaopiga kura za maoni. Lengo la hatua hii ni kuimarisha misingi ya demokrasia, uwazi na kupanua uwakilishi wa wanachama wa CCM katika kuwapata wagombea wa nafasi za uongozi katika chaguzi za vyombo vya dola. Utaratibu utakuwa kama ifuatavyo:-

(a) Kwa upande wa wabunge wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) ngazi ya mikoa, kwa upande wa Tanzania Bara

Mkutano Mkuu Maalumu wa UWT wa Mkoa, ambao utakuwa na wajumbe wafuatao :-

(i) Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa UWT wa Mkoa (Kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za UWT).

(ii) Wajumbe wote wa Kamati za Utekelezaji wa UWT za Wilaya.

(iii) Wajumbe wote wa Kamati za Utekelezaji wa UWT za Kata.

Kwa upande wa Zanzibar Mkutano Mkuu Maalumu wa UWT wa

Mkoa, utakuwa na wajumbe wafuatao :-

(i) Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa UWT wa Mkoa.

(ii) Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Wilaya.

(iii) Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Jimbo.

(iv) Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Kata/Wadi.

(v) Wajumbe wa Kamati za Utekelezaji za Matawi.

(b) Kwa upande wa Jumuiya ya UVCCM na WAZAZI

Kura za maoni kwa waombaji nafasi za Ubunge/Uwakilishi wa viti maalumu wanawake kupitia Jumuiya ya UVCCM na WAZAZI zitapigwa na wajumbe wa Mikutano Mikuu Maalumu ya Taifa, kwa utaratibu ufuatao:-

Mikutano Mikuu ya Taifa ya UVCCM/WAZAZI itakua na wajumbe Wanawake tu; wajumbe hao ni kama wafuatao

(i) Wajumbe wote wanawake wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa UVCCM/WAZAZI.

(ii) Wajumbe wote Wanawake wa Kamati za Utekelezaji za UVCCM/WAZAZI za Mikoa.

(iii) Wajumbe wote Wanawake wa Kamati za Utekelezai za Wilaya UVCCM/Wazazi.

Ukomo wa viti maalum

Kuweka ukomo wa vipindi viwili vya miaka mitano kwa nafasi za ubunge/uwakilishi na udiwani wa viti maalum wanawake. Ukomo huo utaanza kutumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2030.

Vilevile, Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imepitisha Kauli Mbiu rasmi kwa ajili ya kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2025 isemayo;

"KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE"

Kauli mbiu hiyo inaakisi dhamira ya Chama ya kuendeleza juhudi za ujenzi wa Taifa lenye maendeleo jumuishi, mshikamano wa kitaifa na ustawi wa watu wenye kujali UTU.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Issa Haji Ussi (GAVU)
KATIBU WA NEC ORGANAIZESHENI
11 Machi, 2025​
RUBBISH. Ukomo wa mahovyo hovyo yote umewekwa kwenye RASIMU ya Warioba, ambayo CCM na serikali yake WANAPIGA CHENGA kuipitisha iwe KATIBA MPYA.
 
Maoni ya wananchi yangeheshimiwa wabunge wote wawe na ukomo katika ubunge,alafu mawaziri wasitokane katika wabunge bali professional itafanya uwajibikaji na kuondoa hii stereotype ya watu flani kujiona kwamba wao ndio wana title deed ya kushika nafasi flani wizarani
 
Ukomo viti maalumu ni vizur uwekwe kwenye katiba moja kwa moja..

Kimsingi CCM na Upinzani wanakubaliana kwenye hilo
Ccm imeonyesha njia hivyo hadi 2030 itakuwa kwenye katiba mambo mdogo mdogo
 
Back
Top Bottom