CCM yaamua kutuma meseji kwa kila Mtanzania kuwakataa wanaopinga mkataba wa kuuzwa kwa bandari zetu

CCM yaamua kutuma meseji kwa kila Mtanzania kuwakataa wanaopinga mkataba wa kuuzwa kwa bandari zetu

Mimi haijanifikia hiyo sms. Ikifika nawabloku
 
Hata watume message suala hili limeichafua sana Serikali ya CCM. Waking'ang'ania na kuipitisha ndiyo itakuwa mwisho wa CCM. Jambo hili wangeachana nalo. Sasa hivi wananchi ni waelewa sana.
 
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Daniel Godfrey Chongolo kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndg. Samia Suluhu Hassan, anakupongeza Ndg. John Keshokutwa Madenge kwa kuwa mstari wa mbele kukataa wapotoshaji wanaopinga hatua za uboreshwaji wa huduma za Bandari, kama ilivyoelekezwa kwenye Ilani ya CCM.

Chama kitaendelea kuisimamia Serikali itekeleze Ilani ili kutengeneza fursa za maendeleo kwa ajili ya Watanzania wote.

TunaImaniNaSAMIA
Wajinga wanapoteza muda wao. Hapo ndiyo utajua kuwa ndani ya CCM, tena fikiria huyu ni katibu Mkuu, kuna watu wenye uelewa duni kiasi gani.

Sasa meseji ya kipuuzi kama hiyo inabadilisha nini? Yaani unamtumia mtu ambaye huujui hata uelewa wake, yumkini ana uelewa wa kukuzidi wewe maradufu!

Yaani mjinga anataka kuwa mwalimu wa mwerevu!
 
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Daniel Godfrey Chongolo kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndg. Samia Suluhu Hassan, anakupongeza Ndg. John Keshokutwa Madenge kwa kuwa mstari wa mbele kukataa wapotoshaji wanaopinga hatua za uboreshwaji wa huduma za Bandari, kama ilivyoelekezwa kwenye Ilani ya CCM.

Chama kitaendelea kuisimamia Serikali itekeleze Ilani ili kutengeneza fursa za maendeleo kwa ajili ya Watanzania wote.

TunaImaniNaSAMIA
Huu ni ujuha kabisa
 
Sijapata, labda itakua imeenda kwenye block list moja kwa moja...
 
Back
Top Bottom