CCM ya Samia, humkosoi ila ukiutaka Urais, Unaliwa Kichwa. Huutaki Urais ila Ulikosoa utendaji, Unaliwa Kichwa pia!

CCM ya Samia, humkosoi ila ukiutaka Urais, Unaliwa Kichwa. Huutaki Urais ila Ulikosoa utendaji, Unaliwa Kichwa pia!

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2017
Posts
29,314
Reaction score
93,919
Wakuu tuwachukulie Watu Hawa

Makamba na Mpina kama ndo Subjects wetu.

Siasa za Makamba, zilijikita kwenye Harakati za chini chini, hakua anamkosoa Rais Samia kwenye Vyombo vya habari, in fact Makamba alikua anamsifia sana Samia Kuna Ile speech yake ya 'Hilo tu Mh Rais inatosha kukufanya uendelee kua Rais Hadi 2030'.

Makamba Kwa Kuufikiria Urais, HATIMAYE KALIWA KICHWA.

ON the other hand, Kuna MPINA, yeye hajawahi kua na interests zozote na Urais, hakuwahi mponda RAIS Samia kimya kimya, Yeye alijitokeza waziwazi, Bungeni, Vyombo vya habari, Mahakaman, Mikutanoni, kupinga waziwazi baadhi ya mambo ambayo sio tu MPINA aliona ni mabaya Kwa Taifa Bali Wananchi wote waliona hivo pia.

Lakini naye KALIWA KICHWA wakuu🤣.

Sio jambo la kucheka, ila unaweza jiuliza, huyu Mwenyekiti wa CCM, Mwanamama, na Rais, Anataka CCM ya aina gan??.

Binafsi, suala la kutaka Urais sio inshu, ukoshakua Kiongozi, lazima uwaze nafasi za juu zaidi.

Haya Kukosolewa pia sio inshu.

Anataka watu wa aina gani?? Yaan usikosoe na usionyeshe Nia ya kuutaka Urais??. Kifupi uwe MBUMBUMBU?🤣🤣🤣.

LILE SWALI LA KWANINI MAGUFULI HAKUTAKA KABISA KABISA SAMIA KUA MAKAMO, NA ALIMTAKA MWINYI, NADHAN MAJIBU TUNAZIDI KUYAPATA.

Huwa ni hatari sana hata Makazini kuongozwa na MTU Mjinga, mjinga hajiamin, mjinga Silaha yake ni kutumia nguvu kama ana hiyo Mamlaka , mjinga Silaha yake ni Uchawi , Mjinga Yuko Radhi KUUA ili mradi tu abakie kua Boss wa Taasisi.
 
CCM hii inataka mafisadi na wezi pamoja na machawa.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom