William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,400
inwezekana yumo kwenye tuhuma, lakini ni mtu mwenye msimamo kwenye mambo abayo, hayaendani na utashi wa mwenyekiti eg kukemea OIC, sasa hao wengine sifikiri watakuwa na uwezo huo etc.
Mkuu,
Nina issues na hizi dataz.
Moja, kwani Umoja wa Vijana, kama ilivyo katika vyombo, vikao, na ngazi zingine za CCM, hawana utaratibu wa kuwa na viongozi tofauti kutoka bara na visiwani ? Itawezekanaje Rais ajiamulie kushauri eti wagombea wote watoke Zanzibar ?
Mbili, Kikwete amewezaje kutamka CCM kuna rushwa ? Hiyo kwake ni kukubali machafu ya chama tawala, na akitoa madai hayo anaweza kubanwa achukue hatua kwa kutumia ushahidi ambao atadaiwa, maana rushwa ni kosa la jinai. Kikwete atawezaje kweli kutangaza CCM kuna rushwa ?
Tatu, umetuambia kwamba CCM watasikiliza rufani ya Nape. Lakini hapo hapo umetoka kutuambia kwamba CCM wameshaamua, wameshapitisha kwamba ni Wazenji tu ndio watakaogombea. Hapo unaona pamekaa sawa kweli ?
Nne, Kikwete hawezi kumuongelea mtoto wake kwenye kikao cha Central Committee. Hususan kumuhusisha na rushwa. Ni kitu bizarre!!!
Tano, kuna thread ilianzishwa kabla inasema imekuwaje kikao cha CCM kimefanyika Ikulu. Wewe ukakimbia kutafuta "dataz" kali zaidi lakini zilipofika zikaonekana kama dead on arrival kwa sababu zilidai kikao kimefanyika Dodoma, hadi Wakuu kina Masatu walipokushtua. Ulichanganya vipi data hapo?
Unaona matatizo ya "dataz" zako ?
Sasa anza mashambulizi lakini I hope unaelewa kwa nini wengine huwa tunakataa kuzimeza nzima nzima.
Soma HAPA.Ubishi mwingine ni for the sake ya kubisha tu.Could you be gentleman enough na kukiri kuwa ulichemka ku-criticize kabla hujawa na data za kutosha?
Simpe rule ya criticism iko hivi:usikosoe kitu ambcho wewe mwenyewe huna data za kutosha kuhusu unachokikosoa.
Mmeacha kuzungumzia kushindwa kwake kuliongoza Taifa kwenye suala la wizi wa fedha za EPA mmebakia kuimba nyimbo za CCM. Hivi mnafikiri ni bahati mbaya kwa NEC kukutana siku moja baada ya suala la EPA na kuja na maamuzi mazito?
a. Kule kulikoibiwa fedha kwa mabilioni hakuna mtu aliyetimuliwa, kuitishiwa kikao wala nini
b. Kule ambako hakuna wizi wowote ule wala kughushi watu ndio inadaiwa hata kupoteza kazi watapoteza.
Tukisema Ibara 15:1 Iko kazini watu wanasema tunaionea CCM.
MM,
I am with you on this, jamaa wa CCM wanawachanganya watu tu na kuondoa attention kutoka katika issue zinazohitaji immediate attention kama EPA na kutuletea hizi spin za UVCCM.
Tunawaangalia tu walivyoishiwa nyimbo.
Mkuu BAK, heshima mbele.
Haya unayoandika na kuzungumza una weza kututhibitishia?
"Mnyonge mnyongeni na haki yake mpeni"
Rome haikujengwa kwa siku moja, na haya ni maoni yangu reading this situation na ninaweza nikawa wrong pia, na soon tukizipata dataz za mwisho kikao tutaziweka hapa.
Ahsante Wakuu!
Soma HAPA.Ubishi mwingine ni for the sake ya kubisha tu.Could you be gentleman enough na kukiri kuwa ulichemka ku-criticize kabla hujawa na data za kutosha?Simpe rule ya criticism iko hivi:usikosoe kitu ambcho wewe mwenyewe huna data za kutosha kuhusu unachokikosoa.
