CCM ya leo na viongozi wake ni uncomfortable kuliko ya Kikwete na ya miaka ya nyuma na wanasumbuliwa na fear of unknown kutokana na chaguzi kuvurugwa

CCM ya leo na viongozi wake ni uncomfortable kuliko ya Kikwete na ya miaka ya nyuma na wanasumbuliwa na fear of unknown kutokana na chaguzi kuvurugwa

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Iko hivi:

Wakati wa Kikwete na Mkapa, CCM waliweza kujipima kupitia chaguzi wanakubalika kwa kiasi gani au wanakaliwa kwa kiasi gani katika maeneo tofauti ya nchi yetu na hivyo kujipanga kutokana na hali halisi inayowakabili kutoka kwa umma.

Ni kweli hata wakati wakati wa Kikwete na Mkapa, chaguzi hazikuwa huru na za haki, ila walau wananchi waliweza kupiga kura na kutoa picha ya namna gani CCM na wagombea wake wanakubalika au kukataliwa ukilinganisha na wale wa vyama vya upinzani hata kama matokeo yaliyokuwa yanatangazwa yalikuwa ni tofauti na uhalisia.

Sasa alipoingia Jiwe, hata tu zoezi la kupiga kura lilivurugwa, hivyo hakukuwa na picha halisi ya ni kwa kiwango gani CCM inaendelea kuporomoka na ni katika maeneo gani na labda ni wapi walikuwa wanaendelea kukubalika hivyo kuwa na takwimu/data zinazotokana na uchaguzi, data ambazo zingewasaidi kujipanga.

Hali leo hiiinawanyima CCM kujitambua na wanakubalika au kukataliwa kwa kiasi gani na katika maeneo gani hivyo hawajielewi ni ni wapi wanapaswa kujirekebisha na kuongeza nguvu na matokeo wanakuwa na fear of unknown.

Kwa kifupi, wamekosa takwimu za kiuchaguzi ambazo zingeweza kuwasaidia walau kujipanga na matokeo yake wanasumbuliwa na fear of unknown.

Hivyo, mkiona wanasambaz mabango ya picha za Raisi katika kipindi hiki ambacho sio cha kampeni, basi mjue hiyo ni moja ya madhara yatokanayo na hii fear of unknown inayowatesa na bado tutashuhudia mengi tu ya kushangaza katika siku zijazo.
 
Hawajui haki huinua taifa, na haki itawaweka huru🤔 .
Takwimu za uchaguzi ni muhimu sana kwa vyama vya siasa kujitathimimi, takwimu ambazo leo hazipo kwasababu tu kuna mtu aliwatishia wakurugenzi/wasimamizi wa uchaguzi kuwa hawezi kuwalipa mishahara na kuwapa magari ya kutembelea halafu wamtangaze mpinzani mshindi.
 
Hapo walipo wanalazimisha kila rais aendapo kuwe na watu kibao. Matokeo yake wanamwaga fedha nyingi sana, na makundi mengine kama wanafunzi, wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za umma hulazimishwa kuhudhuria ili kuficha hiyo aibu ya kukosa watu. Alichokifanya Magufuli kitasababisha idadi ya wapiga kushuka kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea ndani ya nchi hii.
 
Na ndio maana Samia akienda kufanya ziara anatumia mamluki ili kujaza watu🤣🤣

Mfano , juzi apo mkoani mara wanafunzi wa chuo Fulani walisimamishwa masomo Yao ili kumpokea chief hangaya 🤣 🤣🤣☘️
 
Back
Top Bottom