Labda uweke record yake kwa taifa amewahi kutufanyia nini hasa cha kumfanya awe tofauti na wengine mafisadi waliotajwa na Dr. Slaaa? au?
Kaka Tatizo ni kuwa CCM haijengi bali INABOMOA kilichojengwa na TANU....
ukitaki kulinganisha linganisha vilivyo katika kundi moja yaani ccm, kwa hiyo katika kuona kwangu kati ya hao waliopitishwa kwa ajili ya mwenyekiti wa wazazi, na muona huyo ni bora kuliko hao wengine. licha ya ufisadi wake.
Sawa sawa, hakuna ugomvi kaka hapa tunajadili siasa tu ndugu yangu,
kama unasema licha ya ufisadi wake Mkono ndiye anayefaa, unataka niseme nini tena si umemaliza mkuu the genius wetu JF? au? Bwa ! ha!ha! ah! ah! ah!hasira hasara kaka!
Kuhusu kutofautiana kimawazo kwa mada zitolewazo. Nadhani kutofautiana kulikuwepo, kupo na kutaendelea kuwepo. Hivyo mkuu sio kila mtu anayetofautiana nawe basi ana nia mbaya. Kumbuka uono wako wewe Mkuu sio sawa na uono wa Mfumwa. Tunaweza wote tunaangalia mbele, kumbe mmoja ana ona km 6, mwingine km 3. Hivyo tuendeleze forum yetu kwa hoja.
una jua ndugu yangu mimi mambo ya sifa sinayo wether nipo genius au nafahamiana na watu na hapa najizui kutaja majina sababu itakuwa ni kutaka hizo sifa amazo hazina maana na pia najizui kusema wewe unajuana saana na fulani na fulani maana itakuwa ni kukukashifu ,( hayo ni ya kwangu) na kila binadamu ana uzuri/na ubaya wake , hivyo nakuomba kwa ustaarabu tu especially ukinijibu mimi mambo yanayo reflect hayo usiya weke, maana nakuheshima kama ulivyo, kama weakness unazo ni zako, nikikucheka au kukununia haitasaidia, kwa hiyo mimi nitachukua yalio mazuri yako, na mapungufu yako nitayaacha kama yalivyo, na ikibidi kukushauri nitafanya hivyo kwa ustaarabu tu either kwa uwazi or kwa chati/pembeni kwa sababu na wewe ni binadamu hivyo unahitaji misaada/michango ya wengine kuboresha ulicho nacho.
Field Marshall Es,
Mkuu pamoja na kwamba mimi sio ktk kundi la wafuasi wa chama CCM, ningependa unifahamishe kidogo kuhusiana na hawa vijana waliochaguliwa toka Zanzibar... je, hawa wamechaguliwa kutokana na sifa zipi za uongozi au ndio ktk kuwavuruga tu Mafisadi..
Sijui kama umewahi kufikiria hili wakati ukimpongeza mkulu, lakini Mwenyekiti wenu siku zote ameonyesha dalili mbaya sana ktk uteuzi wake..mara nyingi huteua watu ili kumkomesha mtu mwingine, yaani kuna husda zilizojengwa hivyo kuondoa mzizi wa fitna hutafuta mganga nani kumwondoa mchawi..ndio maana baraza lake la kwanza la mawaziri lilikuwa Hovyoo, tazama Makamba na baadhi za teuzi zake ktk wizara nyeti kote wamejaa watu ambao kusema kweli hawakuwa na uwezo ktk utendaji kazi ila uwezo ktk kuweka vijembe na kufagia njia za mafisadi..
Sasa ikiwa changes haziwezi kutokea ndani ya uongozi wa serikali, zikafuatia ndani ya chama itakuwa vigumu sana kufanya mabadiliko yoyote ya ndani Washington yetu..sura zile bado zipo ndani na zinaendesha nchi!
Kusema kweli picha nzima inanipa kuwa chaguzi hizi hazikulenga uwezo wa watu hao kuongoza ila kuangamiza watu fulani...